Pages

ELIMU KWANZA.

ELIMU KWANZA.
FEDHA SIO KIPAUMBELE CHETU.

Saturday 1 March 2014

Young Africans (Tanzania) 1-0 Al Ahly (Egypt)

- Gor Mahia (Kenya) 2-3 Esperance (Tunisia)
- Dynamos (Zimbabwe) 0-0 AS Vita (DRC)

PICHANI NI MASHABIKI WANAODHANIWA KUWA NI WA SIMBA SC AMBAO WALIANZA KURUSHA VITI BAADA YA YANGA KUFUNGA GOLI. JE HUU NI USTAARABU???

Thursday 27 February 2014

PICHA ZA AJALI MBAYA YA GARI ALIYOPATA MCHUNGAJI WA KANISA LA SABATO DODOMA




Mchungaji Michael Zacharia Twakaniki (katikati)akiwa hospitalini huko Dodoma kushoto mwenye tai ni Mhazini wa jimbo la Mashariki mwa Tanzania katika kanisa la Waadventista Wa Sabato Tanzania Athanas Sigoma alipomtembelea juzi.

ADEBAYO AIPAISHA TIMU YAKE

KOCHA Tim Sherwood aliwataka vijana wake wafanye kazi na Emmanuel Adebayor ameiongoza vizuri kazi hiyo usiku wa kuamkia leo baada ya kuifungia Tottenham Hotspur mabao mawili katika ushindi wa 3-1 Uwanja wa White Hart Lane katika mchezo wa Europa League.
Matokeo hayo yanaifanya Spurs iliyofungwa 2-0 katika mchezo wa kwanza,ipate ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Dnipro na kutinga 16 Bora ya Europa League ambako itakutana na Benfica.
Christian Eriksen alianza kufunga dakika ya 56 kabla ya Mtogo Emmanuel Adebayor kumaliza kazi dakikaza 65 na 69 katika mchezo ambao wageni walimpoteza mchezaji wao, Zozulya aliyetolewa nje kwa nyekundu dakika ya 62, akitoka kuifungia timu hiyo bao dakika ya 48.
Katika mechi nyingine, Valencia imetoka 0 – 0 na Dynamo Kyiv, Trabzonsporimefungwa 2-0 na Juventus, Lyon imeifunga 1 – 0 FC Chornomorets, KRC Genk imefungwa 2-0 na Anzhi Makhachkala, Fiorentina imetoka 1 – 1 na Esbjerg fB, AZ imetoka 1 – 1 na Slovan Liberec na Benfica imeifunga 3 – 0 PAOK Salonika.
Nayo Shakhtar Donetsk imefungwa 2-1 na Viktoria Plzen, Napoli imeifunga 3 – 1 na Swansea City, Ludogorets Razgrad imetoka 3 – 3 na Lazio, Eintracht Frankfurt imetoka 3 – 3 na FC Porto, FC Red Bull Salzburg imeilaza 3 – 1 Ajax, Sevilla imeifunga 2 – 1 NK Maribor, Basel imeichapa 3 - 0 Maccabi Tel Aviv na Rubin Kazan imefungwa 2-0 na Real Betis.

Mkali kweli: Emmanuel Adebayor ameifungia mabao mawili muhimu Spurs na kuivusha Hatua ya 16 Bora ambako itakutana na washindi wa pili wa mwaka jana, Benfica

OFFICIAL: KIM POULSEN ATEMESHWA KIBARUA TAIFA STARS - SALUM MADADI NA HAFIDH BADRU KUONGOZA JAHAZI


Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Kocha wa Taifa Stars, Kim Poulsen wamekubaliana kuvunja mkataba katika makubaliano ambayo ni siri kwa pande zote mbili.

Uamuzi huo umetangazwa leo (Februari 27 mwaka huu) jijini Dar es Salaam kwa pamoja na Rais wa TFF, Jamal Malinzi na Kocha Poulsen mbele ya waandishi wa habari.

NIONAVYO MIMI: AZAM FC HAIWAPENDI WATANZANIA.



Na Oscar Oscar Jr.   0789-784858
Siwezi kushangaa siku moja nikiamka asubuhi na kusikia taarifa kwenye vyombo vya habari kuwa, wamiliki wa timu ya Azam wameamua kununua Ndege yao kwa lengo la kurahisisha Usafiri wa kwenda mikoani kucheza michezo yao ya ligi kuu na ile ya barani Afrika ambayo timu hiyo imekuwa ikishiriki kwa msimu wa pili sasa mfululizo. Kila nchi duniani ina tamaduni zake na moja ya tamaduni za kitanzania ni kushirikiana kwenye matukio muhimu ya kijamii.

Wednesday 26 February 2014

RONALDO, BALE NA BENZEMA KILA MMOJA AFUNGA MBILI REAL IKIWAFUMUA WAJERUMANI 6-1 KWAO

WINGA Gareth Bale ameendelea kung'ara Real Madrid akiiwezesha timu hiyo kutanguliza mguu mmoja Robo Fainali Ligi ya Mabingwa Ulaya kufuatia ushindi wa mabao 6-1 dhidi ya wenyeji Schalke usiku huu.
Mchezaji huyo ghali duniani aliyenunuliwa kwa Euro Milioni 86, alifunga mabao mawili na kutoa pasi mbili za mabao katika ushindi huo mnono.
Kocha Carlo Ancelotti amevutiwa na kiwango cha Bale na akamwagia sifa baada ya mechi hiyo ambayo mabao mengine Real yalifungwa na Karim Benzema na Cristiano Ronaldo kila mmoja mawili pia huku bao la kufutia machozi la wenyeji likifungwa na Klaas-Jan Huntelaar.

Sisi noma; Ronaldo kulia na Bale kushoto wakishangilia moja ya mabao yao usiku huu Real ikishinda 6-1 dhidi ya Schalke

DROGBA ALIVYOWAFANYA CHELSEA JANA...WE ACHA TU!


Mshambuliaji wa Galatasaray, Didier Drogba kushoto akipambana na Nahodha wa Chelsea, John Terry katika mchezo wa kwanza 16 Bora Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku huu, timu hizo zikitoka sare ya 1-1. Drogba alicheza pamoja na Terry Chelsea kwa muda mrefu
Terry akiteleza kuondosha mpira miguuni mwa Drogba

CHELSEA 1-1 NA GALATASARAY ULAYA

CHELSEA imepata sare ya ugenini ya kufungana bao 1-1 na wenyeji Galatasaray katika mchezo wa kwanza wa 16 Bora Ligi ya Mabingwa Bora Ulaya usiku huu.
Fernando Torres alitangulia kuifungia The Blues dakika ya tisa na kuifanya Chesea kuwa timu ya kwanza ya England kufunga bao katika 16 ya Ligi ya Mabingwa msimu huu, baada ya wiki iliyopita Arsenal kufungwa 2-0 na Bayern Munich na Manchester City kufungwa 2-0 na Barcelona, wakati jana Manchester United iIifungwa 2-0 pia ugenini na Olympiacos.
Hata hivyo, wenyeji Galatasaray walisawazisha bao hilo dakika ya 64 kupitia kwa Chedjou.

Hatufungwi sisi; Fernando Torres akishangilia na wenzake baada ya kuifungia bao Chelsea usiku huu