Cristiano Ronaldo sasa yupo katka nafasi nzuri ya kutwaa tuzo yake ya pili ya Ballon d'Or baada ya kufunga mabao matatu yaliyoipeleka Ureno kombe la dunia 2014.
Kwa mujibu wa Sporting Life, Ronaldo amemuondoa Franck Ribery katika kilele cha listi ya wachezaji waliokuwa wakipewa nafasi kubwa ya kutwaa tuzo hiyo.
Pia imeripotiwa kwamba shirikisho la soka duniani FIFA limeongeza muda wa kupiga kura za kumchagua mshindi wa 2013 Ballon d'Or.
Uamuzi wa FIFA kuruhusu makocha na manahodha pamoja na waandishi kuwasilisha majina matatu ya Top 3 kabla ya Nov. 29 tofauti na mwanzo ilivyokuwa Nov. 15, limeleta maswali mengi kutoka kwa wadau wa soka kama ilivyoripotiwa na ESPN FC.