Pages

ELIMU KWANZA.

ELIMU KWANZA.
FEDHA SIO KIPAUMBELE CHETU.

Saturday 2 November 2013

Beckham amtaka Ferguson arejea katika tasnia ya ufundishaji wa soka.




Mchezaji mkongwe wa soka kutoka nchini humo David Robert Joseph Beckham ameonyesha dhamira ya kutaka kumshawishi aliyekuwa meneja wa klabu ya Man utd Sir Alex Ferguson ili aweze kurejea katika tasnia ya ufundishaji wa soka.

ONA picha 16 za Nyumba anayomiliki na kuishi Mzee Majuto 96.0 Tanga pamoja na magari yake


Mwigizaji huyu ambae analipwa mshahara wa milioni 17 mpaka 20 kwa mwezi ndani ya kampuni ya Steps iliyomwajiri, anamiliki pia daladala tatu za kubeba abiria hukohuko kwake 96.0 Tanga alikozaliwa miaka 65 iliyopita huku wazazi wake wote wakitokea mkoani Kigoma.



Hii Noah nyeupe haifanyii biashara, mara nyingi ndio anatumia kuitembelea

YANGA SC YAIPIGA JKT 4-0



Ngassa alifunga bao la kwanza kwa shuti kali la umbali wa mita 20, baada ya kufanikiwa kuwatoka mabeki wawili wa JKT Ruvu, wakati bao la pili alifunga kwa kichwa akiunganisha mpira wa kurushwa na beki Mbuyu Twite.
Pamoja na kumaliza dakika 45 za kwanza wakiwa nyuma kwa 2-0, lakini JKT Ruvu ndiyo waliocheza soka ya kuvutia ya pasi za hapa na pale, huku Yanga wakitumia mashambulizi ya haraka kwa mabeki kupeleka mipira pembeni, ambako mawinga wanatia krosi washambuliaji wagombanie goli.
Kipindi cha pili, Yanga SC waliendelea na staili yao kushambulia kutokea pembeni, huku JKT Ruvu wakionekana kuanza kupoteza mwelekeo na kutoa mwanya zaidi wa kushambuliwa.
Beki Oscar Joshua aliipatia Yanga bao la tatu dakika ya pili ya kipindi cha pili, akiunganisha kona maridadi iliyochongwa na kiungo Simon Msuva.

MASHABIKI SIMBA WATAKA WACHEZAJI WAKONGWE WARUDISHWE



MASHABIKI WA SIMBA

Mashabiki Simba wamepiga kelele na kutala benchi lao la ufundi libadilike na kuwarudisha wachezaji wakongwe.

Zaidi ya mashabiki waliotuma ujumbe mfupi kupitia barua pepe na wale waliopiga simu ya mkononi ya SALEHJEMBE, wamemtaka Kocha Mkuu, Abdallah Kibadeni na wasaidizi wake kufikiria na kugeuza misimamo waliyonayo.

RATIBA YA LIGI KUU YA UINGEREZA LEO JUMAMOSI

Thursday 31 October 2013

MASHABIKI WA SIMBA NA YANGA KUMENYANA BONANZA LA NANI MTANI JEMBE SONGEA.

Na Mwandishi Wetu
Mashabiki wa Simba na Yanga mjini Songea watamenyana vikali katika michezo mbalimbali kupitia bonanza maalum la Nani Mtani Jembe lililoandaliwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager litakalofanyika uwanja wa Maji Maji mjini Songea Jumapili wikendi hii.
Mratibu wa bonanza hilo Amadeus Kalumuna, amesema kuwa michezo mbalimbali ikiwemo soka bonanza la wachezaji saba kila upande, kuvuta kamba, na pia mpira wa mezani maarufu kama fussball itapamba bonanza hilo. Burudani mbalimbali pia zitapamba bonanza hilo zikiwemo burudani ya muziki kutoka bendi ya Mastaa wa Kusini, kikundi cha sanaa cha Umoja Star au maarufu kama “Manyoka”, wacheza show wa Chicharito Group pamoja na wasanii mbalimbali wa muziki wa kizazi kipya wa mkoani Ruvuma.

ONA FUJO ZA MASHABIKI WA SIMBA JANA TAIFA


Nimesikitishwa sana na vitendo vya kihuni vilionyeshwa na wachezaji na baadhi ya wapenzi wa Simba jana pale Neshno.

Simba wanastahili adhabu ikiwemo kufidia uharibu ule wa viti vya kukalia. Na adhabu hiyo isichelewe...
Maggid.



haya ni mabomu ya machozi ambayo yalirushwa ili kudhibiti vurugu hizo

Na Mahmoud Zubeiry, Dar es Salaam
UWANJA wa Taifa, Dar es Salaam jana uligeuka eneo la vita baina ya Polisi mashabiki wa Simba SC, kufuatia Kagera Sugar kupata bao la kusawazisha dakika ya pili ya muda wa nyongeza baada ya kutimia kwa dakika 90 za mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, timu hizo zikitoka 1-1.
Baada ya Salum Kanoni kukwamisha nyavuni mkwaju wake wa penalti, mashabiki wa Simba waliokuwa viti vya Rangi ya Bluu na Chungwa, walianza kung'oa viti na kuvitupia uwanjani.



hapa mashabiki wakikimbia baada ya vurugu hizo kuanza kutokea na mabomu kuanza kurushwa



Mara moja, Polisi walianza kupambana na mashabiki hao kwa kuwatupia mabomu ya machozi, ndipo wakaanza kukimbia. Makocha na wachezaji wa Simba kwa pamoja waliwafuata waamuzi kuwalalamikia- hali ambayo ilifanya watolewe kwa kusindikizwa na Polisi.
Katika mchezo huo, uliochezeshwa na refa Mohamed Theofile wa Morogoro aliyesaidiwa na Said Mnonga na Charles Chambea wote wa Mtwara, ambao walishindwa kuumudu kabisa, hadi mapumziko, Simba SC walikuwa mbele kwa bao 1-0.



hivi ni baadhi ya viti vilivyong'olewa na mashabiki

Bao hilo lilifungwa na mshambuliaji wa kimataifa wa Burundi, Amisi Tambwe dakika ya 45 baada ya kupokea pasi nzuri ya Betram Mombeki na kumpiga chenga beki Salum Kanoni, kabla ya kumchambua kipa Hannington Kalyesebula.

Wednesday 30 October 2013

MSIBANI KWA BABA WEMA... LULU ATOA MITUSI MIZITO jua kisa na mkasa.


Elizabeth Michael ‘Lulu’ akiwa msibani kwa marehemu Balozi Sepetu.

Tukio hilo lililotawaliwa na hasira lilijiri Oktoba 28, 2013 kwenye msiba huo uliokuwa ukiombolezwa nyumbani kwa marehemu, Sinza-Mori jijini Dar es Salaam.

KISA NA MKASA
Ilikuwa wakati Lulu akitinga msibani hapo, ghafla alimfuata mmoja wa waandishi wa habari hii na kuanza kumporomoshea matusi hayo kwa kile alichodai kukerwa na habari iliyowahi kuandikwa juu ya kitendo chake cha kula chakula sahani tatu katika hafla moja iliyofanyika hivi karibuni huko Kunduchi Beach Hotel, Dar.

SIR ALEX FERGUSON AVUNJA YA MAUZO YA KITABU CHAKE



Kitabu cha Sir Alex Ferguson kimeweka rekodi ya kuwa kitabu kilichooza kwa haraka zaidi ndani ya Uingereza kikiuza nakala 115,547 katika siku chache za mauzo. (HM)

Kwa mujibu wa taarifa kutoka The Bookseller, kitabu hicho cha mocha wa zamani wa Manchester United kimevunja rekodi ya Delia Smith, ambaye kitabu chake cha mwaka 1999 cha mapishi kiliuza kopi 112,000 katika wiki take ya kwanza.

BARCELONA YAENDELEZA MPANGO WA KUMSAJILI KIPA WA LIVERPOOL



KLABU ya Barcelona imeendelea na nia yake ya kumsajili kipa wa Liverpool, Pepe Reina. (HM)
Kipa huyo wa Hispania mwenye umri wa miaka 31 amepelekwa kwa mkopo wa muda mrefu Napoli, laki Rafa Benitez bado hajaamua kumnunua jumla wakati Liverpool inataka kuachana naye moja kwa moja.

