
Mpira nyavuni; Bao la kwanza la Azam leo Chamazi
Na Mahmoud Zubeiry, Dar es Salaam
YANGA SC imepanda kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kufuatia ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya JKT Oljoro ya Arusha, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam huku Azam FC ikitoka sare ya 3-3 na Mbeya City, Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, mabao ya Yanga yalifungwa na Simon Msuva dakika 23, Mrisho Ngassa dakika ya 23 na Jerry Tegete dakika ya 53.
Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, hadi mapumziko, timu hizo zilikuwa zimekwishafungana bao 1-1, Azam wakitangulia kupata bao kupitia kwa Humphrey Mieno dakika ya 13 na Mbeya City wakasawazisha kupitia kwa Mwagane Yeya 'Morgan' dakika ya 30.

Ngassa ameifungia Yanga Taifa leo
Mabao yote yalitokana na mipira ya pembeni, Mieno akifunga kwa kuunganisha kwa kichwa mpira wa adhabu uliopigwa na Farid Mussa nje kidogo ya 18, kufuatia kipa David Burhan kudakia nje ya eneo lake na Mwagane aiunganisha krosi ya Deus Kaseke.