Pages

ELIMU KWANZA.

ELIMU KWANZA.
FEDHA SIO KIPAUMBELE CHETU.

Saturday 21 December 2013

ONA PICHA ZA JINSI SIMBA ALIVYO MCHAPA YANGA JANA NA SHAMRA SHAMRA ZA KUPOKEA KOMBE NA MASHABIKI WALIOZIMIA.


Wachezaji wa Simba na Yanga wakisalimiana.

Kikosi cha Simba.

Kikosi cha Yanga.

Benchi la ufundi la timu ya Simba.

Benchi la Ufundi la Yanga.

Henry Joseph wa Simba (kushoto) akichuana na beki wa Yanga, David Luhende.

Henry Joseph wa Simba (kushoto) akichuana na beki wa Yanga, David Luhende.

Mashabiki wa Simba wakishangilia bao la kwanza la timu yao.

Raha ya ushindi.

Furaha kwa Simba.



Hamisi Kiiza akitafuta mbinu za kumtoka, Ramadhani singano.

Ivo Mapunda akiruka juu kuokoa moja ya hatari langoni mwake.

Mashabiki wa Yanga wakiwa hawaamini kilichotokea uwanjani baada ya kuchapwa 3-1 na watani zao wa jadi Simba.

Juma Kaseja akibembelezwa na Mbuyu Twite baada ya kusababisha

Mmoja wa mashabiki wa Yanga akitolewa nje baada ya kuzimia uwanjani.

Emmanuel Okwi akimtoka beki wa Simba.

Wachezaji wa akiba wa Simba wakishangilia baada ya filimbi ya mwisho.

Kocha wa Simba, Zdravko Logarusic akishangilia baada ya timu yake kuibuka na ushindi wa 3-1.
Wachezaji wa Simba wakimnyanyua juu kocha wao, Zdravko Logarusic mara baada ya kumalizika kwa mchezo maalumu wa Nani Mtani Jembe uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Simba ilishinda 3-1.









Waziri wa Sheria na Katiba, Mathias Chikawe akimkabidhi kombe nahodha wa Simba Haruna Shamte.



BAADA YA KIPIGO CHA 3-1 YANGA KUITISHA MKUTANO NA WAANDISHI WA HABARI KESHO, MINZORO AWAPONDA KINA KAVUMBAGU



Wakati uongozi wa klabu ya Yanga
umeitisha mkutano na waandishi wa
habari kesho (Desemba 22), kocha
msaidizi wa mabingwa hao, Fred
Felix Minziro amesema wakati wa
kupanga timu kwa mazoea sasa
umekwisha na wachezaji wanaocheza
soka la mdomoni hawana nafasi
katika timu yao.

Wazaramo: Kabila lenye sherehe lukuki, usipochangia, kushiriki unatengwa



watoto wakipongezwa na wazazi baada ya kutoka jandoni katika mkoa wa pwani. Picha ya Maktaba
Na Aziza Nangwa, Mwananchi
Tanzania ni nchi iliyojaliwa kuwa na makabila zaidi ya 120, yaliyounganishwa na lugha moja ya taifa ambayo ni Kiswahili. Miongoni mwa makabila hayo ya Tanzania, limo Kabila la Wazaramo, ambalo linapatikana katika mikoa ya Pwani na Dar es Salaam.

MATOKEO | Liverpool 3-1 Cardiff City

(1-0) Luis Suárez (25')
(2-0) Raheem Sterling (42')
(3-0) Luis Suárez (45')
(3-1) Jordon Mutch (58')

Liverpool sasa kileleni EPL

GONGA LIKE KAMA UMEPENDA MATOKEO

www.hakileo.blogspot.com

SIMBA NDIE MTANI JEMBE,CHAPA YANGA 3-1 OKWI AWAOKOA,KASEJA HOI.

Dakika chache zilizopita pale jijini Dar kunako mitaa ya TMK Simba sc wameicharaza timu ya Yanga kwa mvua ya magoli 3-1.

Emanueli Okwi ndie alifunga goli la kufuta machozi kwa Yanga huku Golikipa wa yanga Juma Kaseja akidondokwa na machozi mara baada ya kitundikwa goli la tatu.

Kilicho vutia kingine mara baada ya mchezo kuisha ni kitendo cha wachezaji watimu zote mbili kubadilishana jezi.

www.tabasamuleo.blogspot.com

Friday 20 December 2013

BLOGU YA TABASAMU LEO NA MKURUGENZI WA KAMPUNI YA HAKI LEO OSCAR SAMBA ANAWATAKIA MPAMBANO MWEMA WA SIMBA NA YANGA, LEO JIJINI DAR.

PEP GUARDIOLA AONGOZA KULIPWA MSHAHARA MKUBWA DUNIANI KWA MAKOCHA, MOURINHO WA PILI


Kiboko yao: Kocha wa Bayern Munich, Pep Guardiola ndiye anayelipwa zaidi duniani
MAKOCHA WANAOLIPWA ZAIDI DUNIANI
1 Pep Guardiola, Bayern Munich, £14.8m
2 Jose Mourinho, Chelsea, £8.37m
3 Marcelo Lippi, Guangzhou, £8.34m
4 Arsene Wenger, Arsenal, £6.89m
5 Fabio Capello, Russia, £6.51m
6 Carlo Ancelotti, Real Madrid, £6.26m
7 David Moyes, Man United, £4.92m
8 Tata Martino, Barcelona, £4.5m
9 Jurgen Klopp, Borussia Dortmund, £3.59m
10 Manuel Pellegrini, Man City, £3.47m
11 Jorge Jesus, Benfica, £3.34m
12 Brendan Rodgers, Liverpool, £3.25m
13 Sam Allardyce, West Ham, £2.95m
13 Roy Hodgson, England, £2.95m
15 Roberto Mancini, Galatasaray, £2.92m
15 Rafa Benitez, Napoli, £2.92m
17 Luciano Spaletti, Zenit, £2.75m
18 Claudio Ranieri, Monaco, £2.5m
18 Laurent Blanc, PSG, £2.5m
18 Antonio Conte, Juventus, £2.5m
18 Cesare Prandelli, Italy, £2.5m
22 Massimiliano Allegri, Milan, £2.34m

ONA PICHA ZAIDI YA 15,Jinsi Diamond alivyoenda kuwapa zawadi za msimu wa sikukuu watoto yatima Buguruni.



Diamond ametumia siku ya leo Dec 20, 2013 kwenda kutembelea,kutoa zawadi na kula pamoja na watoto na walezi wa kituo cha watoto yatima huko Buguruni Malapa House.

Hawa ndiyo mawaziri waliotenguliwa majukumu yao


Kufuatia majadiliano yanayoendelea Bungeni kuhusu ripoti iliyotolewa na kamati ya ardhi maliasili na utalii, Rais Jakaya Kikwete ametengua majukumu ya mawaziri wanne wa wizara za Maliasili na Utalii,Mambo ya Ndani,Ulinzi na
Jeshi la kujenga Taifa,pamoja na Wizara ya Mifugo na Uvuvi.

Kufuatia maamuzi hayo mawaziri wa Wizara hizo ambao ni Balozi Khamis Kagasheki waziri wa mali asili na utali ambae jna alikwisha kujiuzulu,Shamsi Vuai Nahodha waziri wa ulinzi na usalama,Emmanuel Nchimbi waziri wa mabo ya ndani na Mathayo David Mathayo waziri wa mifugo wameondolewa rasmi nyadhifa zao za uwaziri katika wizara hizo hadi uamuzi mwingine utakapotangazwa na Rais.

Uamuzi huu wa Ris Kikwete umetangazwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda wakati akijibu hoja zilizotolewa na Wabunge.
KWA HABARI KAMA HIZI ZAIDI SOMA www.hakileo.blogspot.com

Extra Bongo; bendi inayoongoza kwa burudani ya ‘unenguaji’ nchini

Mashabiki waliowahi kuhudhuria maonyesho ya bendi ya muziki wa dansi nchini ya Extra Bongo watakubaliana nami kwamba ina wacheza shoo (madansa) makini, wenye uelewa mpana na pengine kukonga zaidi nyoyo za mashabiki katika tasnia hiyo.

Linah na Recho pete na kidole

Kawaida imezoeleka kwamba wasanii wanaofanya muziki wa aina moja huwa hawapatani na mara nyingi hushindwa kuwa karibu kutokana na kunyang’anyana mashabiki, kugombea shoo au ubize unaowafanya washindwe kukutana mara kwa mara.

GUUS HIDDINK KOCHA MPYA UHOLANZI



Guus Hiddink amesaini mkataba wa miaka minne na timu ya taifa ya Uholanzi. (HM)
Kocha huyo wa kidachi amekubali kuchukua majukumu ya kocha sasa wa timu hiyo ya taifa Louis van Gaal baada ya fainali za kombe la dunia mwaka 2014 kwa miaka miwili kama kocha, na kufuatiwa na miaka mingine miwili kama mkurugenzi wa ufundi wa timu hiyo ya taifa.

FIFA WAMETIA BARAKA OKWI KUUZWA YANGA



The Acting Competitions Director of the Uganda FA, Decolas Kiiza, has clarified that FIFA cleared striker Emmanuel Okwi to join Tanzanian league champs Young Africans FC. (HM)
"Yes we wrote to FIFA and they said the player was free to transfer," Kiiza told MTNFootball.com.
Early this week the FA's Chief Executive Officer, Edgar Watson, said they had contacted FIFA to get more clarification on the issue.
Young Africans signed Okwi early this week on a two-year deal and yet FIFA had provisionally released the player to join local side SC Villa from Tunisia's Etoile du Sahel.

