Thursday, 14 November 2013
Kiiza: Mechi 9, mabao 8! Niko juu bwana
Kiiza ambaye ni raia wa Uganda, hakucheza mechi za mwanzoni mwa msimu kwa sababu alikwenda Lebanon kwenye majaribio.
By DORIS MALIYAGA,MWANASPOTI
STRAIKA wa Yanga, Hamis Kiiza, ameridhika na kiwango alichokionyesha mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Bara baada ya kufunga mara nane katika mechi tisa.
Hata hivyo, amekiri kukutana na changamoto nyingi kikosini humo.
Kiiza ambaye ni raia wa Uganda, hakucheza mechi za mwanzoni mwa msimu kwa sababu alikwenda Lebanon kwenye majaribio lakini tangu aliporejea amepata nafasi alizotumia kufunga mabao hayo.
Akizungumza na Mwanaspoti, alisema: “Kama nimecheza mechi tisa na kufunga mabao manane naweza kusema nimefikia malengo ingawa si sana.
“Ni jambo la kumshukuru Mungu kwani nimekutana na changamoto nyingi msimu huu. Hata hivyo siwezi kuzitaja hapa kwa sababu ni mambo ya ndani,” alisema.
Mchezo wake wa mwisho wa mzunguko wa kwanza ulikuwa dhidi ya JKT Oljoro ambapo alitolewa kipindi cha pili na Jerry Tegete aliingia badala yake.
Kitendo hicho hakikumfurahisha mchezaji huyo kwa sababu malengo yake yalikuwa ni kupata fursa zaidi ili aongeze mabao.
Mwanaspoti linajua kwamba mchezaji huyo hafurahishwi na jinsi kocha, Ernest Brandts anavyomtumia kwenye nafasi mbalimbali uwanjani.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment