Fernando Torres alitangulia kuifungia The Blues dakika ya tisa na kuifanya Chesea kuwa timu ya kwanza ya England kufunga bao katika 16 ya Ligi ya Mabingwa msimu huu, baada ya wiki iliyopita Arsenal kufungwa 2-0 na Bayern Munich na Manchester City kufungwa 2-0 na Barcelona, wakati jana Manchester United iIifungwa 2-0 pia ugenini na Olympiacos.
Hata hivyo, wenyeji Galatasaray walisawazisha bao hilo dakika ya 64 kupitia kwa Chedjou.

Hatufungwi sisi; Fernando Torres akishangilia na wenzake baada ya kuifungia bao Chelsea usiku huu

Kitaalamu: Fernando Torres akiifungia bao la kuongoza Chelsea
No comments:
Post a Comment