MAN U YAIBAMIZA NORWICH 4-0



Chicharito (HM)


MSHAMBULIAJI Javier Hernandez 'Chicharito' ameendeleza takwimu zake nzuri ndani ya Manchester United, licha ya kupewa nafasi chache za kucheza kwenye timu hiyo.

Wizkid na P-Square waondolewa kweye kinyang'anyiro MTV EMA 2013




Kwa mara ya pili mfululizo, wasanii wa Nigeria wanaowania Tuzo za MTV katika category ya Africa wameondolewa katika mashindano hayo.
Waandaaji wa Tuzo hizo wametangaza kuwa wasanii wa South Africa, LCNVL wamepigiwa kura kama Best African Act, position iliyowaondoa WizKid na P-Square katika mashndano hayo. Mwaka jana Wizkid na D'banj walikuwa ni washiriki pia kutoka Nigeria ambao hawakupita pia.

RAIS WA CAF AMPONGEZA MALINZI



Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), Issa Hayatou amempongeza Jamal Malinzi kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) katika uchaguzi uliofanyika Oktoba 27 mwaka huu.

Katika salamu zake kwa niaba ya Kamati ya Utendaji ya CAF na familia ya mpira wa miguu Afrika, Rais Hayatou amesema uchaguzi huo unampa Rais Malinzi fursa ya kuupeleka mbele mpira wa miguu nchini Tanzania.

SIMBA, KAGERA SUGAR KUUMANA KESHO


Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inaanza raundi ya 12 kesho (Oktoba 31 mwaka huu kwa mechi kati ya Simba na Kagera Sugar itakayofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni.

Viingilio katika mechi hiyo itakayooneshwa moja kwa moja na Azam Tv kupitia TBC 1 vitakuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 kwa VIP A.

Magazeti ya leo October 30 2013





.


.


.

SIMBA SC KUJIPIMA NA KMKM TAIFA KESHO...MCHAKATO WA KATIBA NAO WASHIKA KASI

Na Ezekiel Kamwga, IMEWEKWA SEPTEMBA 5, 2013 SAA 4:02 ASUBUHI
KESHO Ijumaa, Septemba 6 mwaka 2013, klabu ya Simba itacheza mechi ya kirafiki na mabingwa wa soka wa Ligi Kuu ya Zanzibar, KMKM, Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
Lengo kuu la mechi hiyo ni mazoezi kwa Simba ya kujiandaa na mchezo wake dhidi ya Mtibwa Sugar uliopangwa kufanyika Septemba 14 mwaka huu.
Kikosi kamili cha KMKM kimewasili mjini Dar es Salaam tayari na leo saa tano na nusu kamili nahodha wake, Abdi Kassim Babi na kocha mkuu wa timu hiyo wanatarajiwa kuzungumza na waandishi wa habari katika mgahawa wa City Lounge katikati ya jiji.

Simba SC itacheza na Mafunzo kesho

FIFA YATOA MAJINA YA WANASOKA WANAOWANIA TUZO YA MWANASOKA BORA WA DUNIA.




BLATTER AMUOMBA RADHI RONALDO BAADA YA KUSEMA ANAMPENDA MESSI




RAIS wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), Sepp Blatter ameomba radhi kwa Cristiano Ronaldo baada ya mshambuliaji huyo wa Real Madrid kumchamba katika ukurasa wake wa Facebook.
Mapema Blatter alitoa hotuba iliyomkera Ronaldo kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Oxford, Uingereza. Katika majadiliano yake na wanafunzi hao, Blatter alielezea mapenzi yake kwa Lionel Messi, na akaweka kando kiti chake cha Urais FIFA na kumshambulia kibinafsi Ronaldo. Blatter pia amesemekana kumpiga dongo nyota huyo wa Madrid kwamba anatumia fedha zake nyingi kupamba nywele zake.

MBEYA CITY YAIDUWAZA PRISONS 2-0



MBEYA City imezidi kuipumulia Azam FC kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, kufuatia ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Prisons Uwanja wa Sokoine, Mbeya jana.
Matokeo hayo yanaifanya Mbeya City inayofundishwa na kocha maarufu, Juma Mwambusi itimize pointi 23 baada ya mechi 11, sawa na Azam.

CHELSEA WAIPIGA ARSENAL 2-0 KOMBE LA LIGI


chelsea 53b6d
Wachezaji wa Chelsea wakishangilia ushindi

Monday 28 October 2013

Diamond afanya collabo na Davido




Muziki wa Afrika mashariki ulikuta na muziki wa Afrika Magharibi kwa mara nyingine baada ya Davido na Diamond kuingia studio na kufanya remix ya wimbo My number one. Wimbo huo wali-perform kwa mara ya kwanza kwenye show ya fiesta iliyofanyika jana kwenye viwanja vya Leaders club.Bado taarifa za uwezekano wa wawili hao kufanyia video huo wimbo hazijatoka

YANGA, MGAMBO JKT KUVAANA TAIFA LEO



MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu ya Bara leo itashuka katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kupambana na Mgambo JKT katika mchezo wa raundi ya kumi na moja ya ligi hiyo.
Yanga inaingia uwanjani leo ikiwa na pointi 19 ilizopata katika mechi 10 ilizocheza huku ikiwa nafasi ya nne. Azam inaongoza ligi hiyo ikiwa na pointi 23 ikifuatiwa na Simba yenye pointi 20 huku zote zikiwa zimecheza mechi 10. Mbeya City ni ya tatu ikiwa na pointi 20 katika mechi 10.

Mgengwa; LEO NIMEONGEA KWA SIMU NA PRESIDENT MALINZI NA NYAMLANI...



Ndugu zangu,
Kwa nafasi yangu ya Ujumbe wa Mkutano Mkuu, TFF, katika nyakati tofauti, leo niliongea kwa simu na Rais mpya wa TFF Ndugu Jamal Malinzi na aliyemshinda kwenye nafasi ya Urais Ndugu Athumani Nyamlani.

BREAKING NEWS,JAMAL MALINZI ASHINDA URAIS TFF, KARIA, KIDAO, KABURU NAO WAPETA

JAMAL Emil Malinzi, usiku huu ameshinda Urais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) baada ya kupata kura 72, dhidi ya 52 za mpinzani wake Athumani Jumanne Nyamlani.
Katika uchaguzi huo uliofanyika kwenye ukumbi wa NSSF Water Front, Dar es Salaam, Walace Karia alifanikiwa kushinda nafasi ya Makamu wa Rais kwa kupata kura 67 akiwashinda Nassib Ramadhani kura 52 na Imani Madega sita.

Huyu ndiye Rais wenu mpya TFF; Rais aliyemaliza muda wake TFF, Leodegar Tenga kushoto akimtambulisha Jamal Malinzi kuliakuwa Rais mpya wa shirikisho hilo usiku nwa kuamkia leo ukumbi wa NSSF Water Front, Dar es Salaam

Katika nafasi za Ujumbe; Kanda ya 13; kiungo wa zamani wa Simba SC Wilfred Kidau amepata kura 60 na kuwashinda Muhsin Said kura 50, Omar Abdulkadir kura 10 na Alex Kabuzelia kura nne.
Kanda 12; Khalid Mohamed Abdallah amepata kura 69 na kumshinda Davisa Mosha aliyepata kura 54.
Kanda ya 11 Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ amepata kura 78 na kuwashinda Riziki Majala kura tano, Twahir Njoki kura mbili, Juma Pinto kura 26 na Farid Mbaraka kura 14, Kanda ya 10 ameshinda Hussein Mwamba aliyepata kura 63, huku Charles Komba akipata nne na Stewart Nasima 58.

SIRI,ILE BARUA YA "matoto wa BABU SEYA" PAPII KOCHA KWA RAIS JAKAYA KIKWETE,amemuomba msamaha ili kesi yake iishe.



YAH: MAOMBI YA KUPEWA MSAADA (MSAMAHA) WA KUFUTIWA ADHABU YA KIFUNGO NILIYOPEWA NA MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI KISUTU.

