Saturday, 2 November 2013
YANGA SC YAIPIGA JKT 4-0
Ngassa alifunga bao la kwanza kwa shuti kali la umbali wa mita 20, baada ya kufanikiwa kuwatoka mabeki wawili wa JKT Ruvu, wakati bao la pili alifunga kwa kichwa akiunganisha mpira wa kurushwa na beki Mbuyu Twite.
Pamoja na kumaliza dakika 45 za kwanza wakiwa nyuma kwa 2-0, lakini JKT Ruvu ndiyo waliocheza soka ya kuvutia ya pasi za hapa na pale, huku Yanga wakitumia mashambulizi ya haraka kwa mabeki kupeleka mipira pembeni, ambako mawinga wanatia krosi washambuliaji wagombanie goli.
Kipindi cha pili, Yanga SC waliendelea na staili yao kushambulia kutokea pembeni, huku JKT Ruvu wakionekana kuanza kupoteza mwelekeo na kutoa mwanya zaidi wa kushambuliwa.
Beki Oscar Joshua aliipatia Yanga bao la tatu dakika ya pili ya kipindi cha pili, akiunganisha kona maridadi iliyochongwa na kiungo Simon Msuva.
Kona hiyo ilitokana na kazi nzuri ya kipa wa JKT Ruvu, Sadick Mecks aliyepangua shuti kali la kiungo wa Yanga, Frank Domayo.
Jerry Tegete alikamilisha karamu ya mabao ya Yanga SC dakika ya 88 kwa pasi ya Simon Msuva na kuwafanya mashabiki wa timu hiyo waimbe nyimbo za furaha kuwabeza wapinzani, Simba SC ambao jana walilazimishwa sare ya 1-1 na Kagera Sugar kwenye Uwanja huo.
Yanga SC; Deo Munishi 'Dida', Mbuyu Twite/Ibrahim Job dk45, Oscar Joshua, Nadir Haroub 'Cannavaro', Kevin Yondan/Relianst Lusajo dk78, Athumani Iddi 'Chuji', Simon Msuva, Frank Domayo, Didier Kavumbangu/Jerry Tegete dk64, Mrisho Ngassa na Hamisi Kiiza.
JKT Ruvu; Sadick Mecks, Mussa Zuberi, Kessy Mapande, Omar Mtaki, Damas Makwaya/Richard Msenyi dk64, Nashon Naftali, Amos Mgisa, Haruna Adolph, Paul Ndauka, Samuel Kamutu/Abdallah Bunu dk 64 na Sosthenes Manyasi/Emmanuel Pius dk59.
Raundi ya 12 ya ligi hiyo itaendelea kesho kwa mechi nne zitakazochezwa katika miji minne tofauti.
Mgambo Shooting na Coastal Union zitaoneshana kazi kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga, Mbeya City na Ashanti United zitaumana kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya, Azam na Ruvu Shooting (Azam Complex, Dar es Salaam), na Mtibwa Sugar na Rhino Rangers (Uwanja wa Manungu, Morogoro).
Raundi hiyo itakamilika Novemba 3 mwaka huu kwa mechi moja ambapo Tanzania Prisons itakuwa mwenyeji wa Oljoro kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.
Mechi za kukamilisha mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo zitachezwa Novemba 6 na 7 mwaka huu. Novemba 6 ni JKT Ruvu vs Coastal Union, Ashanti United vs Simba, Kagera Sugar vs Mgambo Shooting, na Ruvu Shooting vs Mtibwa Sugar.
Novemba 7 mwaka huu, Azam itacheza na Mbeya City, Yanga itacheza na Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wakati Rhino itakuwa mwenyeji wa Tanzania Prisons.
Chanzo:bongostaz.blogspot.com
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment