Pages

ELIMU KWANZA.

ELIMU KWANZA.
FEDHA SIO KIPAUMBELE CHETU.

Saturday 14 December 2013

Hii ndo misukosuko iliyojitokeza kwenye utengenezaji wa nyimbo ya Rich Mavoco


Mara nyingi kunatokea vitu vingi sana kwenye maisha ya kimuziki ambavyo huwa hatuvifahamu na vingine hatudhani kama vinaweza kutokea.

Prodyuza kutoka Mazuu Records,Mazuu mwenye hits kadhaa kama Kidela ya Abdul Kiba,I love u ya Kassim Mganga Nakomaa na jiji ya Shilole na Roho yangu ya Rich Mavoco.kaelezea mazingira magumu aliyokutana nayo wakati wa utengenezaji wa nyimbo ya Roho yangu ya Rich Mavoco.

BAADA YA KUUMIA - HIZI NDIO MECHI 8 ATAKAZOZIKOSA ROBIN VAN PERSIE


Mshambuliaji wa Manchester United Robin van Persie atakosekana katika kikosi cha Manchester United kwa mwezi mmoja kutokana na maumivu ya nyama za paja.
Mshambuliaji huyo wa kiholanzi alipata maumivu hayo wakati akipiga kopna katika mchezo wa ushindi dhidi ya Shakhtar Donetsk jumanne usiku na hatocheza tena mpaka mwakani.

HENRY ASEMA ARSENAL INAWEZA KUCHEZA NA YEYOTE



KWANINI waogope? Arsenal inaweza kucheza na timu yoyote. Ndivyo anavyoamini mshambuliaji wa zamani wa timu hiyo, Thierry Henry, baada ya timu hiyo kujichongea kwa kushika nafasi ya pili katika kundi lake la Ligi ya Mabingwa Ulaya.

MR. BEAN MCHEKESHAJI MWENYE ELIMU KUBWA KICHWANI

beenclip_ad596.jpg
KWENYE safari yake ya kwenda mapumziko nchini Kenya mwaka 2001, rubani wa ndege yake binafsi alizimia wakiwa angani na hapo akalazimika kuongoza ndege hiyo kwa dakika kadhaa kabla ya rubani huyo kuzinduka na kuendelea na safari.
Hii si kama ilikuwa sehemu ya vipande vya filamu zake za vichekesho, bali lilikuwa tukio halisi. Hapa anazungumziwa Mr. Bean, mchekeshaji mashuhuri duniani katika filamu za komedi.
Mr. Bean ambaye jina lake halisi ni Rowan Sebastian Atkinson, ni mwigizaji mashuhuri Mwingereza ambaye amepata umaarufu mkubwa duniani kutokana na kuigiza filamu za komedi.
Akiwa amezaliwa Januari 6, 1955 na kushiriki kwenye filamu mbalimbali ikiwamo za ucheshi za Mr. Bean na Blackadder, Atkinson amekuwa tajiri mkubwa miongoni mwa waigizaji wa komedi na kuwa na pato linalokadiriwa kuwa la Dola 130 milioni. Umahiri wa filamu zake za komedi ndizo zinazofanya ziendelee kupendwa hadi sasa na hivyo kumwingizia pesa
Jinsi alivyopiga pesa

Friday 13 December 2013

VAN PERSIE AKANA KUMKUMBUKA FERGSUON, ASEMA MOYES POA SANA TU

Taarifa za Daily Star na Metro zilisema kwamba van Persie amewaambia rafiki zake anamkumbuka kocha wa zamani wa United, Sir Alex Ferguson, na Mholanzi huyo amesema hashawishiki na ufundishaji wa Moyes.

Van Persie alifurahia matunda katika mechi ya kufungua msimu, akifunga mabao mawili katika mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Wigan kabla ya kufunga tena mawili katika ushindi wa United wa 4-1 dhidi ya Swansea.


Mholanzi: Robin van Persie (katikati kushoto) ameshindwa kufunga kwenye Ligi Kuu chini ya kocha mpya, David Moyes

Amepagawa: Mholanzi huyo hakufurahia matokeo dhidi ya Liverpool
Pamoja na hayo, mshambuliaji huyo alishindwa kufurukuta katika sare ya United ya 0-0 nyumbani dhidi ya Chelsea kipigo cha 1-0 dhidi ya Liverpool.

Van Persie alionekana kuchanganyikiwa na hali ya mambo Anfield, na Mholanzi huyo alilimwa kadi ya njano na angeweza kutolewa nje kwa kadi nyekundu kilaini baada ya kupambana na Nahodha wa Liverpool, Steven Gerrard.
Lakini Van Persie, aliyefunga mabao 30 United msimu uliopita, amesema anafurahia zama mpya Old Trafford.


