Pages

ELIMU KWANZA.

ELIMU KWANZA.
FEDHA SIO KIPAUMBELE CHETU.

Wednesday 30 October 2013

SIMBA SC KUJIPIMA NA KMKM TAIFA KESHO...MCHAKATO WA KATIBA NAO WASHIKA KASI

Na Ezekiel Kamwga, IMEWEKWA SEPTEMBA 5, 2013 SAA 4:02 ASUBUHI
KESHO Ijumaa, Septemba 6 mwaka 2013, klabu ya Simba itacheza mechi ya kirafiki na mabingwa wa soka wa Ligi Kuu ya Zanzibar, KMKM, Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
Lengo kuu la mechi hiyo ni mazoezi kwa Simba ya kujiandaa na mchezo wake dhidi ya Mtibwa Sugar uliopangwa kufanyika Septemba 14 mwaka huu.
Kikosi kamili cha KMKM kimewasili mjini Dar es Salaam tayari na leo saa tano na nusu kamili nahodha wake, Abdi Kassim Babi na kocha mkuu wa timu hiyo wanatarajiwa kuzungumza na waandishi wa habari katika mgahawa wa City Lounge katikati ya jiji.

Simba SC itacheza na Mafunzo kesho

Simba inaendelea na mazoezi yake jijini na wachezaji wake wote wapo katika hali nzuri na tayari kwa ajili ya mechi hiyo.
Mechi hiyo itaanza majira ya saa 11 jioni ili kuwezesha watu wengi kwenda uwanjani kutazama mechi hiyo ikizingatiwa kuwa Ijumaa ni siku ya kazi.
Wakati huo huo: Kufuatia tangazo la Mwenyekiti wa Simba, Alhaj Ismail Aden Rage, kuhusu Mkutano wa Katiba uliopangwa kufanyika Novemba mwaka huu, klabu imeanzisha rasmi mchakato wa kuwa na Katiba Mpya itakayokwenda na wakati.
Kutokana na umuhimu wa mawazo ya Wana Simba ndani na nje ya nchi kufahamika kupitia mchakato huu, klabu imeanzisha email maalumu iitwayo maoniyakatibayasimba@gmail.com ambapo wana Simba na wapenzi wa soka kwa ujumla wanatarajiwa kuwasilisha mawazo na michango yao kuhusu nini kinapaswa kuingizwa katika Katiba mpya ya klabu.
Uongozi wa Simba unawaomba wapenzi na washabiki wa soka popote walipo duniani kuchangia mawazo katika njia hii. Mawazo yatakayochangiwa kwenye email hii yatatumika katika kutengeneza rasimu ya Katiba hiyo na rasimu hiyo itapelekwa kwenye matawi yote ya klabu kwa ajili ya kujadiliwa na wanachama.
Mawazo hayo ya wanachama yatasaidia katika kutengeneza Katiba ambayo hatimaye itawasilishwa kwenye Mkutano wa Novemba kwa ajili ya mapitio na kupitishwa.
Wana Simba wanatakiwa kujitokeza katika mchakato huu kwa faida ya kujenga Simba ya kisasa na yenye tija na ufanisi.

No comments:

Post a Comment