Pages

ELIMU KWANZA.

ELIMU KWANZA.
FEDHA SIO KIPAUMBELE CHETU.

Saturday 8 February 2014

LIVERPOOL YAICHANACHANA ARSENAL...AIBU TUPU ni 5-1

LIVERPOOL imewaadhiri Arsenal waliokuwa wanasifiwa wana ukuta mgumu, kwa kuwafumua mabao 5-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England jioni hii Uwanja wa Anfiled.
Mabao ya Liverpool leo yamefungwa na Skrtel dakika ya kwanza na 10, Sterling dakika ya 15 na 52 na Sturridge dakika ya 20.
Bao la kufutia machozi la Arsenal lilifungwa na Arteta dakika ya 69 kwa penalti. Ushindi huo, unaifanya Arsenal ibaki na pointi zake 55 katika nafasi ya pili baada ya kuchea mechi 25, wakati Liverpool imefikisha pointi 50 baada ya mechi 25 pia, ingawa inaendelea kubaki nafasi ya nne.

Furaha tupu: Wachezaji wa Liverpool wakishangilia ushindi wao mnono dhidi ya Arsenal leo

PICHA: YANGA WALIPOWANYOOSHA WACOMORO TAIFA LEO



Kiungo wa Komorozine Sports, Moidjie Ali akimdhibiti mshambuliaji wa Yanga, David Luhenda katika mchezo wa Ligi ya klabu Bingwa Afrika uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Yanga imeshinda 7-0

LIVE SCORE: YANGA SC 4-0 KOMOROZIE DE DEMONI, ARSENAL 0 LIVERRPOOL 4

Friday 7 February 2014


London, England. Milango ipo wazi kwa klabu kubwa za Ligi Kuu England kumsajili kiungo wa Bayern Munich, Toni Kroos ambaye mazungumzo ya mkataba wake mpya na klabu yake yamevunjika.

Kroos, amekuwa akifuatiliwa kwa karibu na Manchester United hasa wakati wa dirisha dogo la usajili ambalo lilifungwa Januari 31.

Kiungo huyo ambaye thamani yake ni Pauni 25 aliingia matatani wiki iliyopita baada ya kutolewa katika mchezo wa Ligi Kuu ya Ujerumani dhidi ya Stuttgart, jambo ambalo lilimchukiza.

Kitendo hicho kilimchefua kocha wake, Pep Guardiola ambaye ameamua kumwondoa katika kikosi chake.

Uamuzi huo unaungwa mkono na wakurugenzi wa Bayern ambao pia wamekataa kumwongezea mshahara Kroos kutoka Pauni 60,000 kwa wiki hadi kufikia Pauni 150,000.

Kroos, anataka alipwe mshahara mkubwa kama ilivyo kwa nyota wengine, Philipp Lahm, Bastian Schweinsteiger, Franck Ribery ambao wanalipwa Pauni 150,000 kwa wiki.

Kijana huyo mwenye umri wa miaka 24 amekuwa akieleza kutoridhishwa kwake na mwenendo na vitendo anavyofanyiwa kwenye klabu hiyo ya Allianz Arena.

Gazeti la Sportsmail wiki iliyopita liliripoti kuwa kocha wa Man United, David Moyes amekuwa akifuatilia kwa karibu hali ya kiungo huyo na hata kuwasiliana wakala wake.

Hata hivyo, Man United huenda ikakutana na upinzani mkali kutoka Man City, Chelsea, Arsenal na Liverpool, zote ambazo zimeelekeza macho yao kwa kijana huyo. Chanzo: mwananchi

SIMBA SC WAWEKA KAMBI SONY KWA AJILI YA MIGAMBO JUMAPILI


Kikosi cha Simba SC kimewasili mjini Tanga na kuweka kambi katika hoteli ya Sony Inn, tayari kwa mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya wenyeji wao, Mgambo Shooting Jumapili Uwanja wa Mkwakwani, mjini humo. Simba SC imewasili Tanga mchana wa leo ikitokea Morogoro, ambako jana ilikuwa na mchezo mwingine wa ligi hiyo dhidi ya wenyeji, Mtibwa Sugar na kutoka sare ya kufungana bao 1-1 Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

Wednesday 5 February 2014

Bill Clinton aingia kwenye kashfa nyingine ya kutoka nje ya ndoa yake

Bill Clinton rais zamani wa Marekani aliwahi kuingia kwenye kashfa kubwa ya kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Monica Lewinsky ambaye alikuwa na miaka 22 kipindi hicho akifanya kazi kama intern ndani ya White house.

PICHA KAMILI SIMBA NA MTIBWA JAMHURI, HANS POPPE NA MAESTRO KAMA 'WAMEPIGWA SHOTI'


Vita ya mabeki; Beki wa kushoto wa Simba SC, Issa Rashid 'Baba Ubaya' akigombera mpira na beki wa kulia wa Mtibwa Sugar, Hassan Ramadhani katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jioni ya jana Uwanja wa Jamhuri, Morogoro ambao ulimalizika kwa sare ya 1-1.


Rmadhani Singano 'Messi' wa Simba SC akitafuta mbinu za kumtoka beki wa Mtibwa Sugar, Hassan Ramadhani

BARCELONA YACHINJA 2-0 KOMBE LA MFALME, EL CLASICO LANUKIA FAINALI COPA DEL REY

TIMU ya Barcelona imejiweka kwenye nafasi nzuri ya kutinga Fainali ya Kombe la Mfalme baada ya jana usiku kuifunga Real Sociedad mabao 2-0 Uwanja wa Camp Nou.
Busquets alianza kuifungia Barcelona dakika ya 42 kabla ya Elustondo kujifunga dakika ya 60.
Barca sasa inaweza kukutana na wapinzani wao wakubwa Hispania katkka fainali ya michuano hiyo, Real Madrid ambayo jana imeifunga Atletico Madrid mabao 3-0.

La kwanza: Kiungo wa Barcelona, Sergio Busquets akishangilia baada ya kuifungia bao la kwanza Barca jana usiku

Tuesday 4 February 2014

BALOTELLI JAMANI KWELI 'MWEHU', HEBU ANGALIA ALIVYONYOA KAMA...

MSHAMBULIAJI wa AC Milan, Mario Balotelli amepamba vichwa vya habari tena baada ya kuibuka na mtindo mpya wa unyoaji kichwani.
Mshambuliaji huyo wa Italia jana usiku aliposti picha za mnyoo wake mpya katika akaunti yake ya Twitter.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 ameonekana wa kipekee kwa mnyoo huo hatari. "Nimemaliza kunyoa, sasa naenda zangu kulala," hayo ndiyo maneno yaliyoambatana na picha hizo.

Inaitwaje hii: Mario Balotelli ameweka kwenye akaunti yake ya Twitter jana usiku picha hii ya mtindo wake mpya unyoaji
Balotelli katika mtindo mpya wa nywele

RASMI TFF YASITISHA MATUMIZI YA TIKETI ZA ELEKTRONIKI


Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limesitisha matumizi ya tiketi za elektroniki kwenye viwanja vyote vyenye huduma hiyo ili kutoa fursa ya kufanyika tathmini ya kina kabla ya kuendelea tena.

Sunday 2 February 2014

Namna Jokate alivyom’sapraiz’ Wema On Stage Arusha.

Unaweza kujikuta ukishindwa kuielewa hii hali lakini inabidi ukubaliane na ukweli halisi wa hiki kilichotokea,Jokate na Wema historia yao ilianzia kwenye shindano la kumtafuta Miss Tanzania 2006 ambapo Mshindi alikua ni Wema Sepetu akifatiwa na Jokate kisha mshindi wa tatu akiwa Lissa Jensen.

ONA JINSI SIMBA SC ILIVYOTOA DOZI NENE JANA TAIFA


Kiungo wa Simba SC, Ramadhani Singano 'Messi' kushoto akiwatoka wachezaji wa JKT Oljoro ya Arusha jana katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Simba SC ilishinda 4-0.

LIBYA MABINGWA WAPYA CHAN - WAITANDIKA GHANA NA KUTWAA UBINGWA


Libya imepata ushindi wake wa kwanza wa kombe la taifa bingwa Afrika kwa mikwaju ya penalti 4-3 dhidi ya Ghana mjini Cape Town Afrika Kusini.

Mechi ya fainali kati ya nchi hizo mbili ilikamilika kwa sare tasa kabla ya Joshua Tijani wa Ghana kukosa bao la penalti na kuipa Libya ushindi wake.

CHELSEA, LIVERPOOL, ARSENAL WAJIANDAA KUISHTAKI MAN CITY KUVUNJA SHERIA YA "FINANCIAL FAIR PLAY" ILI WAFUNGIWE KUCHEZA CHAMPIONS LEAGUE MSIMU UJAO


Arsenal, Chelsea na Liverpool wanaweza kutumia kipengele kidogo kwenye sheria ya "financial fair play' ya UEFA ili kuibania Manchester City haki ya kucheza katika mashindano ya Champions league msimu ujao.

MADRID KUFANYA MATENGENEZO UWANJA WA BERNABEU


Raisi wa Real Madrid Florentino Perez jana alionyesha rasmi ramani mpya ya uwanja wa Santiago Bernabeu utakavyokuwa baada ya kufanyiwa marekebisho. Uwanja huo ambao ni mmoja wa miongoni mwa viwanja bora duniani unatarajiwa kuanza matengenezo hivi karibuni na unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa 2017017.