Wednesday, 18 December 2013
Tottehnam inamtafuta kocha mwengine baada ya kumtimua Andre Villas Boas, na huenda Glenn Hoddle akachukua na fasi hio
Kocha wa Tottehnam Andre Villas Boas na Gareth Bale wakifurahia ushindiREUTERS/Eddie Keogh
Na RFI
Huenda meneja wa zamani wa Tottenham Hotspurs, Glenn Hoddle akarejea tena katika klabu hio kuziba pengo lililoachwa na kocha Andre Villa-Boas ambaye hapo jana alitimuliwa.
Boas alitimuliwa baada ya timu ya Tottehnam kuchapwa na Liverpool mabao 5-0.
Glenn Hoddle aliyeinoa Spurs kati ya mwaka 2001 na 2003, anatajwa kua miongoni mwa makocha ambao huenda wakaziba pengo hilo, na pia yupo karibu sana na mwenyekiti wa Spurs, Daniel Levy.
Kocha wa zamani wa Uingereza Fabio Capello, Meneja wa Swansea Michae Laudrup na mkurugenzi wa ufundi wa Tottehnam Franco Baldini, ni baadhi ya wengine wanaotajwa kua huenda wakachukua na fasi hio.
Wakati Tottenham wakitimua kocha kwa upande wake Meneja wa Liverpool Brenden Rodgers amesema hatua ya timu yake kuisambaratisha Tottenham kwa magoli 5 - 0 katika uwanja wao wa nyumbani wa White Hart Lane ni moja kati ya mechi ya viwango vya juu vilivyoonyeshwa na Liverpool katika kipindi cha uongozi wake.
Rodgers alishika hatamu ya kuinoa Liverpool mwaka 2012 ambapo kwa sasa timu hiyo ipo nafasi ya pili ikiwa nyuma ya Arsenal katika msimamo wa ligi kuu ya England.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment