Pages

ELIMU KWANZA.

ELIMU KWANZA.
FEDHA SIO KIPAUMBELE CHETU.

Saturday, 11 January 2014

TUNAJIFUNZA NINI KWA HABARI YA LAZARO ALIYEFUFULIWA NA BWANA YESU


Mtumishi Gasper Madumla.
Karibu tuendelee kujifunza zaidi siku ya leo,ikiwa leo ni siku ya nne ya fundisho hili.
Tunajifunza mambo mengi sana kupitia habari ya Lazaro wa Bethania mwenyeji wa mji wa Mariumu,yule aliyefufuliwa na Bwana Yesu.Yapo mambo ambayo ni msaada kwetu,na kupitia hayo tutavuka,
Basi nakusalimu katika jina la Bwana Yesu;
Bwana Yesu asifiwe…
Karibu tuendelee...
Na hapa tunasoma;
"Basi Martha akamwambia Yesu,Bwana,kama ungalikuwepo hapa,ndugu yangu hangelikufa. Lakini hata sasa najua ya kuwa yo yoyote utakayomwomba Mungu,Mungu atakupa.Yesu akamwambia NDUGU YAKO ATAFUFUKA."Yoh:21-22.

Imani ya Martha inaonekana wazi wazi ya kwamba ilikuwa ni imani iliyomtegemea Bwana Mungu kwa kiwango kikubwa sana,maana tazama asemapo"Bwana,
kama ungalikuwapo hapa,ndugu yangu asingalikufa"
Alichokiamini Martha ni kwamba Bwana Yesu ana uwezo mkuu wa kuponya ugonjwa wa Lazaro au alichokiamini Martha ni kwamba Bwana Yesu ni mwenye UWEZA hata kusimamisha mauti isimtokee ndugu yake Lazaro.

Haleluya...

Jambo kubwa tunalojifunza hapa ni kwamba,
Kama Bwana angalikuwapo kwako basi usingalikufa kiroho.

Watu wengi leo wameshajifia zao muda mlefu,hali wakionekana bado wakitembea,sababu Bwana hakuwapo mioyoni mwao. Maisha nje ya Bwana ni kutembea huku ukiwa ni mfu kiroho,sababu uzima wa kweli hupatikana ndani ya Bwana Yesu tu.

Ifike wakati sasa nasi tuseme,
"Bwana kama angalikuwapo hapa (ndani yetu)basi tusingalikufa.
Yeye Bwana uhuisha,
Huweka uzima pasipo uzima,
Huponya mahali uonapo hapaponyeki,
Yeye Bwana ndiye njia,uzima na kweli.

" Kwa maana ndani yake Yeye tunaishi,tunakwenda,na kuwa na UHAI wetu." Matendo 17:28

Oooh...Yesuu,mwana wa Daudi uturehemu. Tupate kuyajua hayo.
Ooooh... Ninawiwa...
Fungua moyo wako,upokee hii.

Nimeipenda kauli ya Martha yenye kutambua udhihilisho wa nguvu za Bwana Yesu. Martha alizidi kuamini kwamba,yo yoyote yale ambayo Bwana Yesu ataomba,yatajibiwa. Hakuwa na shaka na hilo.

Sasa sikia Bwana Yesu asemavyo;
"Ndugu yako atafufuka."
Ooh,
Kumbe kufufuka kupo.
nami nikisomaga hapo ninatiwa nguvu juu ya mambo yangu yaliyokufa,maana Bwana Yesu atayafufua.
Haijalishi yamekufa wakati gani,
Haijalishi ni jambo gani lililokufa,
Haijalishi ni mambo ya namna gani,
Nasema haijalishi hata ukubwa wa mambo yaliyokufa,
Lakini mimi najua jambo moja tu,kwamba Bwana atayafufua.

Nami ninakuambia wewe kwamba;Bwana atafufua kila ufu ulio ndani yako.
Yamkini upo ufu ndani yako,
Yamkini usongi mbele kiroho sababu ya umauti wa kiroho ndani yako,
Yamkini hata biashara yako imekufa,
Yamkini tumbo la uzazi li ufu,
Yamkini kila uzaapo mtoto hufa,
Haijalisha hayo yote,BWANA ANAKWENDA KUFUFUA LEO.

Leo lipo neno mahali hapa lisemalo kila kilichokufa KITAFUFULIWA maana Bwana yu hai.
Tumesoma hapo neno linasema,Bwana asema kwako,
“NDUGU YAKO ATAFUFUKA.”
Yamkini mtoto,mume,mke wako amekufa kiroho au hata kimwili,Bwana asema ATAFUFUKA.
Sikia ;
Ikiwa Lazaro yeye aliyekuwa kaburini siku NNE ,akafufuliwa,basi si zaidi sana kwako wewe?
Jambo moja ninalolijua siku ya leo ni kwamba ni kuamini neno la Bwana,kwamba Bwana atafufua kila kilichokufa.
Leo tumeisikia sauti ya Bwana,isemavyo;
“NDUGU YAKO ATAFUFUKA!”

Hili ni neno la kinabii siku ya leo,Nami ninalipokea,sababu hata mimi ninao ndugu wafu.
Bwana asema neno moja tu,kwamba WATAFUFUKA.
Swala la kufufuka ni la Bwana,wewe ni kuamini na kulipokea,wala huitajiki ufanye lolote lile,ni kuamini tu.

"Filipo akasema,Ukiamini kwa moyo wako wote,inawezekana..."Matendo 8:37.

Ndugu yako atafufuka,
Roho yako itafufuka,
Maisha yako yatafufuka.
Katika huo mstari wa 23,pale Yesu alipomwambia Martha ndugu yako atafufuka,unajua ilikuwa sio jambo dogo,
Kauli hiyo ni ngumu kuaminika kwa mtu wa kawaida,maana ukweli kwa macho ya kibinadamu jambo hili,au tamko hili la Bwana Yesu aliwezekani.
Yesu alimjibu Martha jambo kubwa sana ambalo hata yeye alipokeaye ni lazima awe ni mtu wa rohoni.

*Kumbe yapo maneno ya uzima yatamkwayo mbele yetu,lakini shida yetu ni namna gani ya kujiungamanisha nayo…
Najua yapo mambo yaliyokufa kwako,yawezekana roho yako i mfu,Biashara yako i mfu,N.K

• Nami natangaza fursa ya kipekee kabisa kwako,ikiwa bado hujampokea Bwana Yesu kuwa Bwana wa maisha yako,ili Yeye aje na kufufua roho yako,basi muda ndio huu wa kuokoka.
Au ikiwa yapo mapo yaliyokufa kwako,basi kwa mambo hayo yote,usisite kunipigia simu hii;

• 0655-111149

ITAENDELEA…
UBARIKIWE.

No comments:

Post a Comment