Santi Cazorla alifuga bao la kwanza dakika ya 31 kabla ya Tomas Rosicky kufunga la pili 62.
Tottenham, ambayo ilionyesha kuimarika chini ya kocha mpya, Tim Sherwood, ilizidiwa katika safu ya kiungo na washambuliaji wake Emmanuel Adebayor na Roberto Soldado wakajikuta hawana madhara uwanjani.

Matawi ya juu: Kiungo wa Arsenal, Santi Cazorla akishangilia baada ya kufunga dhidi ya Tottenham
Katika mechi nyingine, Manchester City ikiwa pungufu ya mchezaji mmoja ililazimishwa kwenda kwenye mchezo wa marudiano baada ya bao la Scott Dann kuwapa sare ya 1-1 Blackburn Uwanja wa Ewood Park, kufuatia Alvaro Negredo kutangulia kufunga kipindi ca kwanza