Pages

ELIMU KWANZA.

ELIMU KWANZA.
FEDHA SIO KIPAUMBELE CHETU.

Saturday, 22 March 2014

SOMO : MAONO NA NDOTO * sehemu ya saba na nane*

Mtumishi Gasper Madumla.

Haleluya....
Nakusalimu nikikuambia;
Bwana Yesu asifiwe sana...

Leo tunaingia katika kipengele kipya kabisa kuhusu NDOTO.Maana katika siku sita zote tulikuwa tukijifunza kuhusu maono.

Wengi wametafsiri neno NDOTO kwa tafsiri tofauti tofauti,ingawa tafsiri nyingine si tafsiri sahihi. Leo tanajifunza tafsiri sahihi iliyo rahisi kabisa ya neno NDOTO.

Ndoto ni nini?
*Ndoto ni mtiririko wa picha zitembeazo katika akili ya mtu,pindi mtu huyo anapokuwa amelala.

Ndoto huja pale mtu anapokuwa amelala,na ndio maana huwezi kumkuta mtu ambaye ajalala,mtu atembeaye kisha akuambie ya kwamba alikuwa anaota ndoto wakati anatembea.

Hakika ukikutana na mtu kama huyo ni lazima utamshangaa !..
Na swali la kwanza utakalo muuliza mtu huyo ni hili;
"Je wakati unatembea ulikuwa umelala,hata uote?"

YAYA TOURE APIGA HAT TRICK MAN CITY IKIUA 5-0 ENGLAND

MANCHESTER City imerudi kwa hasira katika Ligi Kuu ya England ikitoka kutolewa Ligi ya Mabingwa Ulaya- baada ya jioni hii kuifumua mabao 5-0 Fulham katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Etihad mjini Manchester.
Mwanasoka Bora wa Afrika, Yaya Toure leo amepiga hat trick yake ya kwanza, mabao mawili akifunga kwa penalti dakika ya 26 na 54 na linguine dakika ya 65 akimalizia pasi ya Samir Nasri.
Mabao mengine ya Man City yamefungwa na Fernandinho dakika ya 84, akimalizia pasi ya Milner na Demichelis dakika ya 88. Ushindi huo, unaifanya City ifikishe pointi 63 baada ya kucheza mechi 28 na kupanda nafasi ya tatu mbele ya Arsenal yenye pointi 62 za mechi 30.
Chelsea inaongoza Ligi Kuu England kwa pointi zake 69 za mechi 31, ikifuatiwa na Liverpool yenye pointi 65 baada ya mechi 30, wakati Arsenal yenye pointi 62 ni ya nne.

Mtu wa furaha: Yaya Toure amefunga hat-trick jana Manchester City ikiilaza Fulham mabao 5-0

ROONEY APIGA BAO LA KIHISTORIA MAN UNITED IKING'ARA ENGLAND

MSHAMBULIAJI Wayne Rooney usiku huu amekumbushia enzi za David Beckham alipoifungia bao la umbali wa mita 58 Manchester United ikiifunga West Ham mabao 2-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Upton Park.
Akirejea katika Ligi Kuu baada ya kufanikiwa kutinga Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa kuitoa Olympiacos ya Ugiriki, mwanasoka huyo wa kimataifa wa England aliifungia mabao mawili timu ya David Moyes dakika ya nane na 73 na kuiwezesha kubeba pointi tatu.
Bao la pili la Rooney limemfanya atimize mabao 212 na kumfikia Jack Rowley katika nafasi ya tatu ya ufungaji bora wa kihistoria Man United, lakini ni bao lake la kwanza alilofunga dakika ya nane ambalo litabakia katika kumbukumbu.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 alifunga bao la ajabu, akikumbushia bao alilofunga Beckham dhidi ya Wimbledon mwaka 1996. United sasa inatimiza pointi 51 baada ya mechi 30, ingawa inabaki nafasi ya saba, ikizidiwa pointi mbili na Tottenham Hotspur iliyo nafasi ya sita.
Bao ambalo halitasahaulika: Rooney amefunga bao kutoka umbali wa mita 57.9 Uwanja wa Upton Park usiku huu
Wayne Rooney baada ya kufutumua shuti la mbali
Pongezi: Wachezaji wa United wakimpongeza Rooney baada ya bao la kwanza

ZAMALEK YALAZIMISHA SARE YA 0-0 NA NKANA ZAMBIA, ESPERANCE YAANZA NA SARE PIA UGENIN

Na Mwandishi Wetu, Kitwe
MATUMAINI ya Nkana FC ya Zambia kucheza hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika yamepungua baada ya jioni ya leo kulazimishwa sare ya bila kufungana nyumbani na Zamalek ya Misri katika mchezo wa kwanza wa 16 Bora mjini Kitwe.
Mabingwa mara tano Afrika, Zamalek wamefurahia matokeo ya sare ya 0-0 kwenye Uwanja wa Nkana, wakiamini watamalizia vizuri mchezo wa marudiano mjini Cairo wiki ijayo na kusonga mbele.

Kocha Ahmed Hassan 'Mido' amefanikiwa mpango wa kulazimisha sare ugenini Jumamosi mbele ya Nkana FC
Hii inakuwa mara ya tatu mfululizo mechi kati ya Nkana na Zamalek kumalizika kwa sare Zambia na mechi zilizopita wababe wa Misri wamekuwa wakienda kushinda nyumbani kwao na kusonga mbele.
Katika mchezo wa leo, Nkana walianza vizuri wakisukuma mashambulizi mfululizo langoni mwa wapinzani wao, Zamalek.
Nkana ilipata nafasi ya kwanza nzuri dakika ya tatu tu kupitia kwa mshambuliaji Simon Bwalya, ambaye alipiga kichwa na mpira kupaa juu ya lango kufuatia krosi ya winga Bruce Musakanya akiwa ndani ya eneo la hatari.
Mshambuliaji Ronald Kampamba, pia alipata nafasi nzuri dakika ya 10 akashindwa kuitumia alipopiga mpira wa adhabu uliopaa juu ya lango.
Kocha wa Zamalek, Ahmed Hassan ‘Mido’ alikuwa nyota hivi leo uwanjani kutokana na namna alivyoiongoza vyema timu yake akiwa benchi na kulazimisha sare ya ugenini.
Mido alilundika wachezaji saba nyuma ya mpira kwa muda mrefu wa mchezo na kuvuruga mipango ya Kampamba na Bwalya katika safu ya ushambuliaji ya Nkana.
Mshindi wa jumla baada ya mechi ya marudiano atasonga mbele hatua ya makundi, wakati atakayetolewa ataangukia kwenye mechi za kuwania kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho mwezi ujao.
Katika mchezo mwingine leo, AS Real ililazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 nyumbani mjini Bamako, Mali na Esperance ya Tunisia.
Michuano hiyo itaendelea kesho kwa mechi kati ya TP Mazembe ya DRC na Sewe Sport mjini Abidjan, Horoya ya Guinea itaanzia nyumbani na CS Sfaxien ya Tunisia, sawa na ES Setif ya Algeria itakayoikaribisha Coton Sport ya Cameroon, AC Leopards ya Kongo itakayoikaribisha Al-Hilal ya Sudan na AS Vita ya DRC itaanzia nyumbani na Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini Uwanja wa Tata Raphael mjini Kinshasa, wakati mechi zote za marudiano zitachezwa Jumamosi ya Machi 29, mwaka huu.

EL CLASICO UHONDO WAONGEZEKA, BENZEMA NA PIQUE WAREJEA KUZIONGEZEA NGUVU REAL MADRID NA BARCA ZIKIMENYANA LEO LA LIGA

TIMU za Barcelona na Real Madrid zote zimeongezewa nguvu kuelekea mchezo wa leo usiku wa El Clasico kufuatia habari kwamba Gerard Pique na Karim Benzema watakuwepo kwenye mechi hiyo itakayopigwa Uwanja wa Santiago Bernabeu, Madrid.
Beki Pique hakuwepo wakati Barca inashinda 7-0 dhidi ya Osasuna kutokana na maumivu ya kifundo cha mguu wa kulia, lakini alirejea mazoezini Jumatatu wiki hii.
Pamoja na hayo, Carles Puyol, ambaye ataondoka Nou Camp mwishoni mwa msimu, atakosa mchezo ambao ungekuwa wa mwisho kwake dhidi ya Real kutokana na maumivu ya goti.

