Pages

ELIMU KWANZA.

ELIMU KWANZA.
FEDHA SIO KIPAUMBELE CHETU.

Saturday 16 November 2013

NIGERIA YA KWANZA KUKATA TIKETI YA BRAZIL 2014 BAADA YA KUIFUMUA ETHIOPIA 2-0



Timu ya taifa ya Nigeria imekua nchi ya kwanza ya Afrika kukata tiketi ya kecheza. Fainali za Kombe la Dunia mwakani baada ya ushindi wa mabao 2-0 nyumbani dhidi ya Ethiopia leo. Victor Moses alifunga kwa penalti dakika ya 20 na Victor Obinna akaongeza la pili dakika ya 82 kwa mpira wa adhabu, hivyo Super Eagles kufuzu kwa ushindi wa jumla wa 4-1, baada ya awali kushinda 2- mjini Addis Ababa mwezi uliopita katika mchezo wa kwanza.
www.tabasamuleo.blogspot.com

Nikk wa pili ame-graduate Master of Arts in development management, hizi ni picha 5 kutoka kwenye graduation yake.



Nikki Wa Pili kutoka Weusi amemaliza degree yake ya pili (Masters) kwenye chuo kikuu cha Dar es salaam. Mkali huyu kutoka A town ameshiriki mahafali ya kumaliza masomo yake ya Master of Arts in development management kwenye ukumbi wa Mlimani city na hizi ni baadhi ya picha 5 kutoka kwenye graduation hiyo.


MALINZI KUFUNGUA MICHUANO YA UHAI 2013



Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi atafungua rasmi michuano ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 20 (U20) kwa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom mwaka huu.


Uzinduzi wa mashindano hayo utafanyika leo (Novemba 17 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam saa 2 kamili asubuhi. Mechi ya ufunguzi itakuwa ya kundi A kati ya Azam na Coastal Union.
Mechi nyingine za kesho ni kundi; Yanga na Mbeya City (saa 8 mchana- Uwanja wa Karume), kundi B ni Ruvu Shooting na Ashanti United (saa 4 asubuhi- Uwanja wa Karume), Oljoro JKT na Simba (saa 10 jioni- Uwanja wa Karume).

MIEZI KADHAA BAADA YA KUMPONDA - JOSE MOURINHO ASEMA CRISTIANO RONALDO NDIYE MCHEZAJI BORA KULIKO WOTE ALIOWAHI KUWAFUNDISHA'


Jose Mourinho amesema kwamba kumfundisha Cristiano Ronaldo walipokuwa Real Madrid kinabakia kuwa kitu muhimu na kizuri katika maisha yake.

Wawili hao walikaa pamoja kwa miaka mitatu ndani ya Santiago Bernabeu, huku Ronaldo akifunga jumla ya mabao 168 katika mechi 164 wakati Mourinho akiwa katika benchi la Bernabeu.

Friday 15 November 2013





Raisi wa Bayern Munich Uli Hoeness, anakabiriwa na kesi ya kukwepa kodi itakasomwa mwakani, jana alitokwa na machozi wakati akitangaza klabu yake kuvunja rekodi ya kuingiza mapato makubwa katika cha 113 years.
Katika mkutano wa mkuu wa klabu, Hoeness, ambaye alipokewa kwa shangwe, alishindwa kujizuia na kuanza kulia baada ya mabosi wenzie kumsifia kuiongoza vizuri timu hiyo na kupata mafanikio ya kushinda makombe matatu msimu uliopita.
Hoeness, ambaye anashtakiwa kwa kushindwa kulipa kodi kutoka kwenye fedha zake zilizopo katika moja ya benki huko Uswis.

Hoeness, amekuwa katika klabu hiyo kwa zaidi ya miaka 40 kama mchezaji, kocha na saa raisi, alizungumzia matatizo yake ya kisheria, akisema kwamba alifanya makosa na kushindwa kulipa kodi kutoka kwenye akaunti yake ya nje.
'Nilifanya makosa kutokulipa kodi katika uwekezaji kutoka nje. Sikuchukua mamilioni ya fedha na kuyatoa nje ya nchi," alisema Hoeness, baada ya kujifuta machozi. 'Nitapambana na matatizo.'


'Nina imani kubwa na utawala wa kisheria wa Bavarian.
'Ninatumaini kwamba story hii itakuwa na mwisho mzuri mpaka kufikia mwezi March. Na kama mpaka wakati huo nitaruhusiwa kuendelea kuwa hapa naahidi kuitumikia klabu hii mpaka pumzi yangu ya mwisho.'

BAADA YA KASEJA - HUYU NDIO MCHEZAJI MWINGINE ALIYESAJILIWA NA YANGA




Thursday 14 November 2013

Kiiza: Mechi 9, mabao 8! Niko juu bwana



Kiiza ambaye ni raia wa Uganda, hakucheza mechi za mwanzoni mwa msimu kwa sababu alikwenda Lebanon kwenye majaribio.
By DORIS MALIYAGA,MWANASPOTI
STRAIKA wa Yanga, Hamis Kiiza, ameridhika na kiwango alichokionyesha mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Bara baada ya kufunga mara nane katika mechi tisa.
Hata hivyo, amekiri kukutana na changamoto nyingi kikosini humo.
Kiiza ambaye ni raia wa Uganda, hakucheza mechi za mwanzoni mwa msimu kwa sababu alikwenda Lebanon kwenye majaribio lakini tangu aliporejea amepata nafasi alizotumia kufunga mabao hayo.

