Pages

ELIMU KWANZA.

ELIMU KWANZA.
FEDHA SIO KIPAUMBELE CHETU.

Wednesday 1 January 2014

YAYA TOURE AING'ARISHA MAN CITY ENGLAND Pia ARSENAL imeua 2.0

KLABU ya Manchester City imeanza vyema mwaka 2014 baada ya mabao ya kipindi cha pili ya Yaya Toure na Aleksandar Kolarov kuwapa ushindi wa 3-2 dhidi ya Swansea huo ukiwa ushindi wa tano mfululizo katika Ligi Kuu ya England.
Fernandinho aliifungia City bao la kuongoza, kabla ya Wilfried Bony kuisawazuishia Swansea dakika ya mwisho kipindi cha kwanza.
Lakini Toure akwafungia wageni bao la pili hilo likiwa bao lake la 12 la msimu na Kolarov akafunga la tatu kwa jithada binafsi kabla ya Bony kuifungia tena Swansea. Ushindi huo unaifanya City itimize pointi 44 baada ya kucheza mechi 20.

Bao muhimu: Yaya Toure akiifungia Manchester City bao muhimu leo Uwanja wa Liberty

No comments:

Post a Comment