Pages

ELIMU KWANZA.

ELIMU KWANZA.
FEDHA SIO KIPAUMBELE CHETU.

Friday 7 February 2014


London, England. Milango ipo wazi kwa klabu kubwa za Ligi Kuu England kumsajili kiungo wa Bayern Munich, Toni Kroos ambaye mazungumzo ya mkataba wake mpya na klabu yake yamevunjika.

Kroos, amekuwa akifuatiliwa kwa karibu na Manchester United hasa wakati wa dirisha dogo la usajili ambalo lilifungwa Januari 31.

Kiungo huyo ambaye thamani yake ni Pauni 25 aliingia matatani wiki iliyopita baada ya kutolewa katika mchezo wa Ligi Kuu ya Ujerumani dhidi ya Stuttgart, jambo ambalo lilimchukiza.

Kitendo hicho kilimchefua kocha wake, Pep Guardiola ambaye ameamua kumwondoa katika kikosi chake.

Uamuzi huo unaungwa mkono na wakurugenzi wa Bayern ambao pia wamekataa kumwongezea mshahara Kroos kutoka Pauni 60,000 kwa wiki hadi kufikia Pauni 150,000.

Kroos, anataka alipwe mshahara mkubwa kama ilivyo kwa nyota wengine, Philipp Lahm, Bastian Schweinsteiger, Franck Ribery ambao wanalipwa Pauni 150,000 kwa wiki.

Kijana huyo mwenye umri wa miaka 24 amekuwa akieleza kutoridhishwa kwake na mwenendo na vitendo anavyofanyiwa kwenye klabu hiyo ya Allianz Arena.

Gazeti la Sportsmail wiki iliyopita liliripoti kuwa kocha wa Man United, David Moyes amekuwa akifuatilia kwa karibu hali ya kiungo huyo na hata kuwasiliana wakala wake.

Hata hivyo, Man United huenda ikakutana na upinzani mkali kutoka Man City, Chelsea, Arsenal na Liverpool, zote ambazo zimeelekeza macho yao kwa kijana huyo. Chanzo: mwananchi

No comments:

Post a Comment