Dawa yako Kaseja inakuja




Juma Kaseja
By LASTECK ALFRED,MWANASPOTI MASTRAIKA wawili tegemeo wa Simba, Amissi Tambwe na Betram Mwombeki, wameingia msituni kufanya jambo ambalo si zuri kwa Yanga hususani mabeki wa timu hiyo na kipa wao mpya, Juma Kaseja.
Kaseja amesajiliwa Yanga kuongeza nguvu kwenye mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara na Ligi ya Mabingwa Afrika katika mechi zitakazochezwa mwakani.

USHIRIKINA KATIKA SOKA UPO HATA ULAYA ?




HEBU msomaji cheki jinsi wenzetu wa Ulaya wanavyofanya mambo yao ya kiufundi kistaili!
10. Paul Ince
Mtaalamu huyu wa zamani wa Man united, Liverpool na timu kadhaa nyinginezo alikuwa anahakikisha anakuwa wa mwisho kutoka katika chumba cha kubadilishia nguo katika kila mechi aliyocheza. Si hapo tu bali angesubiria hadi sekunde ya mwisho kabla mchezo kuanza ndipo angevaa jezi yake. Wadau hatujui hii ilimsaidia nini!
9. Laurent Blanc
Nani anakumbuka fainali za kombe la dunia mwaka 1998? Kama una kumbukumbu nzuri utajua kwamba beki wa zamani wa Ufaransa na kocha wa sasa wa timu hiyo hiyo laurent Blanc, alikuwa na utaratibu wa kubusu kipara cha kipa wao Fabien Barthez kabla ya kuanza kwa kila mechi. Sasa sijui alikuwa akionesha mapenzi yake kwa Barthez ama ilikuwa kwa ajili ya kupata bahati, ukweli ni kwamba ilisaidia kwani Ufaransa waliibuka mabingwa mwaka huo!

Tuesday 12 November 2013

Picha na kipande cha video mpya ya Rihanna itakayoka wiki hii vipo hapa



Baada ya video ya Pour it up Rihanna yupo tayari kutoa video nyingine Ijumaa hii. What Now ndiyo video ambayo inafuata na hapa kuna picha na kipande cha video hiyo.




www.tabasamuleo.blogspot.com

KAMPENI YA NANI MTANI JEMBE SASA YAHAMIA KANDA YA KASKAZINI.




Wakazi wa eneo la Maji ya Chai, Arusha wakiangalia burudani iliyokuwa inatolewa na timu ya kampeni ya ‘Nani Mtani Jembe’ inayohusisha mashabiki Simba na Yanga, ili kuzipigia kura timu zao na kushinda kitita kingi kati ya Tsh.100 milioni zilizotelewa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager ambao ndio wadhamini wa timu hizo na timu ya Taifa. Timu hiyo ipo kanda ya Kaskazini na Mashariki inayojumuisha mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Singida na Tanga.






Watalii kutoka nchi mbalimbali wakicheza pamoja na washereheshaji wa kampeni ya ‘Nani Mtani Jembe’ inayohusisha mashabiki Simba na Yanga, ili kuzipigia kura timu zao na kushinda kitita kingi kati ya Tsh.100 milioni zilizotelewa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager ambao ndio wadhamini wa timu hizo na timu ya Taifa. Timu hiyo ipo kanda ya Kaskazini na Mashariki inayojumuisha mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Singida na Tanga. Watalii hao walikuwa wakitembelea maeneo mbalimbali mkoani Arusha












www.tabasamuleo.blogspot.com

Monday 11 November 2013

MABONDIA SAID MBWELWA AMSAMBALATISHA SHABANI KAONEKA NA KALAMA NYILAWILA AMKALISHA KAMINJA RAMADHANI RAUNDI YA KWANZA


Bondia Said Uwezo kushoto akipambana na Sindano Paul wakati wa mchezo wao uliofanyika jumapili katika ukumbi wa Zulu paradaise pugu kulumba Dar es salaam uwezo alishinda kwa point mpambano huo

makala,KUMBUKUMBU YA MIAKA 19 YA KIFO NA SHEREHE YA KUZALIWA UPYA KWA METHOD MOGELLA 'FUNDI'......

Leo Tanzania inakumbuka kumbukumbu ya miaka 19 ya kifo cha mmoja wa mashujaa wake katika soka, huyu si mwingine bali ni Method Mogella ‘Fundi’ ambaye alifariki Dunia Novemba 12, 1994.
Lakini pia siku hiyo hiyo ya kifo chake Method Mogella alizaliwa upya....Fuatilia tamthilia hii ya kusisimua
Method anakumbukwa zaidi kwa kuwa mmoja wa wanasoka waliocheza soka la mafanikio kwa ngazi ya klabu kiasi cha kuonekana mfano wa kuigwa akimudu vyema kucheza nafasi ya kiungo mchezeshaji.
Hadi leo Tanzania ingali haijapata kiungo aliyefanana naye japokuwa wapo vijana wengi wanaojaribu kufuata nyayo zake ambao sasa tunadhani wanaweza kufikia makali ya Method.
Katika kikosi cha Yanga kilichoifunga SC Villa ya Uganda mabao 2-1 na kutwaa ubingwa wa Kombe la Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (sasa Kombe la Kagame), Method alikuwepo kikosini na alitoa mchango mkubwa wa ushindi huo.
Mabao ya Yanga yalifungwa na Edibily Lunyamila na Said Mwamba ‘Kizota’, na hayo ni miongoni mwa mafanikio ya Method alipokuwa akiitumikia Yanga.

BABA YAKE ALIMKATAZA KUCHEZA SOKA


Method aliyezaliwa mwaka 1965 mkoani Morogoro, alionyesha ana mapenzi makubwa na mchezo wa soka tangu alipokuwa anasoma katika shule ya msingi ya Msimbazi Boys wilayani Ilala jijini Dar es Salaam wakati familia yake ilipokuwa inakaa Buguruni.