Thursday, 2 January 2014
Alichokisema Zitto Kabwe kuhusiana na Kesi yake Mahakamani, tazama pia jibu alilotoa John Mnyika
Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe leo ameingia kwenye headline kuhusiana na kile alichokiwasilisha kwenye mahakama kuu juu ya kupinga kujadiliwa kwenye kikao cha kamati kuu ya Chadema,Kikao ambacho kilikuwa kikutane kesho.
Kikao hicho kilikuwa na hoja mbalimbali ikiwa ni pamoja na hoja inayomhusu Zitto,Millardayo.com imepiga exclusive interview na Zitto Kabwe mara baada ya kutoka kwenye viwanja vya mahakama hiki ndicho alichokizungumza juu ya shauri lake alilopeleka mahakamani.
‘Tumekwenda mahakamani kwa ajili ya jambo moja tu kutaka haki itendeke kwa sababu mahakaama ndiyo chombo cha juu kabisa kwenye nchi yetu cha kuweza kutenda haki mara baada ya kamati kuu ya chama changu kufanya maamuzi ya kunivua nafasi zangu ambayo niliandikiwa makosa 11′
‘Nilikata rufaa kwenye baraza kuu la chama ili baraza kuu liweze kuona kama kamati kuu ilifata taratibu za chama kufikia maamuzi yale japo mimi naamini haijafata taratibu za chama lakini kwa bahati mbaya viongozi wangu wa chama changu wameamua kuendelea na kikao cha kamati kuu’.
‘Hawajajibu barua yangu ya nia ya kukata rufaa na kuweza kupatiwa taarifa na mwenendo wa kikao ili niweze kukata rufaa kwa mujibu wa chama Kwa hiyo nimekwenda mahakani ili mahakama iweze kutoa maamuzi ya mimi kuweza kupata nafasi ya kusikilizwa na kujadiliwa’.
‘Nashukuru Jaji John Utamwa ametoa amri ya muda ya kuzuia kamati kuu ya chama kunijadili mpaka hapo Chadema watakapoweza kujibu hoja zilizotolewa na mwanasheria wangu Albert Msando’.
‘Kesho tunarudi mahakamani kwa ajili ya kuendelea na kuweza kupokea majibu kutoka Chadema lakini kikao cha kesho kamati kuu imezuiliwa na mahakama kujadili hoja yoyote inayonihusu,lakini pia mapingamizi yote mwanasheria wa Chadema Tundu Lissu aliyokua ameyaweka dhidi ya mwanasheria wangu Jaji ameyatupilia mbali kwa hiyo kesi inaendelea’.
‘Muhimu katika hili ni haki na mimi kama mtu ambaye siku zote natetea haki sasa ni fursa yangu kutetea haki yangu mwenyewe ya kuweza kusikilizwa ya kutumia taratibu zote za chama katika hali ya kawaida baraza kuu la chama liitwe kwanza lijadili jambo hili kabla ya kikao cha kamati kuu kuitwa’.
Hata hivyo Mbunge wa Ubungo John Mnyika aliijibu tweet yangu ya stori ya Amplifaya kuhusu Zitto Kabwe na hii ishu ya Mahakama.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment