Pages

ELIMU KWANZA.

ELIMU KWANZA.
FEDHA SIO KIPAUMBELE CHETU.

Saturday 2 November 2013

Beckham amtaka Ferguson arejea katika tasnia ya ufundishaji wa soka.




Mchezaji mkongwe wa soka kutoka nchini humo David Robert Joseph Beckham ameonyesha dhamira ya kutaka kumshawishi aliyekuwa meneja wa klabu ya Man utd Sir Alex Ferguson ili aweze kurejea katika tasnia ya ufundishaji wa soka.
David Beckham ambae aliwahi kunolewa na kocha huyo ambae alitangaza kustaafu ufundishaji wa soka mwezi May mwaka huu, amesema anafikiria kumshawishi Sir Alex Ferguson kurejea shughulini kwa kumtaka akinoe kikosi cha klabu anayoimiliki huko nchini Marekani.
Beckham amesema anapendezwa na ufundishaji wa mzee huyo mwenye umri wa miaka 71, na ana hakika endapo atafanikisha mpango wa kumshawishi, klabu yake ya Miami inayoshiriki ligi ya nchini Marekani itapata nafasi kubwa ya kufanya vizuri.



Hata hivyo gwiji huyo ambae alitangaza kustaafu soka mwishoni mwa msimu uliopita baada ya mkataba wake na klabu ya Paris Saint-Germain ya nchini Ufaransa, akaonyesha kubabaisha juu ya kauli hiyo kwa kusema anatania, lakini vyombo vya habari vya nchini kwao Uingereza vimeonyesha kuipa kipaumbele habari hiyo.
Katika hatua nyingine David Beckham amesema hawezi kuzungumza lolote juu ya taarifa iliyoandikwa na Sir Alex Ferguson katika kitabu chake alichokizindua juma lililopita ambayo inaeleza sababu zilizofanya kuuzwa na klabu ya Man Utd na kusajiliwa na klabu ya Real Madrid mwaka 2003.
David Beckham amesema kilichoandikwa na Ferguson katika kitabu hicho chastahili kuheshimiwa na bado yeye binafsi anamuheshimu mzee huyo kwa dhati kutokana na mchango mkubwa aliompa kwa kukisaidia kipaji chake na kufikia hatua ya kujulikana duniani kote.

No comments:

Post a Comment