Pages

ELIMU KWANZA.

ELIMU KWANZA.
FEDHA SIO KIPAUMBELE CHETU.

Monday 6 January 2014

RONALDO AFIKISHA MABAO 400 USIKU HUU AKIIFUNGIA MAWILI REAL IKIUA 3-0 LA LIGA

MSHAMBULIAJI Cristiano Ronaldo usiku huu amefunga bao la 400 katika jumla ya mechi 652 alizocheza, wakati Real Madrid ikiifunga Celta Vigo 3-0 na kuwakaribia vinara wa La Liga, Barcelona kileleni.
Ronaldo alifunga mabao yake katika dakika za 20 na 90 akimalizia krosi za Dani Carvajal na baadaye Gareth Bale, aliyetokea benchi kipindi cha pili, wakati bao lingine la Real limefungwa na Benzema dakika ya 67.
Mabao yake hayo mawili yanamfanya msimu huu atimize jumla ya mabao 29 katika mechi 22 alizocheza, ukiwa ni mwanzo mzuri mwaka huu 2014, baada ya mwaka 2013 kufunga jumla ya mabao 69.

Tabasamu la raha: Mshambuliaji wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo akishangilia baada ya kufunga bao lake la 400


Wawili ghali: Gareth Bale akimpongeza Ronaldo baada ya kufunga bao la 400

Mkali wa mabao: Cristiano Ronaldo akishangilia bao la 400

No comments:

Post a Comment