Pages

ELIMU KWANZA.

ELIMU KWANZA.
FEDHA SIO KIPAUMBELE CHETU.

Monday 18 November 2013

UHURU SULEIMAN MWAMBUNGU AREJEA SIMBA SC, ASEMA NI WAKATI WA KULIPA FADHILA MSIMBAZI



WINGA Uhuru Suleiman Mwambungu ameamua kurejea klabu yake ya Simba SC kumalizia Mkataba wake wa miezi saba kutoka Coastal Union ya Tanga alikopelekwa kwa mkopo mwanzoni mwa msimu.
Uhuru aliyekwenda Coastal akitokea Azam FC alikocheza pia kwa mkopo kwa nusu msimu, ameiambia BIN ZUBEIRY jana usiku kwamba tayari amekwishafuata taratibu za kumrejesha klabu yake.Amesema amekwishauarifu uongozi wa Coastal ambao umeandika barua ya kumrejesha Simba SC baada ya kuitumikia vizuri klabu hiyo katika mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu huu."Kama utakumbuka nilitolewa kwa mkopo Simba SC kwenda Azam FC Desemba mwaka jana kwa sababu sikuwa fiti, nilikuwa nimetoka kwenye maumivu. Lakini namshukuru Mungu nimefika Azam nimepata malezi mazuri na nimecheza kidogo hadi nimefanikiwa kuwa fiti,".
"Mwanzoni mwa msimu nimekwenda Coastal, huko kwa kweli ndiyo mambo yamekuwa mazuri zaidi, nimepata nafasi ya kutosha, nimecheza hadi sasa najiona kabisa nimerudi katika kiwango changu, hiyo ni kwa mtu yeyote aliyeniona anaweza kuthibitisha hilo,"alisema.
Uhuru alisema kwamba umewadia wakati sasa wa yeye kulipa fadhila kwa Simba SC baada ya kumgharimia matibabu ya goti nchini India mwaka juzi alipoumia na kukaa nje ya Uwanja kwa msimu mzima.
"Tangu nimepona kwa kweli sijapata fursa ya kulipa fadhila kwa Simba SC, na ninaamini huu ni wakati mwafaka sasa kuwalipa fadhila Simba SC na nimeamua kurudi klabu yangu, kurudi nyumbani kuisaidia timu yangu,"alisema.
Uhuru pia amesema amekwishafanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe ambaye ameafiki suala hilo na anatarajia mazoezi yatakapoanza atajiunga na wenzake.
Baada ya kuteswa na maumivu kwa miaka miwili, hatimaye Uhuru alionyesha amerejea katika kiwango chake katika mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu, akiichezea Coastal Union.
Pamoja na ujuzi wake, lakini uzoefu wa Uhuru ni kitu ambacho kinatarajiwa kuisaidia sana Smba SC iwapo atasajiliwa katika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu.
www.tabasamuleo.blogspot.com

No comments:

Post a Comment