Pages

ELIMU KWANZA.

ELIMU KWANZA.
FEDHA SIO KIPAUMBELE CHETU.

Wednesday, 29 January 2014

‘KOCHA GUNDU’ AISHUSHA YANGA KILELENI, TANGU AMEKUJA MECHI NNE TIMU IMESHINDA MCHEZO MMOJA TU TENA KWA TAABU

Na Prince Akbar, Tanga
MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Yanga SC wameshushwa kileleni mwa ligi hiyo leo kufuatia kulazimishwa sare ya bila kufungana na Coastal Union Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
Matokeo hayo yanaifanya Yanga itimize pointi 32 baada ya kucheza mechi 15 na kuipisha Azam FC kileleni, ambayo imetimiza pointi 33 baada ya kuifunga Rhino Rangers bao 1-0 leo.
Mchezo ulisimama mara mbili kwa dakika moja na ushei ili kupisha zoezi la uokotaji wa chupa za maji zilizojazwa mikojo na tupu zilizorushwa uwanjani na mashabiki wa timu hizo.

Ubingwa itawezekana? Hans van der Pluijm ameishusha kileleni Yanga SC baada ya mechi mbili tu za Ligi Kuu

Monday, 27 January 2014

ARSENAL WAINGIA MKATABA MPYA MNONO NA PUMA

KLABU ya Arsenal imetangaza kuingia Mkataba wa muda mrefu wa udhamini wa vifaa vya michezo na kampuni ya Puma kuanzia Julai mwaka 2014.
Pamoja na hayo hakuna kiwango cha fedha cha udhamini huo kilichothibitishwa Jumatatu, ingawa dili hilo linatajwa kama kubwa zaidi katika historia ya uhusiani wa Puma na Arsenal.
Inafahima Washika Bunduki hao wanapokea kiasi cha Pauni Milioni 30 kwa mwaka kutoka kwa wadhamini wakuu, shirika la ndege la Emirates, na imeripotiwa dili hilo jipya litakuwa sawa na lile ambalo Puma walitoa wakati wanaiponya timu hiyo Nike, waliokuwa wadhamini wa Arsenal tangu 1994.

Hii ni jezi mpya ya Arsenal? Thierry Henry akiwa na Bacary Sagna, Linford Christie na Olivier Giroud

Hii iko hivi! Picha ya jezi mpya ya Arsenal, ambayo ni sawa na ile aliyokuwa anavaa Henry, imevuja kwenye Twitter

Mtendaji Mkuu, Ivan Gazidis (kulia) akipeana mikono na Mtendaji Mkuu wa Puma, Bjoern Gulden


Dili imetiki: The Gunners imetangaza kuingia Mkataba wa muda mrefu na Puma katika Mkutano na Waandishi wa Habari Jumatatu

MSAINII WA TWANGA PEPETA MCD AMEFARIKI DUNIA.


MPIGA tumba namba moja katika muziki wa dansi hapa nchini Soud Mohamed MCD wa Twanga Pepeta amefariki dunia usiku huu mjini Moshi.
MCD alikuwa huko kwa zaidi ya miezi miwili akiugua na hali yake ilikuwa inaendelea vizuri lakini hali ikabadilika usiku huu na kuaga dunia.

CHELSEA YAIPIGA BAO LA KISIGINO MAN UNITED KWA DIEGO COSTA

KLABU za Chelsea na Atletico Madrid zimekubaliana kubadilishana wachezaji, Diego Costa ahamie Stamford Bridge msimu ujao, kwa mujibu wa vyombo habari Hispania.
Kipa wa Blues, Thibaut Courtois, anayecheza kwa mkopo Atletico, amekuwa akizungumziwa na wengi kama mlinda mlango hodari kinda Ulaya, baada ya kudaka vizuri akiwa na klabu hiyo ya Hispania kwa misimu mitatu.
Lakini kipa huyo mwenye umri wa miaka 21 angependa kubaki Madrid, na kocha wa Chelsea, Jose Mourinho anamtaka mshambuliaji nyota, Costa arejee. Kocha wa Manchester United, David Moyes alitumai kumpata mshambuliaji huyo Old Trafford.

