Pages

ELIMU KWANZA.

ELIMU KWANZA.
FEDHA SIO KIPAUMBELE CHETU.

Saturday 18 January 2014

ARSENAL YAJIWEKA SAWA KILELENI EPL



Santi Cazorla akishangilia baada ya kuifungia Arsenal. Anayemfuata nyuma ni Olivier Giroud.

ARSENAL imekaa mguu sawa kileleni mwa Ligi Kuu ya England kufuatia ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Fulham jioni hii Uwanja wa Emirates.
Shukrani kwake mfungaji wa mabao hayo, Santi Cazorla dakika ya 57 akimalizia pasi ya Jack Wilshere na la pili dakika ya 62. Arsenal sasa inatimiza pointi 51 baada ya kucheza mechi 22.

Wakati huo huo Manchester City imeendelea kuwa mshindani mkuu wa Arsenal kileleni, baada ya kuifunga Cardiff City mabao 4-2 jioni hii Uwanja wa Etihad.
Edin Dzeko alifunga bao la kwanza dakika ya 14, pasi David Silva, Noone akawasawazishia wageni dakika ya 29 pasi ya Gunnarsson kabla ya Jesus Navas kuwafungia wenyeji la pili dakika ya 33.
Kipindi cha pili, City waliingia na moto na kupata bao la tatu dakika ya 77, mfungaji Mwanasoka Bora wa Afrika, Yaya Toure, pasi ya Sergio Aguero. Aguero aliifunga bao la nne City dakika ya 79, pasi ya Yaya kabla ya Campbell kuifungia Cardiff la pili dakika za majeruhi, pasi ya Eikrem.
Ushindi huo unaifanya City ifikishe pointi 50 baada ya kucheza 22, tofauti ya pointi moja na vinara Arsenal.
Katika mechi nyingine za ligi hiyo jioni hii, Sunderland ilitoka sare ya 2-2 na Southampton, Crystal Palace imeifunga 1-0 Stoke City, Norwich City imeifunga 1-0 Hull City na West Ham United imelala 2-1 nyumbani mbele ya Newcastle United.

No comments:

Post a Comment