Atakosekana: Carles Puyol anatarajiwa kuikosa 'El Clasico' yake ya mwisho akiwa na jezi ya Barcelona kutokana na maumivu ya goti


+15
Neymar na Jordi Alba wakiwa mazoezini na wenzao wa Barcelona jana tayari kwa mchezo wa leo


Kiungo Alex Song akitaniana na Neymar kwa kumsukuma uwanjani huku Alba akitazama

Wote wanatabasamu: Gerard Pique alihudhuria uzinduzi wa albamu ya mpenzi wake, Shakira mjini Barcelona Ijumaa
Wakati huo huo, mwanasoka wa kimataifa wa Ufaransa, Karim Benzema anatarajiwa kurejea kwenye kikosi cha Los Blancos baada ya kukosa mechi timu yake ikishinda mabao 3-1 dhidi ya Schalke katika Ligi ya Mabingwa Jumanne.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa Lyon alirejea kwenye kikosi cha kocha Carlo Ancelotti jana baada ya kuumia siku Madrid ikiilaza 1-0 Malaga ugenini.
Vinara wa La Liga, Real wanaingia kwenye mchezo wa leo wakiwa wanawazidi kwa pointi nne wapinzani wao hao, Barcelona walio katika nafasi ya tatu nyuma ya Atletico wanaowazidi pia pointi tatu.

Wakali wawili: Cristiano Ronaldo akifanya mazoezi na Gareth Bale jana tayari kwa mchezo wa leo

Wachezaji wa Real Madrid mazoezini jana

Nyota kweli: Lionel Messi akishuka Uwanja wa mazoezi wa Barcelona, Sports Centre jana kwenda kujifua kwa ajili ya mechi ya leo

Wataalamu: Kocha wa Barcelona, Martino (kushoto) na wa Madrid, Ancelotti nani ataipa ushindi timu yake leo?

Tuesday, 18 March 2014

WOLPER: LAZIMA NIOLEWE NJE YA NCHI


STAA wa filamu za Kibongo, Jacqueline Wolper ameibuka na kudai kuwa, atafanya kila njia ili aolewe na mwanaume wa nje ya nchi na siyo Wabongo ambao hawathamini mastaa.
Akizungumza na Uwazi, Wolper alisema, amefikia uamuzi huo kwa sababu ana uchungu moyoni unaotokana na dhana waliyonayo wanaume wa Kitanzania juu yao, wakiamini kuwa ni wahuni tu hivyo kuwashusha thamani.“Unajua Mtanzania anamchukulia staa kama chombo cha starehe tu na hawezi kumuoa kamwe na hata akimuoa basi hatamthamini kama wanavyothaminiwa wasanii wa huko nje.

KLABU ya Real Madrid imeungana na wapinzani wao nchini Hispania, Barcelona kutinga Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kufuatia ushindi wa mabao 3-1 usiku huu Uwanja wa Santiago Bernabeu mjini Madrid ambao unawafanya wasonge mbele kwa ushindi wa jumla wa mabao 9-2 dhidi ya Schalke ya Ujerumani.

Mabao yaliyoipeleka Madrid Nane Bora ya Ligi ya Mabingwa yamefungwa na Cristiano Ronaldo mawili dakika za 21 na 74 akifikisha mabao 41 msimu huu, na lingine limefungwa na Alvaro Morata dakika ya 75.
Madrid ilishinda 6-1 katika mchezo wa kwanza ugenini, hivyo imesonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 9-2.

