Huku ikiripotiwa kwamba tayari Paris St Germain wanamtaka kiungo huyo Mbelgiji wa Chelsea, Mourinho amesema wiki hii kwamba hatakubali hata ofa ya Pauni 100,000.
Alifunga bao lake dakika ya 57 kabla ya Fernando Torres kufunga la pili dakika tatu kuelekea mwishoni mwa mchezo. Chelsea imetimiza pointi 46 baada ya kucheza mechi 21 ikiwa juu ya Arsenal yenye pointi 45 na Manchester City pointi 44, ambazo zimecheza mechi 20.

Yuko sawa: Eden Hazard alifunga bao la kwanza Chelsea ikiilaza Hull City

Hazard (wa pili kushoto) akifumua shuti kumtungua kipa wa Hull, Allan McGregor
No comments:
Post a Comment