Pages

ELIMU KWANZA.

ELIMU KWANZA.
FEDHA SIO KIPAUMBELE CHETU.

Saturday 28 September 2013

MATOKEO LIGI KUU ENGLAND HAYA HAPA.

MAHUSIANO NA AFYAJUA NAMNA YA KUONGEZA MVUTO WA KIMAPENZI.


NA LILIANI SETH
Mahusiano na afya kwa hakika vinashabiana kwani vinategemeana kwa kufanya  kuwepo furaha angalau kidogo kwa mwanadamu ni wazi kama hauna mahusiano ya aina yeyote ni dhahiri afya yako itadhorota hivyo tarajia afya njema kama unamahusiano.Mahusiano ni neno pana kulingana na uzito na ugumu wa kuzingatia katika mahusiano na pia yapo mahusiano ya aina mbalimbali kama kati ya wazazi na watoto wao,familia moja na nyingine,mtu na mtu  na hata shirika na shirika lakini leo nitazungumzia mahusiano ya mtu na mtu
Ni rahisi kujenga mahusiano na mtu yeyote lakini ni vigumu kudumisha na kufurahia mahusiano hayo kutokana na  utofauti kama wa rika,hali ya kimaisha,tabia,imani na mengineyo mengi hivyo ni vizuri kabla ya kuanzisha mahusiano ni lazima ukubali kuzingatia vitu Fulani ili kuhakikisha unapokuwa na mahusiano yanadumu kwa wakati wote.Katika maisha tunayoishi tunategemea mahusiano ili kutoa na kupokea vitu Fulani ambavyo inawezekana vinafaida au havina faida kwa wakati mwingine vinadhoofu miili yetu

ROSE NDAUKA KUZAA BILA NDOA




Stori: IMELDA MTEMA
Staa wa filamu za Bongowood, Rose Ndauka ambaye ni mjamzito anadaiwa kuwa atazaa kabla ndoa mwezi Aprili, mwakani

TOTTENHAM HOTSPUR 1 - 1 CHELSEA


www.tabasamuleo.blogspot.com

Timu za Tottenham Hotspur na Chelsea zimetoka sare kwa kufungana 1-1 huku Tottenham Hotspur ikiwa ya kwanza kupata goli lake lilofungwa na Gylfi Sigurdsson dakika ya 19 ya mchezo, mpaka mapumziko Tottenham Hotspur ilikuwa ikiongoza kwa goli hilo moja. Chelsea waliweza kupata goli lao la kusawazisha kunako dakika ya 65 kupitia kwa beki wake John Terry. Lakini mambo yalikuwa mabaya kwa siku ya leo baada ya mshambuliaji wa Chelsea Fernando Torres kupewa kadi nyekundu dk 81. Mpaka mwisho wa mchezo Tottenham Hotspur 1 - 1 Chelsea

Endelea kuitembelea Mjengwablog kwa matokeo zaidi ya mechi za leo na habari nyingine(P.T)

MFUNGWA AKUTWA AKIJIUZA.

BAADA Mei mwaka huu kuhukumiwa kifungo cha miezi sita gerezani kwa kosa la kufanya ukahaba, mkazi wa jijini Dar, Blandina Barton amekamatwa tena kwa kosa  hilohilo ikiwa ni mwezi mmoja kabla ya kumaliza kifungo chake, Risasi Jumamosi linakupa mkasa mzima.…


Mtuhumiwa, Blandina Barton baada ya kukamatwa na Poilisi.
Stori: RICHARD BUKOS
BAADA Mei mwaka huu kuhukumiwa kifungo cha miezi sita gerezani kwa kosa la kufanya ukahaba, mkazi wa jijini Dar, Blandina Barton amekamatwa tena kwa kosa  hilohilo ikiwa ni mwezi mmoja kabla ya kumaliza kifungo chake, Risasi Jumamosi linakupa mkasa mzima.www.hakileo.blogspot.com

MAKALA Siri Yanga matokeo ya Ligi Kuu Bara





By MWANDISHI WETU
Matokeo hayo yanaifanya Yanga iwe imepigwa mabao sita kwenye mechi tano licha ya kuwa na mabeki mahiri wanne ambao wanacheza kwenye timu za Taifa ambao ni Cannavaro, Twite, Yondani, Luhende na Barthez

YAKUMBUKE kwanza majina haya; Cannavaro, Twite, Yondani, Luhende na Barthez. Halafu endelea kusoma habari hii.

Kuna timu nne pekee za Tanzania zinazofanya matumizi makubwa zaidi msimu huu ikiwamo kulipa mishahara mikubwa na kuishi kifahari. Ni Yanga, Azam, Simba na Coastal Union. Lakini timu hizo zimeiachia Yanga manyoya.

VIJANA 14 NYOTA WA KIKAPU WAJIANDAA KWENDA USA


photo_a910d.png
Makamu wa Rais wa Shirikisho la mpira wa kikapu nchini-TBF Ndg. Phares Magesa akiwa na baadhi ya wachezaji nyota (vijana) wa timu ya Taifa ya Kikapu ya Tanzania ambao wanatarajiwa kwenda Marekani mwezi wa kumi katikati kwa ajili ya kambi ya Mafunzo katika Chuo Kikuu Cha Post-Connecticut, mafunzo hayo yataendeshwa na Kocha Albert Sokaitis akisaidiwa na Kocha Sconniers. Tuwasaidie VIJANA wetu kwa hali na mali ili washiriki vizuri Mafunzo hayo.www.tabasamuleo.blogspot.com

Friday 27 September 2013

NGASSA ALIPA TFF MIL 45 ZA SIMBA;




Mrisho Ngassa (katikati) akionyesha risti ya malipo aliyopewa TFF baada ya kulipa deni la mil 45, kushoto kwake ni mhasibu wa Yanga, Rose Msamila na kulia ni Afisa Habari wa Yanga Baraka Kizuguto

Kiungo mshambuliaji wa timu ya Young Africans Mrisho Khlafani Ngassa leo amelipa jumla ya mil 45, deni la mil 30 pamoja na faini ya mil 15 za klabu ya Simba SC kwa Shirikisho la Soka nchini TFF ili aweze kuitumikia timu yake kuanzia kesho.

KAMATI YA MAADILI YASHINDWA KUWAADHIBU SHAFFIH DAUDA NA WENZAKE




KAMATI YA MAADILI TFF YATANGAZA UAMUZI
Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imetangaza hukumu ya mashauri nane yaliyowasilishwa mbele yake kwa kumsafisha mlalamikiwa mmoja, kutowaadhibu zaidi washtakiwa sita na kuahirisha kusikiliza shauri moja baada ya mlalamikiwa kutokuwepo. (HM)

YANGA YAWALIPA NSAJIGWA NA MWASIKA




Baada ya vuta ni kuvute huku ikitishiwa kulimwa adhabu na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), klabu Yanga imekubali matokeo na kumalizana na wachezaji wake wa zamani, Stephano Mwasika na Shadrack Nsajigwa 'Fusso' waliokuwa wakiidai klabu hiyo zaidi ya Sh15 Milioni. (HM)

MMILIKI ARSENAL ASEMA WENGER ANABAKI ARSENAL




CHIFU wa Arsenal, Stan Kroenke anataka kocha Arsene Wenger abaki katika klabu hiyo kwa muda mrefu na kuleta taji la Ligi Kuu ya Enland Emirates. (HM)


Mfaransa huyo amekuwa katika klabu hiyo kwa miaka 17 na The Gunners ikiwa inakabiliwa na ukame wa mataji kwa msimu wa tisa sasa, amekuwa akipigwa zengwe aondoke, hususan kutokana na Mkataba wake kumalizika mwishoni mwa msimu.

MAGAZETI LEO JUMAMOSI


Thursday 26 September 2013

‘MASOGANGE AKITUA BONGO TU NDOA’

Stori: Imelda Mtema
MCHUMBA wa ‘video queen’ maarufu Bongo, Agnes Jerald ‘Masogange ‘, Evance Komu amefungua kinywa chake na kusema; siku mchumba wake huyo atakapotia miguu nchini, wanafunga ndoa.
Masogange kwa sasa (juzi) yupo nchini Afrika Kusini alikokuwa akikabiliwa na kesi ya madawa ya kulevya ambapo alifanikiwa kuwa huru baada ya kulipia faini ya randi 30,000 (shilingi 4,800,000) aliyoamriwa na Mahakama ya Kempton.
Akizungumza na gazeti hili hivi karibuni mara baada ya Masogange kuachiwa, Evance alisema anamshukuru Mungu kwa kesi hiyo kumalizika na kinachofuata kwenye uchumba wao ni ndoa tu.
Evance aliweka bayana kuwa kinachomsukuma afanye uamuzi huo kwa sasa ni kutokana na jinsi alivyoguswa na changamoto kubwa alizopitia mchumba wake hivyo ameona kuna kila sababu ya kumuoa kabisa ili apate faraja ya milele.
“Mchumba wangu amepitia majaribu ya kutosha na mimi sioni muda wa kupoteza tena, akitua tu Bongo kinachofuata ni ndoa nina imani itakuwa ndiyo jambo kubwa la kumfariji na kumpa upendo wa hali ya juu,” alisema Evance pasipo kutaja siku ambayo mchumba wake atarejea.
Katika kesi hiyo iliyokuwa ikimkabili Masogange, alishikiliwa na mwenzake Melisa Edward ambaye naye aliachiwa huru kwa kukosekana na hatia.

AMANDA AZOMEWA NA MASHABIKI

www.tabasamuleo.blogspot.com

Stori: Brighton Masalu
MWIGIZAJI wa sinema za Kibongo, Tamrina Posh ‘Amanda’ amejikuta katika wakati mgumu wa kuzomewa  kutokana na kukatiza kitaa akiwa na nguo iliyombana na kuonesha makalio yake yaliyojazia.
Tamrina Posh ‘Amanda’.
Kwa mujibu wa mtoa taarifa,  tukio hilo lilichukua nafasi Ijumaa iliyopita maeneo ya Mwenge, jijini Dar ambapo msanii huyo alikuwa ameenda kwa ajili ya kununua mahitaji mbalimbali ndipo kundi la wanaume wakware lilipoanza kumzomea.
Tukio hilo lilimfanya Amanda apoteze amani ghafla na kuamua kutimka zake eneo hilo huku akiwashangaa. Paparazi wetu hakuwa nyuma, alimpigia simu na kumuuliza kulikoni?
“Daah! Ilikuwa kero kweli, wanaume wazima wanaacha kazi zao na kuanza kunizomea huku wakiniambia kuwa ni dawa za Kichina. Lakini ukweli ni kuwa hii ni asili yangu na si Mchina,” alisema Amanda.

Tuesday 24 September 2013

MANJI AOSHA JINA ,ASEMA ETI YANGA SHWARI WALA HAKUNA MGAWANYIKO


Manji 21 55726
MWENYEKITI wa Yanga SC, Alhaj Yussuf Mehboob Manji amesema hakuna mgawanyiko ndani ya klabu hiyo na habari kwamba Seif Ahmed 'Magari' ametengwa ni uzushi, lakini habari za ndani kutoka kwenye klabu hiyo zinasema uongozi unaamini unahujumiwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF). (HM)WWW.TABASAMULEO.BLOGSPOT.COM

LULU MPYA AZALIWA


lulu1 cb52f
IMENICHUKUA saa kadhaa kuzungumza na mwigizaji nyota katika tasnia ya filamu za Bongo, Elizabeth Michael 'Lulu', hakika yeye ni Lulu kama lilivyo jina lake. (HM)
Kwa wakati huu msanii huyu ni lulu kweli katika tasnia ya filamu za Bongo Movie. Inaaminika kuwa binti huyo ambaye ni hivi karibuni tu alifikisha umri wa kuhesabiwa kuwa ni mtu mzima (miaka 18), naye ameingia katika kundi la wasanii wa kike wasiokamatika kwa kiwango.www.tabasamuleo.blogspot.com

MOYES ASIRUDIE MAKOSA AU TUJIANDAE NA AIBU YA KUKOSA CHAMPIONS LEAGUE



    320158_heroa_ba0fa.jpg
Nilinyanyuka kwenye kochi la nyumbani kwangu nikiwa mzito na kwenda kulala moja kwa moja ikiwa ni mapema sana kuliko kawaida yangu. Hii ilikuwa baada ya kuangalia timu yangu niipendayo ikadhalilishwa katika dimba la Etihad usiku wa jumapili ya wiki iliyopita. Nilijiuliza swali moja tu hivi ni kweli hata kuna ushindani mkubwa msimu huu kama inavyosemekana baina ya vilabu viwili vya jiji la Manchester.(P.T)www.tabasamuleo.blogspot.com

Monday 23 September 2013

BABA WEMA MAUTUUTI

Stori:   Imelda Mtema

MasIkini! Baba mzazi wa Miss Tanzania mwaka 2006 ambaye pia ni staa mkubwa wa filamu, Wema Sepetu, mzee Isaac Abraham Sepetu yupo kitandani akiwa amepooza upande mmoja wa mwili wake.

Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi, mwishoni mwa wiki iliyopita aliiwakilisha serikali kwenda kumjulia hali mzee huyo ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo visiwani Zanzibar na balozi katika nchi mbalimbali ambaye yupo nyumbani kwake Sinza-Mori, Dar.

Katika hali ya kusikitisha, mama mzazi wa Wema, Mariam Sepetu, aliliambia gazeti hili ambalo lilikuwa limeongozana na Nchimbi kuwa, mume wake alipatwa na ugonjwa huo akiwa kazini Zanzibar, ingawa kwa muda mrefu amekuwa akisumbuliwa na kisukari.

Alisema baada ya kupata taarifa za ugonjwa huo,…
Stori:   Imelda Mtema
MasIkini! Baba mzazi wa Miss Tanzania mwaka 2006 ambaye pia ni staa mkubwa wa filamu, Wema Sepetu, mzee Isaac Abraham Sepetu yupo kitandani akiwa amepooza upande mmoja wa mwili wake.
Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi (kulia), akimjulia hali mzee Isaac Abraham Sepetu.
Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi, mwishoni mwa wiki iliyopita aliiwakilisha serikali kwenda kumjulia hali mzee huyo ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo visiwani Zanzibar na balozi katika nchi mbalimbali ambaye yupo nyumbani kwake Sinza-Mori, Dar.www.tabasamuleo.blogspot.com

HUKUMU YA MASOGANGE.. MCHEZO UMECHEZWA!

“Hivi jamani, hiki sasa ni kiini macho. Tuliambiwa lakini watatoka tu. Mamlaka ya mapato kule Sauzi waliona ni madawa ya kulevya, mahakama ikaona ni kemikali hatari, mnadhani nani mkweli hapo?”
Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe wakati akionyesha picha ya Masogange kwa wanahabari.
Stori:  Waandishi Wetu
VIDEO Queen wa Bongo, Agnes Gerald Waya ‘Masogange’ na shosti yake, Melissa Edward wapo huru kufuatia kesi iliyokuwa ikisikilizwa nchini Afrika Kusini ya kukamatwa na madawa ya kulevya aina ya Crystal Methamphetamine ya Sh. bilioni 6.8, lakini baadhi ya wadau nchini wanasema kuna mchezo umechezwa, Ijumaa Wikienda limebaini mambo ya kushangaza nyuma ya pazia.
Masogange na Melissa walikamatwa Julai 5, mwaka huu kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oliver Tambo uliopo Kempton Park jijini Johannesburg nchini humo. Wawili hao wameishi mahabusu kwa saa 1824.
MMOJA HURU, MMOJA AHUKUMIWA
Uhuru wa Masogange ni baada ya Mahakama ya Kempton jijini Johannesburg kumtia hatiani kwa kuingiza kemikali hatari nchini humo, akatakiwa kulipa faini ya randi 30,000 (Sh. milioni 4.8 za Bongo) au kifungo cha miaka 2 jela.
Melissa yeye hakukutwa na hatia kwa vile ilibainika mizigo aliyokutwa nayo aliombwa na Masogange amsaidie kubeba baada ya kukutana ndani ya ndege ya Shirika la South Africa Airlines.
Agnes Gerald Waya ‘Masogange’.
KUMBE SI CRYSTAL MATHAMPHETAMINE
Habari kutoka nchini humo zinasema mdhamini wa Masogange (jina halijapatikana) alipigana kuhakikisha staa huyo na nduguye ambaye amezaliwa naye kwa mama mkubwa wanakuwa huru na kurejea Bongo.
Katika kupigana huko, mdhamini huyo alifurahia matokeo ya uchunguzi wa mkemia mkuu wa serikali ya nchi hiyo kuyaona madawa hayo kuwa si Crystal Methamphetamine bali ni Ephedrine ambayo si unga ila ni kemikali hatari ambayo ikichanganywa na dawa nyingine hupatikana unga halisi.www.tabasamuleo.blogspot.com

NAPOLI YAILAZA AC MILAN 2-1, BALOTELLI AKOSA PENATI, ALIMWA KADI NYEKUNDU

Mshambualiaji Mario Balotelli akitulizwa na mchezaji mwenzake wa Milani. (HM)
balotelli2 8570f

pepe 88285
MSHAMBULIAJI Mario Balotelli amekosa penalti kwa mara ya kwanza maishani mwake wakati AC Milan ikilala 2-1 nyumbani katika mchezo wa Serie A dhidi ya vinara Napoli Jumapili hii.
Balotelli, ambaye amefunga penalti zake zote 21 za awali katika mechi rasmi, alishuhudia mkwaju wake ukiokolewa na kipa Pepe Reina dakika ya 60.