Karibuni atakuwa wa Blue? Diego Costa anaweza kuwa njiani kuelekea Stamford Bridge


Vidole gumba juu: Kwa vyovyote, kipa Thibaut Courtois anayedaka kwa mkopo wa muda mrefu Atletico, atahamia moja kwa moja klabu hiyo
Costa amefunga mabao 19 katika La Liga msimu huu, akishika nafasi ya pili kwa ufungaji nyuma ya Cristiano Ronaldo wa Real.
Kipaumbele cha Mourinho katika usajili huu ni mshambuliaji, na Mreno huyo amegoma kuondoka Januari.
Chelsea ilitaka kipa Courtois asaini Mkataba mpya licha ya kwamba hajawahi kuchezea timu ya Stamford Bridge, lakini Mbelgiji huyo angependa kuchezea klabu kwa Mkataba wa kudumu badala ya mkopo.
Courtois awali alisema atarejea Chelsea tu kuwa kipa namba moja mbele ya Petr Cech.

MZEE DUDUE WA MSANI KIKUNDI CHA FUTUHI CHA AFARIKI DUNIA


SAA KUMI NA MOJA KATIKA HOSPITALI YA BUGANDO BAADA YA KUUGUA KWA MUDA MFUPI,ENDELEA KTUFWATILIA TUTA KUPA HABARRI KAMILI PUNDE.
www.hakileo.blogspot.com

YANGA WAMEMNUNUA WAPI EMMANUEL OKWI?


Na BARAKA MBOLEMBOLEWakati ligi kuu ikianza, mchezaji mwenye thamani kubwa zaidi, Mganda, Emmanuel Okwi amekuwa mmoja wa watazamaji mwenye thamani kubwa. Je, Yanga wameingia ' mkenge' katika usajili wake?. Hili linaweza kuwa swali ambalo majibu yake yapo wazi. Kwanza, Okwi ni mchezaji wa Etoile du Salehe ya Tunisia ambao walimnunua kutoka timu ya Simba.

Sunday, 26 January 2014

NI CHELSEA NA MAN CITY, ARSENAL NA LIVERPOOL ROBO FAINALI KOMBE LA FA

KLABU ya Manchester City itamenyana na Arsenal katika Robo Fainali ya Kombe la FA wakati Chelsea itamenyana na Liverpool siku kadhaa kabla ya kumenyana na vigogo wa Ulaya, Barcelona na Bayern Munich katika Ligi ya Mabingwa.

Changamoto: Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho atakuwa na kazi mbele ya Manchester City

OSCAR ANOGESHA BIRTHDAY YA MOURINHO LEO, AIFUNGIA BAO PEKEE CHELSEA DHIDI YA STOKE KOMBE LA FA

BAO pekee la Oscar limempa raha Jose Mourinho akitimiza miaka 51 ya kuzaliwa baada ya kuilaza 1-0 Stoke City katika mchezo wa Raundi ya Nne ya Kombe la FA.
Mourinho alimpanga Oscar namba 10, nafasi ya Juan Mata aliyehamia Manchester United na akaziba vyema pengo hilo kwa kufunga dakika ya 28.

Mshindi wa mechi: Oscar akishangilia baada ya kuifungia kwa mpira wa adhabu Chelsea jana.

SIMBA SC YAANZA MZUNGUKO WA PILI KWA KUWAFUMUA RHINO - MESSI AENDELEZA MAKALI


Ramadhani Singano 'Mess' (kulia), akishangilia bao pekee aliloifungia timu yake katika mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara dhidi ya Rhino Rangers ya Tabora katika mchezo uliofanyika jana kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Ramadhani Singano akiipangua ngome ya Rhino Rangers ya Tabora.