Pages

ELIMU KWANZA.

ELIMU KWANZA.
FEDHA SIO KIPAUMBELE CHETU.

Monday 16 December 2013

HASSAN DILUNGA AANZA MAZOEZI NA KINA CHUJI, NIYONZIMA

KIUNGO mpya wa Yanga, Hassan Dilunga leo asubuhi ameanza mazoezi katika klabu yake mpya aliyojiunga nayo hivi karibuni akitokea Ruvu Shooting ya Pwani.

Dilunga alikuwa mchezaji wa pili kusajiliwa na Simba baada ya Yanga baada ya Juma Kaseja ili kutimiza matakwa ya kocha Ernie Brandts ambaye aliwataka wachezaji hao ili kuimarisha kikosi chake.
Kiungo huyo aliwasili katika mazoezi hayo yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Bora, Kijitonyama na kujiunga na wenzake walioanza mazoezi hayo wiki mbili zilizopita.

Dilunga alikuwa sambamba na nyota wengine wa Yanga waliokuwa wakizitumikia timu zao za taifa katika michuano ya Kombe la Chalenji iliyofanyika Kenya na kumalizika wiki iliyopita huku wenyeji wakitwaa ubingwa.
Wachezaji walioanza mazoezi leo sambamba na Dilunga ni Deo Munishi, Frank Domayo, Athuman Idd ‘Chuji’ na Mrisho Ngassa ambao walikuwa wakiichezea timu ya taifa ya Tanzania Bara maarufu kama Kilimanjaro Stars ambayo iliishia robo fainali ya michuano hiyo.

Muda mfupi baada ya mazoezi hayo, Dilunga alisema hawezi kuzungumza maneno mengi kwa kuwa ndiyo kwanza amejiunga na timu hiyo hivyo aachwe hadi atakapofanya mazoezi kwa siku kadhaa.
“Unajua siwezi kusema lolote hapa kama unavyoona mimi nimeanza mazoezi leo sasa hakuna ninalolijua katika timu lakini nikitulia kwa muda naweza kuwa na jambo la kuongea,” alisema Dilunga.
Yanga inafanya mazoezi kujiandaa na mechi yake dhidi ya Yanga itakayochezwa Jumamosi ijayo kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ambayo imeandaliwa na wadhamini wao Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).
Pia Yanga inajiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Bara itakayoanza Januari 25 mwakani. Maandalizi hayo ya Yanga pia yanahusu ushiriki wao wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika mwakani.

No comments:

Post a Comment