Pages

ELIMU KWANZA.

ELIMU KWANZA.
FEDHA SIO KIPAUMBELE CHETU.

Saturday, 8 March 2014

RAHISI NGAMIA KUPENYA TUNDU LA SINDANO KULIKO AL AHLY KUITOA YANGA LEO

CHANZO; NA BIN ZUBEIRY
YANGA SC usiku wa leo inashuka kwenye Uwanja wa Border Guard, Alexandria nchini Misri kumenyana na wenyeji, Al Ahly katika mchezo wa marudiano, Raundi ya Kwanza Ligi ya Mabingwa Afrika.
Yanga itamenyana na mabingwa hao wa Afrika, ikiwa kwenye mazingira mazuri ya kusonga mbele, kufuatia ushindi wa bao 1-0 katika mchezo wa kwanza nyumbani Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Suala si ushindi tu, kiwango ambacho walichoonyesha Yanga SC Jumamosi ya wiki iliyopita na aina ya uchezaji wa kushambulia kwa kasi ndiyo vitu vinavyotia matumaini zaidi, hasa baada ya kocha wa timu hiyo, Mholanzi, Hans van der Pluijm kusema watarudia kucheza namna hiyo leo.


Hata kama Yanga SC watacheza mchezo wa kujihami zaidi, bado watakuwa tishio kwa Ahly kwa kuhofia wanaweza kufungwa kwa mashambulizi ya kushitukiza.

CHELSEA YAUA 4-0, ETO'O AFUNGA NA KUSHANGILIA KAMA KIBABU CHA KUTEMBELEA MKONGOJO

CHELSEA imetanua mbawa zake kileleni mwa Ligi Kuu ya England, kufuatia ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Tottenham Hotspur Uwanja wa Stamford Bridge usku huu.
Mabao ya The Blues leo yamefungwa na Samuel Eto'o dakika ya 56, Edin Hazard dakika ya 60 na Demba Ba mawili dakika za 88 na 89.
Ushindi huo, unaifanya Chelsea itimize pointi 69 baada ya kucheza mechi 28 na kujiimarisha kileleni, ikiizidi kwa pointi saba Liverpool iliyo nafasi ya pili kwa pointi zake 59 sawa na Asrenal, nao wakiwa wamecheza mechi 28 pia. Manchester City ni ya nne sasa kwa pointi zake 57, lakini ina mechi mbili mkononi.

Mimi kizee; Eto'o akishangilia kama mzee baada ya kufunga kuwabeza wanaomuita mzee kwenye timu hiyo, baada ya kocha Jose Mourinho pia kusema ana umri mkubwa

BARCELONA YAPIGWA NA KITUMU CHA KUSHUKA DARAJA LA LIGA

KLABU ya Barcelona leo imecheza sokambovu mno zikiwa zimebaki siku tatu kabla ya kukutana na Manchester City katika mchezo wa marudiano wa Hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Ulaya na kufungwa na bao 1-0 Real Valladolid iliyo hatarini kushuka.
Bao hilo pekee lililozaimisha Barca iliyoongozwa na nyota wake Lionel Messi leo, lilifungwa na Mtaliano Fausto Rossi dakika ya 17 Uwanja wa Manispaa mjini Valladolid.
Huo ni ushindi wa kwanza wa Valladolid tangu Januari ambao unaiinua hadi nafasi ya 17 kutoka ya 18 kwa kutimiza pointi 26 baada ya kucheza mechi 27, wakati Barcelona inabaki nafasi ya pili kwa pointi zake 63 baada ya kucheza mechi 27,moja zaidi dhidi ya vinara, Real Madrid wenye pointi 64.

Siku mbaya ofisini: Nyota wa Barcelona, Lionel Messi akiwa haamini macho yake baada ya kipigo cha Valladolid

KWANINI KIWANGO CHA OSCAR KIMESHUKA KATIKA SIKU ZA HIVI KARIBUNI?

Oscar alianza msimu huu akiwa kwenye form nzuri, kiungo mchezeshaji huyo wa kibrazil alifunga mabao 5 katika mechi zake 12 za kwanza premier league na akawa chaguo la kwanza la Jose Mourinho. Mourinho alijenga kikosi chake kumzunguka Oscar, huku Oscar akicheza kama namba 10 anayekaba kuanzia juu, akitafuta kufunga au kutoa assists. Lakini katika miezi ya karibuni kiwango cha Oscar kinaonekana kupungua.
Kushuka kiwango
Pamoja na kufunga mabao 5 katika michezo 12 ya kwanza ya msimu wa EPL, Oscar ameweza kufunga bao 1 tu katika michezo 14 iliyofuatia na huku kiwango chake katika eneo la kushambulia kikiwa chini. Takwimu zinaonyesha kupiga mipira iliyolenga goli kumeshuka kwa 44%. Mchoro wa hapo unaonyesha takwimu za mchezo wake jinsi zilivyoshuka.

