Pages

ELIMU KWANZA.

ELIMU KWANZA.
FEDHA SIO KIPAUMBELE CHETU.

Thursday 24 April 2014

REAL MADRID NA BAYERN MUNICH KATIKA PICHA JANA BERNABEU


Juu kwa juu: Cristiano Ronaldo (katikati) akiwa ameruka juu zaidi ya Alaba (wa pili kushoto) na Dante kuwania mpira wa juu katika Nusu Fainali ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Ulaya jana Uwanja wa Bernabeu mjini Madrid, Hispania. Real ilishinda 1-0.
Franck Ribery wa Bayern Munich (kushoto) akimfukuzia Daniel Carvajal wa Real
Mfungaji wa bao pekee la Real, Karim Benzema akishangilia baada ya kufunga Uwanja wa Santiago Bernabeu
Kula gwala, kamalizie kazi: Ronaldo akimpisha Gareth Bale dakika ya 74
Philipp Lahm na Gareth Bale (kulia wakigombea mpira wa juu
Beki Mbrazil wa Bayern, Dante (kushoto) akipitia mpira miguuni mwa Angel di Maria wa Real
Thomas Muller (katikati) wa Bayern akililia penalti
Beki wa Real Madrid, Sergio Ramos (kushoto) akiosha mbele ya mshambuliaji wa Bayern, Bastian Schweinsteiger
Schweinsteiger akimdhibiti kiungo wa Real Madrid, Xabi Alonso (katikati)
Mabeki wa Real, Pepe (kushoto) na Sergio Ramos (katikati) wakienda hewani kuondosha hatarini mpira wa juu kutoka kwa Ribery



Kipa wa Real, Iker Casillas (kulia) akiokoa mpira kichwani kwa Javier Martinez
Cristiano Ronaldo akimtoka Jerome Boateng

TARIMBA: NINA DHAMIRA YA KURUDI KUONGOZA YANGA SC

Na Amran Muhina, Dar es Salaam
RAIS wa zamani wa klabu ya Yanga SC ya Dar es Salaam, Tarimba Abbas amesema kwamba ana dhamira ya kurudi kuiongoza klabu hiyo, katika uchaguzi ujao uliopangwa kufanyika Juni 15, mwaka huu.
Tarimba ameiambia BIN ZUBEIRY jana kwamba, kwa sasa bado mapema mno kuzungumzia jambo hilo ingawa kama mwana-Yanga ana haki yake kikatiba.
“Ni mapema mno kusema nitagombea, maana uchaguzi ni mpaka Juni ni kipindi kirefu sana, lakini kama mwana-Yanga dhamira ninayo ingawa inaweza isiwe sasa, ila ninachoweza kusema ni mapema mno kuzungumzia jambo hilo,” alisema Tarimba.


Tarimba kulia akizungumzia pembeni ya Mkurugenzi wa Masoko wa Vodacom, Kevin Twissa

Tarimba ambaye kwa sasa ni kada wa CCM, Diwani wa Kata ya na Mkurugenzi wa Tume ya Michezo ya Kubahatisha ni kati ya watu ambao wana Yanga SC wanawataka sana waingie kuongoza klabu hiyo pamoja na Davis Mosha.
Angu Shadrack na wanachama wenzake vijana wa Kariakoo wanajipanga kumfuata Davis Mosha kumshawishi achukue fomu za kugombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti, wakati Tarimba Abbas wanataka awania Uenyekiti wa klabu hiyo.
“Tunajipanga kuwafuata Mosha na Tarimba kuwaomba wagombee, hawa viongozi wetu wa sasa wametuangusha sana, tunataka watu ambao hatutawajaribu, tunajua ni watu wa kazi na wana mapenzi na Yanga,”alisema Angu.
Gazeti la Spoti Leo la leo nalo limewanukuu wanachama wa Yanga wakisema wanaamini Tarimba anastahili kuvaa viatu vya Manji kutokana na uwezo mkubwa aliouonyesha wakati akiwa Rais wa Yanga mwanzoni mwa miaka ya 2000.
“Tumeshakaa mara kadhaa wana-Yanga kujadili nani anafaa kuongoza baada ya Manji kumaliza muda wake, lakini wengi mawazo yetu yameangukia kwa Tarimba. Tunaamini ni kiongozi mzuri na anaweza kuipeleka Yanga pazuri,” alisema Juma Mohammed ‘Kamanda’ aliyejitambulisha anatoka Yanga Bomba.
Naye mwanachama mwingine wa Yanga, Suleiman Mussa, alisema wameanza mikakati ya kuangalia nani atafaa kuiongoza Yanga na wanajipanga kwenda kumuona Tarimba ili kumshawishi wakati ukifika ajitose kwenye uchaguzi huo.