Mkali kweli: Ronaldo akishangilia baada ya kuifungia Real Madrid ikiilaza 3-1 Schalke
Mchezaji ghali duniani, Gareth Bale akimkumbatia Ronaldo baada ya kuitumia pasi yake vyema kufunga

ETO'O AIPELEKA CHELSEA ROBO FAINALI LIGI YA MABINGWA ULAYA, DROGBA APATA MAPOKEZI MAZURI DARAJANI

CHELSEA itaendelea kupeperusha bendera ya England kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya usiku huu kuitoa Galatasaray ya Uturuki kwa jumla ya mabao 3-1 Uwanja wa Stamford Bridge, London.
Baada ya kutolewa kwa Manchester City na Arsenal katikati ya wiki iliyopita, Chelsea imejikatia tiketi ya kuingia Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa kwa kuifunga mabao 2-0 timu hiyo ya mchezaji wao wa zamani nyota, Didier Drogba.
Mabao ya Chelsea yamefungwa Samuel Eto'o 'Kikongwe' dakika ya nne na Gary Cahil dakika ya 43. Katika mchezo mwingine usiku huu, Real Madrid imeifunga Schalke mabao 3-1 Uwanja wa Santiago Bernabeu na kuwatoa Wajerumani hao kwa jumla ya mabao 9-2 baada ya awali kushinda 6-1 ugenini. Leo mabao ya Real yalifungwa na Cristiano Ronaldo dakika ya 21 na 74 na lingine Alvaro Morata dakika ya 75, wakati la Schalke limefungwa na Tim Hoogland dakika ya 31.

Kikongwe machachari: Samuel Eto'o akishangilia baada ya kuifungia Chelsea bao la kwanza dakika ya nne Uwanja wa Stamford Bridge

Sunday, 16 March 2014

PIRLO AIPAISHA ZAIDI YA KILELENI JUVE SERIE A

MKONGWE Andrea Pirlo ameiwezesha Juventus kupaa kwa pointi 17 zaidi kileleni mwa Serie A kufuatia bao lake pekee la ushindi dakika ya 89 kwa mpira wa adhabu wakiilaza Genoa 1-0.
Mabingwa hao watetezi walikutana na mchezo mgumu Uwanja wa Luigi Ferraris mbele ya Genoa, lakini walipambana hadi mwishoni mwa mechi hiyo Pirlo alipofunga bao linalozidi kuwakatisha tamaa, Roma walio katika nafasi ya pili ambao wanacheza leo.
Mechi nyingine za jana usiku, Fiorentina iliilaza mabao 3-1 Chievo Uwanja wa Artemio Franchi na AC Milan ikalala 4-2 nyumbani mbele ya Parma.

Shujaa: Wachezaji wa Juventus wakimpongeza Pirlo baada ya kufunga bao la ushindi dhidi ya Genoa katika mchezo wa Serie A jana

IBRAHIMOVIC AIPELEKA KULEEEE PSG...KARIBU KABISA NA UBINGWA

MSHAMBULIAJI Zlatan Ibrahimovic jana alifunga mabao mawili kwa mara ya tano katika mechi moja msimu huu wa Ligue 1 akiiwezesha Paris St Germain kuifunga St Etienne 2-0 na kuendelea kuongoza kwa pointi nane zaidi ligi hiyo.
Mabao hayo mawili ya kipindi cha kwanza ya mfungaji huyo bora wa mabingwa hao wa Ufaransa, yametosha kuipa timu ya Laurent Blanc ushindi wa saba mfululizo kwenye mashindano yote na kuzidi kuwaacha Monaco walio nafasi ya pili.
Monaco ilipunguza pengo la pointi kidogo baada ya ushindi wa mabao 3-2 juzi dhidi ya Lyon, huo ukiwa ushindi wao wa tano katika mechi sita zilizopita.

Mawili ya maana: Zlatan Ibrahimovic ameibeba Paris Saint-Germain kwa ushindi wa 2-0 dhidi ya St Etienne kwenye Ligue 1

LIVERPOOL YAICHARAZA MACHESTER UNITED



Steven Gerard alifunga mikwaju miwili ya penalty na kukosa ya tatu Liverpool ikiendelea kuimarisha matokeo yake baada ya kuwacharaza mabingwa watetezi wa ligi ya uingereza Machester United tatu bila katika uga wao wa nyumbani Old Trafford.

ARSENAL YAIPIGA SPURS 1-0



ARSENAL imepata ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Tottenham Hotspur Uwanja wa White Hart Lane mjini London jioni hii katika mchezo wa Ligi Kuu ya England.