1. Wachezaji na viongozi wa timu itakayosababisha mchezo kuvurugika na hatimaye kuvunjwa, itapoteza mchezo huo hata kama ilikuwa inaongoza kwa magoli na timu pinzani itapewa ushindi wa pointi tatu na magoli matatu, iwapo timu pinzani inaongoza kwa magoli zaidi ya matatu, itabakia na idadi ya magoli hayo iliyokwishafunga.
2. Magoli yaliyofungwa na wachezaji wa timu iliyosababisha mchezo kuvunjika yatafutwa lakini magoli yaliyofungwa na timu pinzani hayatofutwa na yataendelea kuonekana katika idadi ya magoli yaliyofungwa na wachezaji wa timu hiyo wakati wa kutafuta mfungaji bora.
3. Endapo itatokea vurugu ya aina yoyote ile na kusababisha mchezo kusimama, mwamuzi atasubiri kwa dakika zisizozidi kumi na tano, na endapo hali ya vurugu bado inaendelea mwamuzi atavunja mchezo na kuwasilisha taarifa ya mchezo kwa kamati ya Usimamizi ya ngazi husika.
4. Timu iliyosababisha vurugu itapoteza mapato yote ya mchezo.
5. Timu iliyosababisha kuvurugika kwa mchezo italipa faini ya shilingi 300,000/=.
3. Faini hiyo italipwa kabla ya mchezo unaofuatia.
4. Mchezaji/wachezaji na kiongozi/viongozi watakao bainika kusababisha vurugu zilizopelekea mchezo huo kuvunjika watafungiwa kujihusiha namasuala yote ya mpira kwa kipindi cha miaka mitano.
5. Endapo uvunjikaji wa mchezo utakuwa nje ya kanuni ya 22(3), mchezo huo utarudiwa kama inavyoainishwa katika kanuni ya 9(e) na utachezeshwa na waamuzi wengine katika siku itakayo pangwa na chombo husika.
No comments:
Post a Comment