Pages

ELIMU KWANZA.

ELIMU KWANZA.
FEDHA SIO KIPAUMBELE CHETU.

Saturday, 7 December 2013

KILI STARS YAIVUA UBINGWA UGANDA NA KUTINGA NUSU FAINALI - KUKIPIGA NA HARAMBEE DEC 10


Timu ya Kilimanjaro Stars leo hii imefanikiwa kufuta uteja kwa Uganda baada ya kuifunga timu hiyo katika mchezo wa robo fainali ya kombe la CECAFA Challenge Cup.

Mchezo huo wa robo wa fainali uliochezwa jioni ya leo Kili Stars imefanikiwa kuivua ubingwa The Cranes na kuingia robo nusu fainali baada ya kushinda mikwaju ya penati 3-2 huku kipa Ivo Mapunda akiibuka kuwa shujaa.

MATOKEO EPL: MAN UNITED HALI YAZIDI MBAYA YAPIGWA NA NEWCASTLE - CHELSEA NAYO CHALI - MAN CITY YAKAZIWA


Manchester United 0-1 Newcastle
Southampton 1 – 1 Manchester City,
Liverpool 4 – 1 West Ham United,
Stoke City 3 – 2 Chelsea
West Brom 0 - 2 Norwich
Palace 2 – 0 Cardiff

WANACHAMA SIMBA KUTINGA BUNGENI JUMANNE.


WANACHAMA wa klabu ya Simba wanaompinga Mwenyekiti wa klabu hiyo, Ismail Aden Rage wataelekea mjini Dodoma Jumanne kwa ajili ya kuonana na Spika wa Bunge hilo, Anna Makinda kuelezea namna Mwenyekiti huyo anavyovunja Katiba ya klabu hiyo.
Awali wanachama hao walipanga kuondoka leo kwenda Dodoma ili kesho Jumatatu waonane na spika lakini wamehairisha kutokana na kesho kuangukia siku ya Uhuru ambapo watu awaendi makazini.
Akizungumza jijini Dar es Salaam kwa niaba ya wanachama wenzake, Katibu wa tawi la mzambalauni,

Thursday, 5 December 2013

'MATOKEO MABAYA HAYATOTUATHIRI KIBIASHARA - TUNA UWEZO WA KUSAJILI WACHEZAJI WATANO' - ASEMA BOSS WA MANCHESTER UNITED


CEO wa klabu ya Manchester United Ed Woodward amesisitiza kwamba klabu yao haihitaji kuendelea kushinda mataji ili kuweza kuendela kuvutia wadhamini.


United imeweza kupunguza kwa kiasi kikubwa deni lao kutoka na kuongezeka kwa wadhamini wengi kwenye klabu hiyo.

MAKALA ;HISTORIA YA MANDELA.



Miaka ya Mapema
1952


Rolihlahla Mandela, mwanawe chifu, alizaliwa katika kijiji kimoja kiitwacho, Mvezo katika mkoa wa Eastern Cape nchini Afrika Kusini tarehe 18 Julai mwaka 1918. Alikuwa mtu wa kwanza katika familia yake kwenda shule. Mwalimu ambaye hata hangeweza kutaja jina lake vyema, alizoea kumuita Nelson. Alitoroka mjini Johannesburg mwaka 1941 ili kuepuka kulazimishwa kuoa mapema. Alikutana na Walter Sisulu aliyemsaidia kupata kazi katika kampuni ya ya Witkin Sidelsky na Eidelma. Pia alijiunga na chama cha (ANC)
1 kati ya 10



Kesi ya Uhaini
1956


Mandela alifuzu kama wakili na kuanzisha kampuni ya kwanza ya sheria inayomilikiwa na mtu mweusi mwaka 1952 na kuiendesha kwa ushirikiano na Oliver Tambo, na kutoa huduma za kisheria kwa wale ambao walikosa uwakilishi. Akihofiwa kupigwa marufuku na serikali ya ubaguzi wa rangi, ANC ilimtaka Mandela kuhakikisha kuwa chama hicho kinaweza kuendesha harakati zake kimya kimya. Alikamatwa mwaka 1956 na kufunguliwa mashtaka ya uhaini yeye pamoja na wenzake 155. Baada ya kesi yake iliyochukua miaka minne, ilitupiliwa mbali . Mnamo mwaka 1958, Mandela alimuoa Winnie Madikizela.



