Pages

ELIMU KWANZA.

ELIMU KWANZA.
FEDHA SIO KIPAUMBELE CHETU.

Saturday 4 January 2014

ARSENAL RAHA KWA KWENDA MBELE, MAN CITY MGUU NJE, NDANI FA

TIMU ya soka ya Arsenal imefuzu kutinga Raundi ya Nne ya Kombe la FA baada ya kuwafunga wapinzani wa London Kaskazini, Tottenham mabao 2-0 Uwanja wa Emirates.
Santi Cazorla alifuga bao la kwanza dakika ya 31 kabla ya Tomas Rosicky kufunga la pili 62.
Tottenham, ambayo ilionyesha kuimarika chini ya kocha mpya, Tim Sherwood, ilizidiwa katika safu ya kiungo na washambuliaji wake Emmanuel Adebayor na Roberto Soldado wakajikuta hawana madhara uwanjani.

Matawi ya juu: Kiungo wa Arsenal, Santi Cazorla akishangilia baada ya kufunga dhidi ya Tottenham
Katika mechi nyingine, Manchester City ikiwa pungufu ya mchezaji mmoja ililazimishwa kwenda kwenye mchezo wa marudiano baada ya bao la Scott Dann kuwapa sare ya 1-1 Blackburn Uwanja wa Ewood Park, kufuatia Alvaro Negredo kutangulia kufunga kipindi ca kwanza
City ilimpoteza Dedryck Boyata aliyeonyeshwa kadi nyekundu.Katika mechi nyingine, Barnsley imefungwa 2-1 na Coventry City, Yeovil Town imeifunga 4 - 0 Leyton Orient, Bristol City imetoka 1 - 1 na Watford, Southend United imeifunga 4 - 1 Millwall, Middlesbrough imefungwa 2-0 na Hull City, West Bromwich imefungwa 2-0 na Crystal Palace, Kidderminsterimetoka 0 - 0 na Peterborough.
Doncaster Rovers imefungwa 3-2 na Stevenage, Stoke City imeifunga 2 - 1 na Leicester City, Southampton imeifunga 4 - 3 Burnley, Newcastle United imefungwa 2-1 na Cardiff City, Rochdale imeshinda 2 - 0 dhidi ya Leeds United, Wigan Athletic imetoka 3 - 3 na Milton Keynes Dons, Norwich City imetoka 1 - 1 na Fulham.
Aston Villa imefungwa 2-1 na Sheffield United, Macclesfield Town imetoka 1 - 1 na Sheffield Wednesday, Bolton Wanderers imeshnda 2 - 1 dhidi ya Blackpool, Everton imeifunga 4 - 0 Queens Park Rangers Brighton imeifunga 1 - 0 Reading, Grimsby Town imefungwa 3-2 na Huddersfield Town, Ipswich Town imetoka 1 - 1 na Preston North End.

Beki wa Blackburn, Scott Dann akimtungua kipa Costel Pantilimon kuifungia timu yake bao la kusawazisha dhidi ya Manchester City

No comments:

Post a Comment