TIMU za Barcelona na Real Madrid zote zimeongezewa nguvu kuelekea mchezo wa leo usiku wa El Clasico kufuatia habari kwamba Gerard Pique na Karim Benzema watakuwepo kwenye mechi hiyo itakayopigwa Uwanja wa Santiago Bernabeu, Madrid.
Beki Pique hakuwepo wakati Barca inashinda 7-0 dhidi ya Osasuna kutokana na maumivu ya kifundo cha mguu wa kulia, lakini alirejea mazoezini Jumatatu wiki hii.
Pamoja na hayo, Carles Puyol, ambaye ataondoka Nou Camp mwishoni mwa msimu, atakosa mchezo ambao ungekuwa wa mwisho kwake dhidi ya Real kutokana na maumivu ya goti.
Atakosekana: Carles Puyol anatarajiwa kuikosa 'El Clasico' yake ya mwisho akiwa na jezi ya Barcelona kutokana na maumivu ya goti
+15
Neymar na Jordi Alba wakiwa mazoezini na wenzao wa Barcelona jana tayari kwa mchezo wa leo
Kiungo Alex Song akitaniana na Neymar kwa kumsukuma uwanjani huku Alba akitazama
Wote wanatabasamu: Gerard Pique alihudhuria uzinduzi wa albamu ya mpenzi wake, Shakira mjini Barcelona Ijumaa
Wakati huo huo, mwanasoka wa kimataifa wa Ufaransa, Karim Benzema anatarajiwa kurejea kwenye kikosi cha Los Blancos baada ya kukosa mechi timu yake ikishinda mabao 3-1 dhidi ya Schalke katika Ligi ya Mabingwa Jumanne.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa Lyon alirejea kwenye kikosi cha kocha Carlo Ancelotti jana baada ya kuumia siku Madrid ikiilaza 1-0 Malaga ugenini.
Vinara wa La Liga, Real wanaingia kwenye mchezo wa leo wakiwa wanawazidi kwa pointi nne wapinzani wao hao, Barcelona walio katika nafasi ya tatu nyuma ya Atletico wanaowazidi pia pointi tatu.
Wakali wawili: Cristiano Ronaldo akifanya mazoezi na Gareth Bale jana tayari kwa mchezo wa leo
Wachezaji wa Real Madrid mazoezini jana
Nyota kweli: Lionel Messi akishuka Uwanja wa mazoezi wa Barcelona, Sports Centre jana kwenda kujifua kwa ajili ya mechi ya leo
Wataalamu: Kocha wa Barcelona, Martino (kushoto) na wa Madrid, Ancelotti nani ataipa ushindi timu yake leo?
No comments:
Post a Comment