Kufungwa Maisha
1964


Sheria ya hali ya hatari ilitangazwa baada ya polisi kuwaua waandamanaji 69 mjini Sharpville mwaka 1960. Serikali ilihofia kuwa wangelipiza kisasi na hivyo kuharamisha chama cha ANC. Chama hicho baadaye kiliendesha harakati zake za kijeshi kichinichini wakiongozwa na Mandela.Mwaka 1962, Mandela alikamatwa kwa kosa la kuondoka nchini bila kibali. Wanachama wengine wa ANC walikamatwa. Akiwa jela Mandela alishtakiwa kwa kosa la hujuma. Yeye na wengine saba walihukumiwa jela katika kisiwa cha Robben mwaka 1964



Huru hatimaye
1990
Jamii ya kimataifa iliiwekea vikwazo zaidi serikali ya ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini. Vikwazo vya kwanza viliwekwa mwaka 1967.Shinikizo zilizaa matunda na mnamo mwaka 1990, rais FW De Klerk akakiondolea marufuku chama cha ANC. Tarehe 11 Februari, Mandela aliachiliwa baada ya miaka 27 jela. Umati wa watu ulimshangilia huku yeye pamoja na mkewe wakiondoka sehemu ya jela. Katika mkutano wa kwanza wa chama cha ANC mwaka uliofuata, Mandela alichaguliwa kama kiongozi wa chama .Mazungumzo yakaanza ya kuunda serikali ya pamoja ya waafrika weusi na wazungu.



Tuzo ya amani ya Nobel
1993


Mnamo mwaka 1993, Mandela na rais wa nchi hiyo wakati huo, walituzwa tuzo ya amani ya Nobel kwa juhudi za kuleta uthabiti Afrika Kusini. Akikubali tuzo hiyo, Mandela alisema kuwa '' tutafanya kila tuwezalo kuweza kuleta mageuzi duniani.''



Rais mpya
1994
Mnamo mwaka1994,kwa mara ya kwanza katika historia ya Afrika Kusini, watu wa rangi zote walipiga kura katika uchaguzi huru na wa kidemokrasia. Mandela alichaguliwa. Akihutubia umma, katika sherehe ya kuapishwa kwake, tarehe 10 mwezi Mei, mwaka 1994, alisema: "uhuru utawale, Mungu aibariki Afrika!'' Tatizo lake kubwa lilikuwa ukosefu wa nyumba za kutosha kwa watu maskini na mitaa ya mabanda iliendelea kuongezeka.Thabo Mbeki alichukua uongozi wa nchi huku Mandela akiuza sera za nchi hiyo kimataifa.



Akitoka Robbben
1995


Kuadhimisha miaka mitano baada ya kuachiliwa kwake, Nelson Mandela alizuru kisiwa cha Robben mwezi Februari mwaka 1995 alikozuiliwa kwa miaka 18. Ziara yake ilikuwa mwaka 1956 mwezi Februari pamoja na wafungwa wenzake waliowahi kufungwa kisiwani humo na kufanya kazi ngumu. Mapafu ya Mandela yanasemekana kuathirika alipokuwa anafanya kazi katika machimbo ya mawe.



'Usiniite''
2004


Thabo Mbeki alichukua mamlaka kutoka kwa Mandela kama kiongozi wa chama tawala ANC na hata kushinda uchaguzi wa mwaka 1999.Mandela alimuoa Graca Machel, mjane wa aliyekuwa rais wa Msumbiji, akiwa na miaka 80. Aligunduliwa kuwa na saratani ya Tezi Kibofu na hivyo kuanza matibabu.Mnamo mwaka 2004, alitangaza kujiuzulu, akisema kuwa anataka maisha ya kimya nyumbani kwake na familia yake. Kwa mzaha aliwaambia wandishi wa habari wasimpigie simu.



Sherehe ya siku ya kuzaliwa kwake
2008


Wanamuziki, waigizaji na wanasiasa waliungana na Mandela katika sherehe kubwa uwanja wa Hyde Park mjini London kusherehekea miaka 90 ya kuzaliwa kwake. Akiongea na wale waliofika, aliwaambia, ''ni wakati kwa kizazi kipya kuchukua uongozi, kibarua kwenu sasa.''



Kuugua
2010


Mandela aliweza kuonekana hadharani mara kadhaa baada ya kustaafu. Ingawa alionekana katika sherehe ya kukamilika kwa dimba la kombe la dunia mwaka 2010 nchini humo. Januari mwaka 2011, alilazwa hospitalini kwa ukaguzi maalum, huku serikali ikiwakumbusha watu kuwa aliwahi kupata matatizo ya kupumua. Alipokea matibabu ya ugonjwa wa mapafu mwaka 2012 na pia mwaka 2013 .

nawww.hakileo.blogspot.com

Tuesday, 3 December 2013

Kilimanjaro Stars Yatua Salama Nairobi Timu ya Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars) imewasili salama Nairobi, Kenya tayari kwa


Timu ya Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars) imewasili salama Nairobi, Kenya tayari kwa mashindano ya Kombe la Chalenji yanayoanza kesho (Novemba 27 mwaka huu) katika Uwanja wa Nyayo.

Kilimanjaro Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager iliwasili saa 3 usiku kwa ndege ya RwandAir, na imefikia katika hoteli ya Sandton iliyoko katikati ya Jiji la Nairobi.

Kwa mujibu wa programu ya Kocha Mkuu Kim Poulsen, Kilimanjaro Stars leo (Novemba 26 mwaka huu) ni mapumziko ambapo kesho itafanya mazoezi kujiandaa kwa mechi yake ya kwanza dhidi ya Zambia itakayochezwa Novemba 28 mwaka huu Uwanja wa Machakos.

ZANZIBAR HEROES YAPIGWA NA KENYA - HATARINI KUAGA MASHINDANO YA CHELLENJI




Na Baraka Mpenja wa Fullshangwe.COMMICHUANO ya kombe la Mataifa ya Afrika mashariki na kati, CECAFA Challenge imezidi kushika kasi leo nchini Kenya ambapo wenyeji Kenya wameungana na Wahabeshi wa Ethiopia kutinga hatua ya robo fainali baada ya kuifumua Zanzibar Heroes mabao 2-0, Uwanja wa Afrah, Nakuru.

Alikuwa ni Beki wa Azam fc, inayoshiriki ligi kuu Tanzania bara, Joackins Atudo aliyekuwa wa kwanza kuandika bao la kwanza dakika ya 6 na baadaye mshambuliaji wa AFC Leopards ya Kenya, Allan Wanga akaandika kimiani bao la pili dakika ya 60.

Monday, 2 December 2013

Taarifa kamili ya Kocha mpya wa Simba Sc


Mashabiki wa Timu ya Simba, walimpokea kwa shangwe na nderemo, kocha wao mpya aliyetua nchini jana machana.

Kocha huyo akikabidhiwa taji la maua na mashabiki baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Julius Nyerere Dar.

Kumekuwa kukitokea furaha kwa mashabiki, viongozi na hata wachezaji wa Klabu zetu kubwa hapa nchini, wakati wanapokuwa wanamkaribisha Kocha au Mchezaji mpya kwa kumtambulisha kwa mbwembwe nyingi, lakini anapotokea kakosea kidogo haijalishi ni muda gani amekwisha kaa na Klabu husika,anaweza kutimuliwa ama kuanzishiwa mizengwe hadi akakata tamaa ya kuonyesha yale yote aliyojiandaa nayo kuifanyia Klabu husika.



Kocha mpya wa Simba SC, Mserbia Zdravko Lugarusic amesaini Mkataba wa miezi sita mbele ya Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe leo mchana Mbezi, Dar es Salaam.

Snura kuachia wimbo wake mpya hivi Karibuni 'Ushaharibu'

Hitmaker wa Majanga 'Snura', anatarajia kuja na wimbo mpya utakaoitwa “Ushaharibu”.Wimbo huu utakuwa ni muendelezo wa nimevurugwa.

KIINGILIO MECHI YA TANZANITE 1,000/



Washabiki watakaoshuhudia mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia kwa wasichana wenye umri chini ya miaka 20 kati ya Tanzania (Tanzanite) na Afrika Kusini watalipa kiingilio cha sh. 1,000.

Mechi hiyo ya kwanza ya raundi ya pili ya michuano hiyo itachezwa Jumamosi (Desemba 7 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni.

Matola: Simba, Yanga badilikeni

KOCHA wa kikosi cha Simba B, Selemani Matola, amezitaka klabu za Simba na Yanga kuachana na mtindo wa kusajili wachezaji wale wale na sasa zijikite kuwapandisha vijana kutoka vikosi vya vijana.
Matola ameliambia Mwanaspoti kuwa kuna haja ya klabu hizo kubwa nchini kuona ni jinsi gani zinawasajili vijana badala ya kuendelea na mfumo wa kubadilishana tu wachezaji bila ya kufanya usajili wa maana.

Toure ndiye bora zaidi Afrika




Yaya Toure aliteuliwa mara tano kuwania tuzo hili lakini akafanikiwa kushinda mwaka huu

Yaya Toure ametangazwa mshindi wa tuzo ya BBC ya mwaka 2013 ya mchezaji bora zaidi wa soka barani Afrika.

Mchezaji huyo wa Ivory Coast, na ambaye pia ni kiungo wa klabu ya Manchester City ya Uingereza, na ambaye jina lake limekuwepo kwa miaka minne iliyopita katika orodha ya wachezaji wanaowania tuzo, aliwashinda Pierre-Emerick Aubameyang, Victor Moses, John Mikel Obi na Jonathan Pitroipa, katika kuibuka mshindi.