Pages

ELIMU KWANZA.

ELIMU KWANZA.
FEDHA SIO KIPAUMBELE CHETU.

Saturday 18 January 2014

LIGI KUU UINGEREZA, MATOKEO YA MECHI ZA JANA.





Chanzo, Live Scores,

ARSENAL YAJIWEKA SAWA KILELENI EPL



Santi Cazorla akishangilia baada ya kuifungia Arsenal. Anayemfuata nyuma ni Olivier Giroud.

ARSENAL imekaa mguu sawa kileleni mwa Ligi Kuu ya England kufuatia ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Fulham jioni hii Uwanja wa Emirates.

NYOTA WATATU COASTAL UNION WAPATA ULAJI OMAN, NI NYOSSO, SANTO NA DANNY LYANGA

Na Mahmoud Zubeiry, Muscat
WACHEZAJI watatu wa timu ya soka ya Coastal Union ya Tanga, beki Juma Nyosso, kiungo Jerry Santo na mshambuliaji Danny Lyanga wanatakiwa na klabu ya Al Musannaa ya Ligi Kuu ya Oman, imefahamika.
Habari ambazo BIN ZUBEIRY imezipata mjini hapa zimesema kwamba klabu hiyo imekwishakutana na


Jerry Santo kulia akiwa na Salum Esry jana kabla ya chakula cha usiku

YANGA KUIVAA KS FLAMURTARI


Young Africans kesho itashuka dimbani kucheza na timu ya KS Flamurtari Vlore inayoshika nafasi ya tano kwenye msimamo wa Ligi Kuu nchini Albania ikiwa ni sehemu ya mchezo wa kirafiki wa kujipima nguvu kwa timu zote, mchezo utakaofanyika katika eneo la Side Manavagat.

RONALDO KUWANUNULIA GARI JIPYAAAA MADAKTARI REAL MADRID...NI FURAHA YA BALLON D'OR

NI kazi ngumu kuwa mchua misuli wa Cristiano Ronaldo, lakini wakati mwingine inalipa.
Mchezaji huyo ambaye hivi karibuni ameshinda tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia, FIFA Ballon d’Or amewaahidi madaktari wa Madrid kuwanunulia gari mpya baada ya kushinda tuzo hiyo wiki hii.
Katika mahojiano ya hivi karibuni na Sportsmail, kocha wa Real Madrid, Paul Clement amezungumzia mambo ambayo Ronaldo atayafanya atakaporejea kutoka kwenye mechi za katikati ya wiki za Ligi ya Mabingwa.

Wote wanatabasamu: Cristiano Ronaldo amewaahidi madaktari wa Real Madrid kuwanunulia gari mpya baada ya kushinda Ballon d'Or

HENRY AITABIRIA UBINGWA ARSENAL.


Mshambuliaji mstaafu mwenye uraia wa kifaransa (Thiery Henry) aliyekuwa akiichezea club ya Arsenal iliopo kaskazini mwa jiji la London amesema kuwa timu hiyo itatwaa ubingwa wa ligi kuu ya uingereza mwaka huu.

Thursday 16 January 2014

RIHANNA AJICHORA TATTOO YA MSALABA MKONONI, ASEMA ANAPENDA MAMBO YA KIROHO


Rihanna akijipiga picha kwa simu yake baada ya tattoo yake kukamilika ©Twitter/Rihanna News
Mwanamuziki Rihanna mzaliwa wa Barbados amejichora (tattoo) ya msalaba mdogo katika mkono wake wa kuume na kusifia mchoro huo ambao kwa mwanamuziki huyo unamuongezea michoro mingine ya kiroho iliyo mwilini mwake tangu aanze kujichora.