WACAMEROON WAMGOMEA SAMUEL ETO’O KUSTAAFU

etoo 9a7ba
BAADA ya kupangwa na vigogo kwenye mchujo wa kufuzu Kombe la Dunia, Kocha Msaidizi wa Cameroon, Martin Ndtoungou, amesema bado wanamhesabu straika Samuel Et'o kuwa nahodha wao licha ya kudaiwa kwamba amestaafu kuichezea timu hiyo. (HM)
Eto'o aliripotiwa kuwaeleza wenzake kwamba mechi dhidi ya Libya iliyofanyika wiki iliyopita ilikuwa ya mwisho kwake kuichezea Cameroon, lakini mashabiki wengi wa timu hiyo wanaamini presha ya mchezo ndicho kitu kilichomsukuma fowadi huyo kuibuka na kauli ya kustaafu soka la kimataifa.www.tabasamuleo.blogspot.com

P SQUARE WANATISHA AFRIKA

SQUARE1 89dc2KUNA jambo moja ambalo mashabiki wa timu ya soka ya Arsenal wa Bongo wanajivunia kwa sasa. Unajua hao mashabiki wamefanya nini? Wamegeuza kibwagizo cha wimbo maarufu wa 'Personally' unaotamba kwa sasa wakaupa jina la 'Arsenally'. 
(HM)Wimbo huo ni wa wakali wa muziki wa Afrika kwa sasa ambao ni Peter na Paul Okoye wa Nigeria. Kimuziki wakali hao wanajulikana kwa jina la P-Square.www.tabasamuleo.blogspot.com

Sunday 22 September 2013

MAN UNITED MAJANGA yalala kwa CITY

 Man City yainyuka Man United 4-1 katika mechi iliyoisha muda mfupi ulopita. Mcheki Yaya Toure anavyoshangilia goli hapa. Haya sasa, hapa twasema Manuel Pellegrini kamzidi David Moyes ujanja, au hizi ni mbio za sakafuni tu? PICHA | AFP
UNITED MAJANGA BPL: Man City yainyuka Man United 4-1 katika mechi iliyoisha muda mfupi ulopita. Mcheki Yaya Toure anavyoshangilia goli hapa. Haya sasa, hapa twasema Manuel Pellegrini kamzidi David Moyes ujanja, au hizi ni mbio za sakafuni tu? PICHA | AFP
 

MAKALA: VITA YA FELLAINI DHID YA YAYA TOURE ITACHANGIA SANA MATOKEO YA MWISHO YA MANCHESTER DERBY LEO HII



Mbio za usajili wa kiungo wa kati katika klabu ya Manchester United zilileta vituko na maneneo mengi sana katika dirisha la


Cesc Fabregas alikuwa chaguo la kwanza lakini kadri muda ulivyokuwa ukienda ndivyo ilivyoonekana wazi asingeweza kuondoka Barca. Kiungo wa Athletic Bilbao Ander Herrera alikuwa kiungo mwingine aliyetakiwa kama ilivyokuwa kwa Luka Modric. Na wakati Arsene Wenger akivunja kibubu na kulipa kiasi cha £42.5million kwa ajili ya Mezut Ozil katika siku ya mwisho ya usajili, David Moyes akarudi kwenye klabu yake ya zamani na kumsajili mchezaji wa Everton Marouane Fellaini kwa ada ya uhamisho wa £27.5m – usajili ambao umemfanya mchezaji wa zamani wa United Teddy Sheringham kusema kwamba klabu yake ya zamani imemsajili mtu asiye sahihi.


Wakati ikiwa bado mapema sana, kiwango cha United katika mchezo wa Champions League dhidi ya Bayer Leverkusen, ambao Fellaini alianza, unaonyesha kwamba Moyes alimpata mchezaji ambaye alikuwa anatakiwa na kuliliwa sana Old Trafford.