ZAMALEK YAPENYA TUNDU LA SINDANO, WAGANDA WAFANYA MADUDU KAMPALA BAADA YA KUANZA VIZURI MECHI YA KWANZA

Na Prince Akbar, Dar es Salaam
ZAMALEK ya Misri imepenya kwenye tundu la sindano kuelekea Hatua ya 16 ya Ligi ya Mabingwa Afrika kufuatia kulazimisha sare ya bila kufungana Angola usiku wa jana mbele ya wenyeji Kabuscorp katika mchezo wa marudiano wa Raundi ya Kwanza.
Zamalek inayofundishwa na mshambuliaji wa zamani wa kimataifa wa Misri na Tottenham Hotspur ya England na klabu hiyo ya Cairo, Ahmed Hassan ‘Mido’ ilipata ushindi mwembamba wa bao 1-0 katika mchezo wa kwanza nyumbani na kutengeneza hofu ya kutolewa.

Wazembe hawa; KCC ilianza kwa sare ya 2-2 ugenini, lakini imefungwa 2-1 nyumbani leo

Tuesday, 4 March 2014

NTEZE JOHN LUNGU AOKOKA, AWA MCHUNGAJI MAREKANI

Na Dina Ismail, Dar es Salaam
MSHAMBULIAJI wa zamani wa kimataifa wa Tanzania, Nteze John Lungu sasa amekuwa Mchungaji wa kanisa moja la kilokole nchini Marekani, imeelezwa.
Rafiki mmoja wa karibu Nteze, ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba, Nteze aliyewika Pamba FC ya Mwanza na Simba SC ya Dar es Salaam, kwa sasa amekuwa mtumishi wa Mungu baada ya kustaafu soka.

Mtumishi wa Bwana; Mchungaji Nteze John Lungu (watatu toka kushoyo) aliyekuwa mchezaji wa timu ya Pamba ya Mwanza na Simba Sports Club ya Dar es Salaam pamoja na Watanzania wa Seattle, ndugu, jamaa na marafiki kwa pamoja wakiwa kwenye makaburi ya Holy Rood kwenye safari ya mwisho ya mpendwa wao Flora Ndimbo Glimsdale aliyefariki tarehe 12/30/2013, huko Seattle Washington State na kuzikwa Jumatatu Jan 6, 2014/

MARTESACKER NA ROSICKY WAONGEZA MIKATABA ARSENAL

NYOTA wawili wa Arsenal, Per Mertesacker na Tomas Rosicky wamekubali kusaini mikataba mipya ya kuendelea kupiga kazi Uwanja wa Emirates.
BIN ZUBEIRY inafahamu The Gunners imekuwa ikiwatongoza wachezaji hao kuongeza mikataba tangu Septemba mwaka jana - na sasa klabu hiyo ya Ligi Kuu ya England imethibitisha wachezaji hao wanabaki.
Mertesacker ametweet picha akiwa kijana mdogo amevaa jezi ya Arsenal na kuandika maelezo: "Tangu nikiwa mdogo hadi sasa, najivunia kuwa gunner! Asante mashabiki kwaa sapoti yenu. Furaha kuongeza muda na @Arsenal.

Bado yupo sana; Beki Mjerumani Per Martersacker ameongeza Mkataba Arsenal hadi mwaka 2017

TFF KUWACHUKULIA HATUA ZAIDI WAWILI TWIGA STARS

Na Boniface Wambura, Dar es Salaam
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) linatafakari hatua zaidi za kinidhamu dhidi ya wachezaji wawili wa kikosi cha Twiga Stars walioondolewa kwenye timu hiyo na Kocha Rogasian Kaijage.
Kocha Kaijage aliwatimua kambini wachezaji Mwapewa Mtumwa na Flora Kayanda kutokana na vitendo vya utovu wa nidhamu wakati Twiga Stars ikijiandaa kwa mechi ya marudiano ya michuano ya Afrika kwa Wanawake (AWC) dhidi ya Zambia.


Twiga Stars ilipoteza mechi ya kwanza ugenini mabao 2-1 na kutoka sare ya bao 1-1 katika mechi ya marudiano iliyochezwa Februari 28 mwaka huu Uwanja wa Azam Complex, hivyo kutolewa katika mashindano hayo kwa jumla ya mabao 3-2.

Monday, 3 March 2014

YANGA SC NA AHLY MAPATO YA MLANGONI MILIONI 488

Boniface Wambura, Dar es Salaam
MECHI ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Yanga na Al Ahly kutoka Misri iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki imeingiza sh. 448,414,000.
Mapato hayo yametokana na watazamaji 50,202 waliokata tiketi kushuhudia pambano hilo kwa viingilio vya sh. 7,000, sh. 13,000, sh. 25,000 na sh. 35,000. Yanga ilishinda mechi hiyo kwa bao 1-0.

