
Klabu ya Simba imefanikiwa kukata tiketi ya kucheza fainali ya kombe la Mapinduzi baada ya kuifunga URA ya Uganda mabao 2-0.
mabao ya Simba kwenye mchezo huo yamefungwa na beki Joseph Owino pamoja na kiungo Amri Kiemba huku kiungo Owen Kasule wa URA akilimwa kadi nyekundu kwa kumchezea madhambi Ramadhani Singano.
Simba sasa itacheza fainali siku ya Jumatatu na timu ya KCC pia toka nchini UGANDA iliyoitoa AZAM kwa mabao 3-2.

Hingera rasta; Wachezaji wa Simba wakimpongeza mwenzao, Amri Kiemba kushoto baada ya kufunga bao la pili katika Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Simba rahaa

Amri Kiemba akipambana na mabeki wa URA

Ramadhani Singano ''Messi' akifanya yake dhidi ya beki wa URA

Messi ni balaa

Beki wa Simba, Haruna Shamte akimdhibiti mshambuliaji wa URA

Beki wa URA akimdhibiti msambuliaji wa Simba, Amisi Tambwe

Mfungaji wao bao la kwanza la Simba SC, Joseph Owino akiondoka na mpira

Awadh Juma wa Simba SC akipasua katikati ya wachezaji wa URA

Kiungo wa URA Milos Ilic akimtoka mchezaji wa Simba SC, Haroun Chanongo

Issa Rashid 'Baba Ubaya' wa Simba akigombea mpira na mchezaji wa URA

Katikati ni Amri Kiemba akiwa amesujudu baada ya kufunga bao la pili

Shabiki maarufu wa Simba SC, Abdulfatah Salim Saleh, mmiliki wa hoteli a Sapphire Court mjini Dar es Salaam kulia alikuwepo

Kikosi cha Simba SC leo

Makocha wa Simba SC kulia na wakisalimiana na makocha wa URA kabla ya mechi, Simba SC itamenyana na KCC ya Uganda pia katika fainali keshokutwa baada ya timu zote za Tanzania zilizoshiriki mashindano hayo kutolewa.