Pages

ELIMU KWANZA.

ELIMU KWANZA.
FEDHA SIO KIPAUMBELE CHETU.

Saturday 4 January 2014

RANGI YA MWAKA 2014 NI ZAMBARAU



Mwaka 2013 umemalizika na tumeanza mwaka mpya wa 2014 tukiwa na matumaini mapya. Kama ilivyo ada kila mwaka huwa kuna rangi inayotawala ambayo kwa kawaida hutangazwa na Kampuni ya Pentone ya nchini Marekani.
Rangi ya mwaka 2013 ilikuwa kijani iliyokolea, ambapo ilishuhudiwa wabunifu mbalimbali wa mitindo ya mavazi, hata mapambo wakiitumia katika maonyesho yao ya matoleo mapya ya kazi zao.

Kwa mwaka huu. tayari rangi ya mwaka imetajwa na tayari baadhi ya wabunifu wameshatoa matoleo yao mapya wakiyanakshi kwa rangi hiyo.

Unajua ni rangi gani?

Rangi ya mwaka 2014 ni Zambarau. Inajulikana kama Zambarau mpauko kwa Kiingereza ikiitwa;' Radiant Orchid'.

Wataalamu wa mambo ya rangi wanaitaja rangi hii kuwa miongoni mwa
'secondary color', yaani rangi inayotokana na mchanganyiko wa rangi nyingine za msingi. Rangi hizo ni nyekundu na bluu.

Ni miongoni mwa rangi za kuvutia zinazotumiwa na watu wa rika na jinsia zote. Katika kipindi cha hivi karibuni, rangi hiyo imeshuhudiwa ikitumiwa kwa madhumini tofauti, hivyo kufanya mandhari husika kuwa na mvuto wa kipekee.

Licha ya kupendeza kwenye kucha, midomoni, hata kwenye maeneo mengine mwilini, rangi hiyo inavutia zaidi kwenye vyakula; kwa mfano katika keki na hata vinywaji.

'Zambarau inaendana na rangi gani?

Jinsi ya kuichanganya rangi hii itatagemea na aina gani ya uliyotumia kwani zipo aina nyingi, zenye mwonekano tofauti. Hivyo, mtumiaji anatakiwa kuwa makini katika hili.

Wakati mwingine unaweza kuchanganya zambarau iliyokolea na ile iliyopauka, pia ukaleta maana katika mitindo. Katika hili unashauriwa kutumia rangi moja kwa kiasi kidogo zaidi ya nyingine, ili kuifanya ionekane zaidi.

Pia kama utatumia zambarau ya kukoza, pia siyo vibaya ikiwa utatumia rangi nyingine za kuwaka katika kupamba au kunakshi vazi lako. Pamoja na hayo, wataalamu wanashauri wavaaji kutotumia rangi hiyo katika mavazi kuanzia kichwani hadi mguuni.

Jambo hili litakufanya usifikie lengo lako la kupendeza,badala yake utaonekana kichekesho.

Umuhimu wa rangi ya zambarau katika mitindo

Rangi ya zambarau inamaanisha maisha. Ni miongoni mwa rangi zenye nguvu zaidi za kuvuta hisia kimaisha. Kwa kuvaa rangi hii utakuwa mwenye kujiamini, kama vile haitoshi, utakuwa mwenye kuweka nguvu zaidi katika mambo yako yajayo.

Tofauti na rangi nyingine, rangi hii ina sifa mbili. Unaweza kuvaa na kuonekana mnene, wakati huohuo unaweza kuvaa na kuoenekana mwembamba zaidi ya umbo lako halisi.

Ikiwa utavaa zambarau ya giza, utaonekana mwembamba kuliko uhalisia wako na ukivaa ya kuwaka utaonekana kinyume chake.

Rangi hii ina sifa zinazofanana na rangi ya njano, 'hot pink'

na rangi nyingine zinazofanana hizo. Kitendo cha kuonekana haraka kabla ya nyingine, hujenga hisia ya kujiamini kwa mvaaji husika.

Nenda na wakati , tupia zambarau! Chanzo: Mwananchi

No comments:

Post a Comment