Pages

ELIMU KWANZA.

ELIMU KWANZA.
FEDHA SIO KIPAUMBELE CHETU.

Monday 23 September 2013

NAPOLI YAILAZA AC MILAN 2-1, BALOTELLI AKOSA PENATI, ALIMWA KADI NYEKUNDU

Mshambualiaji Mario Balotelli akitulizwa na mchezaji mwenzake wa Milani. (HM)
balotelli2 8570f

pepe 88285
MSHAMBULIAJI Mario Balotelli amekosa penalti kwa mara ya kwanza maishani mwake wakati AC Milan ikilala 2-1 nyumbani katika mchezo wa Serie A dhidi ya vinara Napoli Jumapili hii.
Balotelli, ambaye amefunga penalti zake zote 21 za awali katika mechi rasmi, alishuhudia mkwaju wake ukiokolewa na kipa Pepe Reina dakika ya 60.

Hata hivyo, 'Supermario' aliifungia Milan dakika ya 90 na ushei kabla ya kuonyeshwa kadi ya pili ya njano na kutolewa nje miwishoni mwa mchezo. Mabao ya Napoli yalifungwa na Britos dakika ya sita na Higuaín dakika ya 54 pasi ya Zuniga. Chanzo: binzubeiry

No comments:

Post a Comment