MESSI AIPIGIA MABAO YOTE BARCA IKISHINDA 2-0 KOMBE LA MFALME, LAKINI NEYMAR AUMIA NA HUENDA AKAWAKOSA MAN CITY LIGI YA MABINGWA
Home » Unlabelled » MESSI AIPIGIA MABAO YOTE BARCA IKISHINDA 2-0 KOMBE LA MFALME, LAKINI NEYMAR AUMIA NA HUENDA AKAWAKOSA MAN CITY LIGI YA MABINGWA
MSHAMBULIAJI wa Barcelona, Neymar ameumia kifundo cha mguu akiichezea timu yake mechi ya Copa del Rey ikishinda 2-0 jana dhidi ya Getafe katika mechi ya Kombe la Mfalme.
Sasa Mbrazil huyo anaweza kuukosa mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Manchester City mwezi ujao.
Lionel Messi alifunga mabao yote katika mechi hiyo ya marudiano ya 16 Bora na kufanya ushindi wa jumla wa 6-0.
Barça itasafiri hadi Etihad Februari 18 katika mchezo wa kwanza wa hatua ya mtoano Ligi ya Mabingwa na Mbrazil, Neymar huenda akawa bado anauguza maumivu ya kifundo cha mguu wa kulia.

Messi alifunga mabao yote mawili ya Barca jana Kombe la Mfalme

VOGTS, WOLFGANG WAIBUKIA KAMBI YA YANGA

Wachezaji wa zamani wa timu ya Taifa ya Ujerumani ambao kwa sasa ni makocha wa timu ya Taifa ya Azerbeijan Berti Vogts na msaidizi wake Wolfgang leo jioni kabla ya mazoezi waliibuka katika viwanja vya hotel ya Sueno Beach na kuongea kidogo na makocha wa Young Africans Hans na Mkwasa masuala ya kiufundi kisha kuagana nao na kuwaacha waendelee na progam yao ya mazoezi.
Vogts amabaye alikuwa kocha mkuu wa timu ya Taifa Ujerumani kwa miaka nane (1990-1998) na kufanikiwa kushinda kombe la Ulaya mwaka 1996, na kufika hatua ya robo fainali ya kombe la Dunia mwaka 1998 alikuwa ameambatana na kocha wake msaidizi Wolfagang .
Kocha mpya wa Young Africans mholanzi Hans Van Der Plyum leo ameanza rasmi kazi ya kukinoa kikosi cha mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania bara katika viwanja vya hoteli ya Sueno Beach Side baada ya jana kuiongoza katika ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya timu ya Altay SK.

Mkwasa na Wolfagang

Wednesday 15 January 2014

YANGA YAMKARIBISHA KWA 2-0 BABU MHOLANZI, OKWI NA DIDIER WAFANYA KWELI, KIIZA AKOSA PENALTI

Na Baraka Kizuguto, Antalya
YANGA imemkaribisha vizuri kocha Mkuu mpya Hans van der Pluijm leo baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya timu ya Altay SK iliyopo Ligi Daraja la pili nchini Uturuki katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliofanyika leo mchana katika viwanja vya Sueno eneo la Side Manavgat.
Kocha Hans ambaye aliwasili jana jioni na kuongea na wachezaji kwa pamoja kabla ya chakula cha usiku alisisitiza nidhamu, upendo na kujituma miongoni mwa wachezaji na benchi la ufundi kitu ambacho mpaka sasa amefurahishwa na ushirikiano anaopewa na wachezaji na viongozi kwa ujumla.

Kocha Pluijm aliiona Yanga kwa mara ya kwanza leo Antalya

SIMBA SC KUCHEZA NA MTIBWA SUGAR UWANJA WA TAIFA JUMAMOSI


Simba SC itacheza mchezo wa kirafiki na Mtibwa Sugar ya Morogoro Jumamosi wiki hii Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Mchezo huo unakuja siku chache baada ya timu hiyo kushika nafasi ya pili kwenye Kombe la Mapinduzi visiwani Zanzibar, kufuatia kufungwa 1-0 na KCC ya Uganda Jumatatu wiki hii, Uwanja wa Amaan, Unguja. Aidha huo utakuwa mchezo wa kwanza Simba kucheza nyumbani, tangu imfunge mpinzani wake wa jadi, Yanga SC 3-1 kwenye mechi ya Nani Mtani Jembe, Desemba 21, mwaka huu.