Thursday 19 December 2013

Nicki Minaj aingia rasmi kwenye ulimwengu wa movie, hii hapa ni trailer ya movie hiyo.



Nicki Minaj alitajwa kuwa namba 4 na Forbes.com kwenye list ya wasanii wa Hiphop walioingiza pesa nyingi sana kuanzia June 2012 hadi June 2013 kwa kuingiza dola millioni 29 kutokana na kazi yake ya muziki,American Idol,Pepsi na vitu vingine.

DAKIKA 90 SARE MTANI JEMBE, PENALTI ZITAAMUA MSHINDI SIMBA NA YANGA JUMAMOSI


Mechi iliyopita ya watani wa jadi iliisha kwa sare ya 3-3 Uwanja wa Taifa, lakini Jumamosi lazima mshindi apatikane
Na Mahmoud Zubeiry, Dar es Salaam
IWAPO dakika 90 za mchezo wa Nani Mtani Jembe baina ya Simba SC na mahasimu wao, Yanga zitamalizika kwa sare Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, basi moja kwa moja sheria ya mikwaju ya penalti itachukua nafasi yake, imeelezwa.

YANGA YAUZA MCHEZO milioni 90



NA MJENGWA BLOG

OKWI: NIKIPANGWA KESHO NITACHEZA VIZURI NA KUFUNGA, NGASSA NA KIIZA WOTE NIMECHEZA NAO TIMU MOJA


Okwi kushoto akiwa na Mussa Katabaro, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga

Na Mahmoud Zubeiry, Dar es Salaam
MSHAMBULIAJI mpya wa Yanga SC, Emmanuel Arnold Okwi amesema japokuwa hajapata fursa ya kufanya mazoezi na timu yake mpya, lakini hana wasiwasi akipangwa Jumamosi katika mechi dhidi ya timu yake zamani, Simba SC atacheza kwa uelewano mzuri na wachezaji wenzake wapya, kwa kuwa yeye ni mchezaji wa kimataifa.
Okwi aliyewasili jana Dar es Salaam akitokea kwao, kampala, Uganda kuja kuanza kuutumikia Mkataba wake wa miaka miwili, aliiambia BIN ZUBEIRY jana kwamba hana shaka akipangwa atacheza vizuri na kuwafurahisha mashabiki wa timu yake hiyo mpya kwa sababu ana uzoefu wa kimataifa.
“Kwanza mtu kama (Mrisho) Ngassa nimecheza naye Simba SC, na (Hamisi) Kiiza tunacheza naye timu ya taifa (Uganda), hakuna wasiwasi, mimi nikipangwa nao tutacheza kwa uelewano sana pale mbele na nitafunga,”alisema Okwi.

Wednesday 18 December 2013

SHIRIKISHO LA SOKA UGANDA LAANDIKA BARUA FIFA KUULIZIA UHALALI WA USAJILI WA OKWI YANGA.


NA SHAFFIH DAUDA
Shirikisho la soka nchini Uganda limeandika barua kwenda FIFA likisaka ufafanuzi kuhusu uhamisho wa mshambuliaji Emmanuel Okwi aliyeuzwa kutoka SC Villa kwenda Yanga.

Siku ya jumatatu, Okwi alirirpotiwa kujiunga na mabingwa wa Tanzania bara klabu ya Yanga kwa ada ya uhamisho wa $100,000 kwa mkataba wa miaka miwili, na huku huko nyuma FIFA ilimuidhinisha Okwi kujiunga kwa mkopo na klabu ya SC Villa akitokea klabu ya Tunisia Etoile du Sahel.

SAKATA LA UONGOZI WA SHIRIKISHO LA MPIRA WA KIKAPU NCHINI LAENDELEA,MALUWE ADHIBITSHA KUGOMBEA NAFASI YA UKATIBU MKUU.


Wakati uchaguzi mkuu wa shirikisho la mpira wa kikapu Tanzania TBF ukitarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi huu, baadhi ya viongozi mchezo huo wameibuka na kuweka bayana baadhi ya mapungufu yaliyopo kwenye uongozi unaomaliza muda wake.

KIINGILIO MECHI YA MTANI JEMBE 5,000/-


NA MENGWA BLOGU
Kiingilio cha chini kwenye mechi ya Mtani Jembe kati ya Simba na Yanga itakayochezwa Jumamosi (Desemba 21 mwaka huu) ni sh. 5,000. Kiingilio hicho ni kwa viti vya rangi ya kijani ambavyo ni 19,648.

Kwa upande wa viti vya rangi ya bluu kiingilio ni sh. 7,000, viti vya rangi ya chungwa itakuwa sh. 10,000, VIP C kiingilio ni sh. 15,000, VIP B itakuwa sh. 20,000 wakati VIP A yenye viti 748 tu tiketi moja itapatikana kwa sh. 40,000.