
Vita ya mabeki; Beki wa kushoto wa Simba SC, Issa Rashid 'Baba Ubaya' akigombera mpira na beki wa kulia wa Mtibwa Sugar, Hassan Ramadhani katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jioni ya jana Uwanja wa Jamhuri, Morogoro ambao ulimalizika kwa sare ya 1-1.

Rmadhani Singano 'Messi' wa Simba SC akitafuta mbinu za kumtoka beki wa Mtibwa Sugar, Hassan Ramadhani

Messi na Hassan

Messi akipambana kuwatoka mabeki wa Mtibwa Sugar

Mshambuliaji wa Simba SC, Ali Badru akiwatoka mabeki wa Mtibwa Sugar

Kocha wa Mtibwa Sugar, Meck Mexime aliyeipa mgongo kamera akimtuliza Nahodha wake, Shaaban Nditi baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu kwenye mchezo huo

Beki wa Mtibwa Sugar, Juma Mpakala kushoto akipambana na mshambuliaji wa Simba SC, Ali Badru

Haroun Chanongo wa Simba SC kulia akigombea mpira na Jamal Mnyate wa Mtibwa Sugar

Mshambuliaji wa Simba SC, Amisi Tambwe akimtoka beki wa Mtibwa Sugar, Salvatory Ntebe, huku Messi akiwa tayari kutoa msaada

Kiungo wa Simba SC, Jonas Mkude akimtoka kiungo wa Mtibwa Shaaban Kisiga

Mshambuliaji wa Mtibwa Sugar, Juma Luizio akipasua katikati ya wachezaji wa Simba SC, Haroun Chanongo kulia na Jonas Mkude kushoto

11 walioanza Mtibwa Sugar leo

11 wa Simba SC walioanza leo

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera kulia akiwasalimi wachezaji wa Simba SC kabla ya mechi. Hapa amepeana mikono na beki Joseph Owino. Katikati ni Messi na kushoto Donald Mosoti

Wakubwa; Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe kulia ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili na Ibrahim Masoud 'Maestro' wakifuatilia mchezo huo
No comments:
Post a Comment