Husika na somo hilo hapo juu.
Mimi ni mfungwa katika gereza kuu Ukonga. Kwa heshma na taadhima na kwa kutambua utu na huruma yako ya kiMUNGU ulionayo dhidi ya binadamu wenzako pamoja na mamlaka uliokabidhiwa na Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Naanguka na kushika miguu yako mitukufu muheshimiwa rais. Nakuomba msaada (msamaha) kwako muheshimiwa rais, kwa njia hii ya maandishi kusudi niweze kuondolewa adhabu ya kifungo cha maishagerezani,niliyohukumiwa na mahakama tajwa hapo juu. Mh.Rais mimi nimefungwa nikiwa bado kijana mwenye umri mdogo, na ukweli kutoka moyoni sikufanya kosa hilo. Si mimi, baba yangu Nguza wala ndugu yangu yeyote aliyefanya kitendo kile. Lakini wenye mamlakawakatuona tuna hatia na kuamua kuteketeza kizazi chetu gerezani.

Natamani kiama ifike ili mwenyezi Mungu aweke wazi ukweli wote uliojificha nyuma ya pazia. Mpaka sasa natambua wazi hatima pamoja na dhamana ya maisha yangu ipo katika mikono yako

mitukufu Mh. Rais Naomba huruma yako muheshimiwa Rais maana mimi ni mtoto wako ninaehitaji

huruma yako wewe mzazi. Lakini pia sisi ni binadamu wenye nafsi na miili kama wengine. Waliotumia mamlaka yao kutuweka gerezani nao ni binadamu pia, wenye miili na nafsi. Ipo siku nafsi zetu zitapaswa kutoa hesabu ya tuliyoyafanya hapa duniani. wakati huo miili yetu tunayoitumia

kunyanyasa wanyonge itakuwa imeoza mavumbini.
Natumaini kauli yako ya mwisho ndio itakayoleta pumzi ya uhai nafsini mwangu. Nakutakia kazi njema, afya njema na maisha marefu.

Mungu akubariki.

Wako mtiifu

Mfungwa NO:836'04

JOHNSON

NGUZA (PAPII KOCHA)

AZAM FC YAICHARAZA SIMBA SC 2-1 NA KUPAA KILELENI LIGI KUU BARA



Na Mahmoud Zubeiry, Dar es Salaam
AZAM FC imerejea kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kufuatia ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Simba SC ikitoka nyuma kwa bao 1-0.
Shujaa wa Azam leo alikuwa ni mshambuliaji kutoka Ivory Coast na mfungaji bora wa Ligi Kuu msimu uliopita, Kipre Herman Tchetche aliyefunga mabao yote ya timu hiyo ya Alhaj Sheikh Said Salim Awadh Bakhresa.
Kwa matokeo hayo, Azam inatimiza pointi 23 na kujinafasi kileleni, ikiwazidi kwa pointi tatu Simba SC na Mbeya City katika nafasi ya pili.
Wachezaji wa Azam wakishangilia ushindi wao leo

MCHEZO MCHAFU TFF....!!ni rushwa katika uchaguzi.



Saa chache baada ya Rais wa aliyemaliza muda wake wa Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF), Leodegar Tenga kuwaonya wajumbe wa Mkutano Mkuu kujiepusha na ushawishi wa rushwa katika uchaguzi huo, baadhi ya wagombea waliziba masikio na kujikuta wakiishia kulala lupango.

Taarifa zinasema wajumbe wawili majina tunayo, usiku wa kuamkia jana walilala kwenye Kituo cha Polisi Tabata wakituhumiwa kupokea hongo ya Sh3 milioni sambamba na majina ya wapigakura usiku wa kuamkia jana.

Habari za ndani ambazo gazeti hili ilizipata kutoka ndani ya wagombea hao, zilisema kuwa baada ya watuhumiwa hao kukamatwa waliwataja wagombea waliowatuma kugawa fedha hizo kwa lengo la kuomba kura.

Hata hivyo watuhumiwa hao waliachiwa kwa dhamana jana asubuhi huku kesi hiyo inatarajiwa kuhamishwa kwenye Taasisi ya Kupambana na Rushwa Takukuru leo kwa hatua zaidi.