Pages

ELIMU KWANZA.

ELIMU KWANZA.
FEDHA SIO KIPAUMBELE CHETU.

Sunday 16 March 2014

IBRAHIMOVIC AIPELEKA KULEEEE PSG...KARIBU KABISA NA UBINGWA

MSHAMBULIAJI Zlatan Ibrahimovic jana alifunga mabao mawili kwa mara ya tano katika mechi moja msimu huu wa Ligue 1 akiiwezesha Paris St Germain kuifunga St Etienne 2-0 na kuendelea kuongoza kwa pointi nane zaidi ligi hiyo.
Mabao hayo mawili ya kipindi cha kwanza ya mfungaji huyo bora wa mabingwa hao wa Ufaransa, yametosha kuipa timu ya Laurent Blanc ushindi wa saba mfululizo kwenye mashindano yote na kuzidi kuwaacha Monaco walio nafasi ya pili.
Monaco ilipunguza pengo la pointi kidogo baada ya ushindi wa mabao 3-2 juzi dhidi ya Lyon, huo ukiwa ushindi wao wa tano katika mechi sita zilizopita.

Mawili ya maana: Zlatan Ibrahimovic ameibeba Paris Saint-Germain kwa ushindi wa 2-0 dhidi ya St Etienne kwenye Ligue 1
+8
Ibrahimovic amefunga mabao mawili jana kuiwezesha PSG kuendelea kuongoza ligi ya Ufaransa kwa pointi nane zaidi

No comments:

Post a Comment