BAADA YA B12 NA ADAMU MCHOMVU KUTIMULIWA CLOUDS KIJANA HUYU NDIO AMESHIKA MIKOBA YAO



Raymond Mshana (25), mzaliwa wa Same, Kilimanjaro.
HIVI karibuni, watangazaji nyota waliojizolea umaarufu mkubwa Bongo kupitia Redio Clouds FM, wakitangaza kipindi cha XXL, Hamisi Mandi ‘B12’ na Adam Mchomvu ‘Baba John’ walisimamishwa kazi kituoni hapo kwa muda usiojulikana.

Tuesday 14 January 2014

COASTAL UNION YAENDELEZA UBABE OMAN, MTAWAKOMA WAKIRUDI LIGI KUU


Coastal Union ya Tanga imeshinda mechi ya pili mfululizo katika ziara yake ya Oman, baada ya jioni ya leo kuwafunga wenyeji Nadi Oman mabao 2-0 kwenye Uwanja wa mjini Muscat. Mabao ya mabingwa hao wa Ligi Kuu 1988 yalitiwa kimiani na wachezaji waliopandishwa kutoka timu ya vijana, mshambuliaji Mohammed Miraj na beki Yussuf Chuma.

OMBI LANGU LA “KIJINGA” KWA RAIS WA TFF.




Kheri ya mwaka mpya ndugu watanzania mahali popote mlipo. Ujinga ni sehemu ya maisha na kila mwanadamu yawezekana ana mambo yake ya kijinga. Mimi natumia muda huu kuja na ombi langu la kijinga kwa raisi mpya wa TFF.

ARSENAL KUTOA PAUNI MILIONI 37 KUMSAJILI 'NEW VAN PERSIE, NI KINDA HATARI LA UJERUMANI...WENGER UDENDA WAMWAGIKA

KLABU ya Arsenal ipo tayari kutoa Pauni Milioni 37 kumnunua kinda mwenye kipaj Mjerumani ambaye wanaamini atakuwa Robin van Persie mwingine.

Sunday 12 January 2014

CHELSEA YATOA PAUNI MILIONI 25 KUMSAJILI NEMANJA

KLABU ya Chelsea imetoa ofa ya Pauni Milioni 25 kumsajili kiungo wa Benfica ya Ureno, Nemanja Matic arejee Stamford Bridge.
Kiungo huyo hodari alijiunga na Chelsea mwaka 2009, lakini akacheza mechi mbili tu kabla ya kutimkia Ureno mwaka kama sehemu ya dili ya David Luiz kutua Stamford Bridge.
Pamoja nayo, kocha Jose Mourinho sasa anaona Matic kama mtu anayefaa katika nafasi ya kiungo mkabaji wa timu yake.

Anarudi? Kiungo wa Benfica, Nemanja Matic (kulia) anahusishwa na kurejea Chelsea kwa Pauni Milioni 25

REAL MADRID YAZIPUMULIA BARCA NA ATLETICO KILELENI..LA LIGA NAYO MWAKA HUU USIIPIMIE!

NAYO MWAKA HUU USIIPIMIE!
TIMU ya Real Madrid imepunguza pengo la pointi hadi kubaki tatu dhidi ya vinara Barcelona na Atlecito Madrid wenye pointi 50 kila mmoja, kufuatia ushindi wa 1-0 ugenini dhidi ya Espanyol.
Shukrani kwake kiungo wa zamani wa Tottenham, Luka Modric aliyefanya kazi nzuri ya kutengeneza bao hilo pekee linaloifanya Real iendelee kuwamo kwenye mbio za ubingwa kwa kufikisha pointi 47.
Nyota huyo wa Croatia, alileta raha ndani ya kikosi cha Carlo Ancelotti dhidi ya Espanyol baada ya kupiga shuti zuri la mpira wa adhabu lililounganishwa kimiani na beki Mreno, Pepe.