UNAMKUMBUKA YULE BONDIA FRANK BRUNO...SASA NI MTENGENEZA NYWELE WANAWAKE SALUNI

MBABE wa zamani ulingoni, Frank Bruno amesema amerudi mazoezini tena, lakini safari hii akijifua kuwa mtengeneza nywele za wanawake saluni.

Bingwa huyo wa zamani wa dunia wa nsonsi za kulipwa mwenye umri wa miaka 52 sasa alikumbana na suluba nyingi enzi zake ulingoni.

Lakini baada ya msoto wa kutafuta msimamo mpya wa maisha tangu astaafu mwaka 1996, inatokea anataka kuhamishia umahiri wake wa ulingoni kwenye nywele za mabinti.

Wapendanao: Frank Bruno akiwa na mpenzi wake,Nina Coletta ambaye anamsaidia kujifunza kazi za kutengeneza nywele za wanawake

OKWI NA KIIZA TAYARI WAPO ZAMBIA NA THE CRANES, WATAONDOKEA HUKO KWENDA CAIRO

Na Mahmoud Zubeiry, Dar es Salaam
WASHAMBULIAJI Waganda wa klabu ya Yanga SC, Emmanuel Okwi na Hamisi Kiiza wamewasili jioni hii mjini Ndola, Zambia kujiunga na timu yao ya taifa, Uganda, The Cranes kwa ajili ya mchezo wa kirafiki wa kimataifa Jumatano dhidi ya wenyeji Chipolopolo.
Okwi na Kiiza ambao waliichezea Yanga SC Jumamosi ikiifunga Al Ahly ya Misri bao 1-0 katika mchezo wa kwanza kuwania kutinga Hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Afrika Uwanja wa Taifa, Dar ves Salaam waliondoka leo nchini.

Watu wa kazi; Okwi kulia akiwa na Kiiza, tayari wapo Zambia kuitumikia timu yao ya taifa ya Uganda

AZAM KUMSAJILI MFUNGAJI BORA KOMBE LA MAPINDUZI, KOCHA OMOG ATOA BARAKA ZOTE

Na Mahmoud Zubeiry, Dar es Salaam
MFUNGAJI bora wa michuano ya Kombe la Mapinduzi mwaka huu, Mganda Owen Kasule amefuzu majaribio katika klabu ya Azam FC na sasa atasajiliwa kwa ajili ya msimu ujao.
Kocha Mcameroon Joseph Marius Omog ameridhishwa na uwezo wa kiungo huyo mshambuliaji wa URA ya Uganda baada ya majaribio ya wiki mbili na ameuambia uongozi umsajili.

Kifaa kipya Chamazi; Kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda, Owen Kasule atasajiliwa Azam FC baada ya kufuzu majaribio

Sunday, 2 March 2014

Lupita Nyon'go ashinda tuzo ya Oscar

Lupita Nyong'o,ameshinda tuzo ya muigizaji bora msaidizi katika filam aliyoshiriki "12 Years a Slave", akizungumza katika tuzo za 86 za Oscar huko Hollywood, California March 2, 2014. REUTERS/Lucy Nicholson (UNITED STATES TAGS: ENTERTAINMENT) (OSCARS-SHOW) - RTR3FY5W
Mcheza sinema maarufu Lupita Nyong’o ambaye ni raia wa Kenya, Jumapili ameshinda tuzo la kifahari la Oscar huko Hollywood California.

Lupita alipata tuzo hilo kwa kuwa muigizaji msaidizi bora zaidi kwenye filamu iitwayo“12 years A Slave”.
Baada ya kupokea tuzo hilo, Lupita alitoa hotuba yenye hisia kali na kuwashukuru wote waliomwezesha kushinda tuzo hilo la Oscar.

Awali macho ya dunia kwa wapenzi wa filam yalielekezwa huko Hollywood kutizama tuzo za mwaka wa 86 za Oscar zikitunukiwa wasanii mbali mbali wa filam duniani.

Kwa upande wa Afrika mcheza filamu mwingine wa mara ya kwanza Barkhad Abdi ambaye ni raia wa Somalia aliteuliwa kuwania katika nafasi ya waigizaji wasaidizi ambapo alishiriki katika filamu “Captain Phillips” ambapo muigizaji Jared Leto alipata ushindi.

Vyombo vya habari vya Kenya viliripoti kuwa wakenya na waafrika kwa jumla walikuwa wakisubiri kuona ikiwa muigizaji Lupita Nyong’o atapata tuzo hilo. Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta pia alikuwa ametuma salamu za kumtakia ushindi Lupita ,katika ujumbe kwenye ukurasa wake wa Facebook.