MPIRA UMEKWISHA, YANGA 2- 3 AZAM FC

YangaVsAzam_cee32.pngFULL TIME AZAM 3-2 YANGA

DK 90: Gooo Joseph Kimwaga anaipatia Azam bao la 3.

DK 80: Timu zinashambuliana kwa zamu

DK 69 Kipre Tchetche anapiga penati na kuisawazishia Azam.

DK 68 Azam wanapata penati baada ya Kelvin Yondan kuunawa mpira.

Dakika ya 66, Hamis Kiiza anaipatia Young Africans bao la pili

Azam FC 1 - 2 Young Africans
Dakika ya 60, Azam FC 1 - 1 Young AfricansAnaingia Hamis Kiiza kuchukua nafasi ya Jerson Tegete


DK 50: Didier Kavumbagu anaisawazishia Yanga

Kipindi cha pili cha mchezo kimeanza, Azam FC 1 - 0 Young Africans

Dk 45 HALF TIME! Azam 1-0 Yanga

Dk 43 Mbuyu Twite anapiga shuti kali kuelekea lango la Azam lakini mpira unagonga mwamba na kutoka nje.

OMMY DIMPOZ AWADATISHA MASHABIKI WA MARYLAND NCHINI MAREKANI

Mashabiki waki-show love kwa Ommy Dimpoz.


Msanii mahiri wa muziki wa Bongo Flava, Faraji Nyembo 'Ommy Dimpoz' akipagawisha wakazi wa Maryland nchini Marekani jana.
Mashabiki waki-show love kwa Ommy Dimpoz.…

MTANGAZAJI WA 100 KISS FM AUWAWA KATIKA TUKIO BAYA LILITOKEA KENYA

Mtangazaji wa habari katika kituo cha redio cha Kiss FM kwa jina la ''Ruhila Aditya'' ni miongoni mwa waliopoteza maisha yao katika shambulizi hilo.
 
 
PICHA  ya enzi za
uhai wake ''Ruhila Aditya''

HUYU HAPA , REDD'S MISS TANZANIA 2013 PHOTOGENIC HAPPINESS





MISS Tanzania 2013, Happiness Watimanywa akipunga mkono mara baada ya kuvikwa taji la Redd’s Miss Tanzania 2013 usiku wa Septemba 21, Ndani ya Ukumbi wa Mlimani City na kuwashinda warembo wenzake 29.



Na Father Kidevu Blog

HATIMAYE kitendawili cha nani atanyakua taji la Redd’s Miss Tanzania 2013 kimeteguliwa usiku huu na mrembo Happiness Watimanywa kutoka Mkoa wa Dodoma na Kanda ya Kati kufanikiwa kutawazwa Mshindi wa taji hilo na kuwashinda warembo wengine 29 waiokuwa wakiwania taji hilo.

Nyota ya Happiness ilionekana dhahiri kung’aa vyema katika fainali hizo mwaka huu tangu pale alipofanikiwa kutwaa taji la Miss Tanzania Photogenic 2013 na kuwa mrembo wa kwanza kuingia nusu fainali.

Wakati Happiness akinyakua Taji hilo pamoja na zawadi ya Gari na kitita cha shilingi Milioni 8 nafasi ya pili ilikwenda kwa mrembo Latifa Mohamed kutoka Kitongoji cha Kigamboni na Kanda ya Temeke na nafasi ya Tatu ikienda kwa Miss Tanzania Sports Woman, Clara Bayo.

Pamoja nao warembo wengine walio ingia hatua hiyo ya tano bora ni Lucy Tomeka na Elizabeth Prety.

Hii ndio tano bora ya Redd's Miss Tanzania 2013. Je nani hapa ataondoka na taji, gari na kitita cha Milio ni 8? Warembo hao kutoka kushoto ni Happiness Watimanywa (Miss Photogenic), Elizabeth Pretty, Clara Bayo (Miss Sports Women), Lucy Tomeka na Latifa Mohamed.

www.tabasamuleo.blogspot.com



Fainali za Miss Tanzania 2013 ndio zinaendelea usiku huu ndani ya Mlimani City jijini Dar es Salaam. Gari ndo hilo hapo Je nani ataingia ndani na kuliendesha? Tusubiri Majaji. Hadi sasa Top 5 ndo ishatajwa.