Kutokana na maombi niliopokea kwa njia ya mails nyingi kutoka kwa wadau, baada ya kukata tumbo kwa wiki mbili, waliuliza ni diet gani nimetumia ili kufanikisha zoezi hilo.
Jibu langu ni hili:
Hii sio ya kitaalamu bali ni mimi ninavyofanya na ndio inayonisaidia kupunguza tumbo.
Kwasababu vitu vya formula mimi huwa siwezi kuvifuata na huwa naviona vigumu sana kwahiyo huwa najaribu kuishi vile ninavyoweza.
Na kizuri zaidi ni kwamba hii sio diet ya kujinyima.
Ila unaweza usifanikiwe pia kutokana na mwili wako kwakua tumeumbwa tofauti lakini unaweza kujaribu kama itafanya kazi

Tukianza na asubuhi nikiamka mimi kama Binti Machozi, naanza kunywa maji glass 3 kabla ya kupiga mswakwi.
Na nikiisha amka nakunywa maji ya uvugu vugu yaliokamuliwa ndimu au limao glass zingine tatu kabla ya kunywa Chai.
Ukizoea maji ni matamu kuliko hata biere
Kuwa Teja wa Maji kuna raha yake pia