Juu kwa juu: Beki wa Real Madrid, Pepe akiruka juu kufungwa kwa kichwa bao pekee la ushindi la timu yake jana

SIMBA SC YAWANIA TAJI LA 40 LEO

Na Mahmoud Zubeiry, Zanzibar
TIMU ya soka ya Simba SC, leo inawania taji la 40 tangu ianzishwe mwaka 1936, wakati itakapomenyana na KCC ya Uganda katika Fainali ya Kombe la Mapinduzi, Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Timu hiyo maarufu kama Wekundu wa Msimbazi, ilianzishwa mwaka 1936, enzi hizo ikijulikana kwa jina la Queens, yaani Watoto wa Malkia, kabla ya baadaye kubadilisha jina na kuwa Eagles, yaani ndege aina ya Tai, jina ambalo halikudumu sana nalo likatupwa na kuwa Sunderland, ambalo lilidumu hadi mwaka 1971 lilipobadilishwa na kuwa Simba SC hadi leo.

Kikosi kazi; Kikosi cha Simba SC katika Kombe la Mapinduzi

Hawa ndo wachezaji pekee aliokua akiwahofia ubingwa Yaya Toure


Mara nyingi hutokea kwenye mashindano yoyote kuna mtu au watu utakua unawahofia pengine kulingana na viwango sawa vya uchezaji au wao kukuzidi maarifa kidogo,hiko ndicho kilichotokea kwa Nyota toka Manchester City mchezaji Yaya Toure ambaye ameshinda kwa mara ya tatu mfululizo tuzo ya mchezaji bora barani Afrika,ushindi ambao umekosolewa na maafisa wakuu wa soka nchini Nigeria.

MAN CITY YAREJEA KILELENI LIGI KUU ENGLAND, MWAKA HUU KAZI IPO

MABAO ya Edin Dzeko na Alvaro Negredo yametosha kuipa ushindi wa 2-0 Manchester City dhidi ya Newcastle Uwanja wa St James Park na kurejea kileleni mwa Ligi Kuu England.
Nyota wa Bosnia alifunga bao la kwanza dakika ya nane akiunganisha krosi ya Aleksandar Kolarov kumtungua kipa Tim Krul.
Kikosi cha Alan Pardew kilidhani kimepata bao la kusawazisha baada ya shuti la mbali la Cheick Tiote kumpita kipa Joe Hart na kutinga nyavuni, lakini likakataliwa kwa sababu Yoan Gouffran alikuwa ameotea.
Negredo akaifungia City bao la pili dakika za majeruhi. Ushindi huo unaifanya City irejee kileleni baada ya kutimiza pointi 47 kutokana na mechi 21, ikiishusha Chelsea yenye pointi 46 baada ya kucheza mechi 21 pia katika nafasi ya pili. Arsenal sasa ni ya tatu kwa pointi zake 45, ingawa imecheza mechi 20.


Kazi nzuri: Mshambuliaji wa Manchester City, Edin Dzeko (kulia) akimtungua kipa wa Newcastle, Tim Krul kuifungia bao la kwanza timu yake

MALINZI AANZA KUPAMBANA NA DAWA ZA KULEVYA SOKA YA TANZANIA

Na Boniface Wambu, Ilala
RAIS wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amezindua programu ya kutoa elimu ya kupambana na matumizi ya dawa za kulevya kwa vijana iitwayo Ishi Huru.
Programu hiyo iliyozimduliwa jana (Januari 10 mwaka huu) jijini Dar es Salaam iko chini ya taasisi ya Africa Inside Out inayoongozwa na Rebecca Young wakati washirika (partners) ni TFF na kampuni ya Rhino Resources ya Marekani.



Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi akizungumza kwenye uzinduzi wa programu ya Ishi Huru jijini Dar esSalaam.

WABUNGE WA MUUNGANO WAKIWAPASHIA WAWAKILISHI LEO GYMKHANA, HUYO HALIMA MDEE NA ESTHER BULAYA...


Mbunge wa jimbo la Kawe, Dar es Salaam, Halima Mdee kushoto akiruka juu kuwania mpira wakati wa mazoezi ya timu ya Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jioni leo Uwanja wa Gymkhana, Zanzibar kujiandaa na mchezo dhidi ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar kesho kwenye Uwanja huo katika mfululizo wa sherehe za miaka 50 ya mapinduzi ya Zanzibar.