Pages

ELIMU KWANZA.

ELIMU KWANZA.
FEDHA SIO KIPAUMBELE CHETU.

Saturday, 11 January 2014

KOCHA ALIYEMUIBUA VAN NISTERLOOY AJA KESHO KUFANYA MAZUNGUMZO NA YANGA

Na Prince Akbar, Dar es Salaam
KLABU ya Yanga SC imemualika kwa mazungumzo, kocha ‘babu’, Johannes Franciscus ‘Hans’ van der Pluijm, aliyewahi kuifundisha Berekum Chelsea ya Ghana, ambaye anaweza kutua Dar es Salaam kesho iwapo atafanikiwa kupata ndege.
Hakuna nafasi katika ndege za kutoka Ghana kuja Dar es Salaam na babu huyo anahaha kutafuta ndege ya kuunganisha na kama akifanikiwa basi atakuja nchini kesho, ikishindana wakati wowote mapema wiki ijayo.

Atakuwa kocha mpya wa Yanga? Hans van der Pluijm anatarajiwa kutua kesho kwa mazungumzo

Pluijm anakuja kufanya mazungumzo na Yanga, baada ya uongozi wa klabu hiyo kuridhishwa na wasifu wake katika orodha ndefu ya walimu zaidi ya 30 walioomba kazi Jangwani.
Franciscus Johannes ‘Hans’ van der Pluijm alizaliwa Januari 3 mwaka 1949 na alianzia kwenye kucheza soka akiwa kipa.
Enzi zake aliidakia kwa miaka 28 klabu ya FC Den Bosch akicheza mechi 338 ndani ya misimu 18 na alipostaafu baada ya kuumia goti akawa kocha wa timu hiyo.
Alianza vyema ukocha akiiwezesha FC Den Bosch kutwaa ubingwa wa Daraja la Kwanza na kupanda Ligi Kuu na ndiye aliyempa nafasi ya kwanza mshambuliaji Ruud van Nistelrooy akiwa kinda wa miaka 17 tu kucheza kikosi cha kwanza cha timu hiyo.

Van Nisterlooy aliibuliwa na van der Pluijm

Aprili mwaka 1995, alisaini Mkataba wa miaka miwili na SBV Excelsior kabla ya kutimuliwa Januari 1997 na nafasi yake ikachukuliwa na Msaidizi wake, John Metgod.
Hiyo ilifuatia timu hiyo ya Rotterdam kushinda mechi mbili tu na sare tatu katika mechi 17 za msimu mzima.
Baada ya kuboronga Ulaya, ndipo akahamia Afrika mwaka 1999, alipokwenda kufundisha Ashanti Gold SC ya Ghana, akianza na Mkataba wa mwaka mmoja.
Ajax ya Uholanzi ikanunua hisa katika klabu hiyo Ijumaa ya Juni 18, mwaka 1999 asilimia 51 naye akatupiwa virago na kuhamia Saint-George SA ya Ethiopia kabla ya mwaka 2010 kujiunga na B-juniors Feyenoord ya Ghana, ambayo ni tawi la timu hiyo ya Rotterdam.
Mwaka 2012 alijiunga na Berekum Chelsea ambako pia alifukuzwa mwaka jana na kuhamia Medeama ya Ghana pia ambako nako alifukuzwa baada ya mechi saba tu, kufuatia matokeo mabaya mwanzo mwa msimu, akivuna pointi nane kati ya 21.
Je, mwalimu huyu ataisaida Yanga SC, au imeuvagaa mkenge mwingine baada ya kumtema Mholanzi mwenzake, Ernie Brandts mwezi uliopita?

No comments:

Post a Comment