Wednesday 23 April 2014

DIEGO COSTA AWAPA ISHARA NZURI CHELSEA...NI DALILI ZA KUHAMIA DARAJANI

MSHAMBULIAJI wa Atletico Madrid, Diego Costa anaweza kuwa katika jaribio la kuing'oa Chelsea katika Ligi ya Mabingwa Ulaya, lakini alikuwa mwenye furaha kupita kiasi wakati anawapungia mkono mashabiki wa timu hiyo baada ya mechi ya jana.
Inafahamika mshambuliaji huyo ni chaguo la kwanza la kocha Jose Mourinho katika orodha ya wachezaji anaotaka kuwasajili msimu ujao na kitendo cha kuwapungia kwa furaha mashabiki wa Chelsea jana kimezidi kuongeza dalili za kuhamia kwake London.
Chelsea ilitoka sare ya bila kufungana na Atletico Madrid Uwanja wa Vicente Calderon, inamaanisha mchezo bado upo kati kwa kati kuelekea mechi ya marudiano Jumatano ijayo.

Anawapa dalili? Diego Costa akiwapungia mkono mashabiki wa Chelsea baada ya mechi usiku wa jana

Upinzani: Mshambuliaji huyo anaweza kuja kuwa mchezaji mwenzake John Terry msimu ujao, japokuwa jana walizinguana sana uwanjani
Baada ya filimbi ya mwisho mashabiki wa Chelsea walibaki uwanjani wakati baadhi ya wachezaji wanapita mbele yao kuondoka.

REAL HATARINI KUWAKOSA GARETH BALE NA RONALDO LEO DHIDI YA BAYERN, WOTE WAGONJWA

WINGA Gareth Bale yuko shakani kuichezaea Real Madrid katika Nusu Fainali ya Kwanza ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya mabingwa wa Ujerumani, Bayern Munich kutokana na kusumbuliwa nugonjwa wa mafua.
Nyota huyo wa Wales hajasafiri na wenzake kwa ajili ya mchezo wa kwanza leo Uwanja wa Sangtiago Bernabeu.
Kocha wa Real Madrid, Carlo Ancelotti pia anatilia shaka uzima wa Cristano Ronaldo. Nyota huyo wa Ureno anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya muda mfupi kabla ya mchezo wa leo.

Shaka tupu: Gareth Bale anasumbuliwa na mafua kuelekea mchezo wa leo dhidi ya Bayern Munich

Pigo: Madrid inaweza kumkosa Bale na Cristiano Ronaldo leo
Ikiwa Bale ataukosa mchezo wa leo, litakuwa pigo kwa Ancelotti, ambaye alimwagia sifa nyingi winga huyo katika Mkutano na Waandishi wa Habari kuelekea mchezo wa leo.
Bale anang'ara kwa sasa, baada ya kufunga bao la ushindi katika fainali ya Copa del Rey dhidi ya Barcelona wiki iliyopita na kocha wake akasema mchezaji huyo aliyesajiliwa kwa Pauni Milioni 86 kutoka Tottenham atakuwsa mkali zaidi msimu ujao Hispania ambao utakuwa wa pili kwake Real.
"Gareth ni mtoto mkali,"alisema Ancelotti. "Anavutia kwa kujiamini kiasi cha kutosha hususan kutokana na bao alilofunga dhidi ya Barcelona katika fainali,"alisema.