Pages

ELIMU KWANZA.

ELIMU KWANZA.
FEDHA SIO KIPAUMBELE CHETU.

Thursday 16 January 2014

RIHANNA AJICHORA TATTOO YA MSALABA MKONONI, ASEMA ANAPENDA MAMBO YA KIROHO


Rihanna akijipiga picha kwa simu yake baada ya tattoo yake kukamilika ©Twitter/Rihanna News
Mwanamuziki Rihanna mzaliwa wa Barbados amejichora (tattoo) ya msalaba mdogo katika mkono wake wa kuume na kusifia mchoro huo ambao kwa mwanamuziki huyo unamuongezea michoro mingine ya kiroho iliyo mwilini mwake tangu aanze kujichora.

Mwanamuziki huyo mwenye historia ya kuimba kanisani enzi hizo akiwa kwao Barbados amechorwa tattoo hiyo na mchoraji maarufu wa jijini New York nchini Marekani ambaye pia alihusika kumchora tattoo mwimbaji mwingine kinda Justine Bieber aitwaye Bang Bang ambaye hata kwa upande wake amesifia mchoro huo aliomchora mwimbaji huyo.

Rihanna kwa nyakati tofauti amewahi kukaririwa akisema anahusudu sana michoro hiyo ama tattoo na kwamba mwilini mwake ana michoro zaidi ya 20 ikiwemo inayohusiana na mambo ya Kiroho kitu ambacho hata mchoro huo mpya umeingia kwenye idadi hiyo.



Hata hivyo kujichora kwake msalaba aimaanishi kwamba ameokoka ingawa ameonekana kupenda sana mambo ya Kiroho katika maisha yake ambayo yametawaliwa na mizunguko ya hapa na pale inayomfanya watu wakamtoa katika idadi ya watu watakaorithi uzima(ingawa siri hiyo anaijua muhusika na Mungu wa mbinguni). Endelea kumuombea mwimbaji huyo kwamba isije ikawa ni kujichora tu bali pia aweze kurudi kanisani kumtukuza Mungu.

Chanzo : CP

No comments:

Post a Comment