Chupuchupu nyekundu: Van Persie alikuwa ana bahati kutoonyeshwa kadi nyekundu baada ya kumchezea rafu Gerrard (katikati)

Baba: Kuna madai kwamba Van Persie anamkumbuka Ferguson, kocha aliyemnunua United
Aliliambia De Telegraaf: "Ni babu kubwa kufanya kazi na kocha mpya David Moyes. Ninafurahia mtindo wa Moyes. Anafanyisha mwenyewe mazoezi; yupo karibu na wachezaji na anatuandaa na kutupa maelekezo vizuri kwa mchezo dhidi ya wapinzani wafuatao. Ambayo inatuweka vizuri,".
"Kuna hali nzuri ya kufurahisha katika klabu. Taji la mwaka jana limetupa njaa zaidi ya mataji,"alisema.

HIKI NDICHO KIFO CHA SOKA YA WAINGEREZA...MAKOCHA TISA WAMWAGA FEDHA KUNUNUA WACHEZAJI LIGI KUU ENGLAND LAKINI HAKUNA MTOTO WA NYUMBANI HATA MMOJA

TULIJUA England wako hatarini kufuzu kushiriki kwenye Kombe la Dunia, tulijua timu ya vijana chini ya miaka 21 ya England haitavuka hatua ya Makundi katika michuano ya Ulaya wakati wa kiangazi – walifungwa mechi zote tatu wao wakifunga bao moja tu.
Tulijua timu ya vijana ya England chini ya miaka 20 itafanya vibaya wakati wa michuano ya dunia Uturuki na kabla ya kutoka katika hatua ya makundi. Timu ya England chini ya miaka 20 haijawahi kushinda mechi tangu wakati Jamie Carragher na Michael Owen walipoichezea mwaka 1997.

Kaa pembeni Waingereza: Brendan Rodgers hajasajili hata mchezaji mmoja wa nyumbani wakati wa kiangazi



Tunacheki pembeni: Manuel Pellegrini na Arsene Wenger wameamua kuamini vipaji vya nje.

Kombe la Chalenji limepita, tujipange kwa AFCON 2015

NA TANZANIA DAIMA
MICHUANO ya Kombe la Chalenji kwa nchi wanachama wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa), imefikia tamati jana mjini Nairobi, Kenya.

Tanzania, kwa sura ya Jamhuri ya Muungano, ilikuwa na timu mbili kwenye michuano hiyo ambazo ni Kilimanjaro Stars ya bara na Zanzibar Heroes kwa upande wa visiwani.

Lulu: Nadhani sihitaji simu ya mkononi



Elizabeth Michael maarufu Lulu.PICHA|MAKTABA
Na Herieth Makwetta,Mwananchi
Akiongea na Starehe, Lulu alibainisha kuwa kwa siku hupigiwa simu zisizokuwa na idadi na zisizo na faida kwake, lakini akakiri kwamba idadi kubwa ya watu wanaompigia simu ni mashabiki wake.
Mwigizaji anayefanya vizuri sokoni kwa sasa,Elizabeth Michael maarufu Lulu, amesema kuwa hatamani tena kutumia simu ya mkononi kwani amekuwa akisumbuliwa na watu wasiokuwa na mambo ya msingi ya kumweleza wanaompigia simu mara kwa mara.

HARAMBEE MABINGWA CHALLENGE 2013



Na Mahmoud Zubeiry, Nairobi
KENYA 'Harambee Stars' ndiyo mabingwa wapya wa Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge baada ya usiku huu kuifunga Sudan 'Mwewe wa Jangwani' mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Nyayo, Nairobi, Kenya.
Shukrani kwake, Nahodha wa timu hiyo, Alan Wanga aliyefunga mabao yote hayo katika mchezo wa leo uliokwenda sambamba na sherehe za miaka 50 ya Uhuru wa Kenya.

MATENGENEZO YA UWANJA WA SOKOINE MBEYA YAENDELEA!





Saleh Kupaza (kulia ) akiwa na mtaalam wa kutengeneza viwanja...

HATIMAE SIMBA YAMALIZANA NA IVO MAPUNDA NA BEKI DONALD MOSOTI OMWANWA




Simba pia imemsainisha beki wa kati wa Gor Mahia Donald Mosoti Omwanwa,amesaini mkataba wa miaka miwili mbele ya katibu mkuu wa Simba Evodius Mtawala.




Donald Mosoti Omwanwa.....

Ivo Mapunda akisaini mkataba wa miaka miwili kuichezea Simba mbele ya katibu mkuu wa timu hiyo Evodius Mtawala.

aibu ,ONA SIKU WACHEZAJI WA ZANZIBAR I WALIPOFUKUZWA HOTELINI KENYA!




Wednesday 11 December 2013

Kipigo cha Kili Stars chamuibua Ndolanga

ALIYEKUWA Mwenyekiti wa kilichokuwa Chama cha Soka Tanzania (FAT, sasa TFF), Muhidin Ndolanga, amesema chombo hicho chini ya Rais Jamal Malinzi hakitapata mafanikio kutokana na uwepo wa mabaki ya uongozi uliopita chini ya Leodegar Chilla Tenga.

DAVID MOYES ASAFIRI MPAKA JIJINI MADRID KUMUANGALIA KIUNGO KOKE - ATLETICO MADRID WATAJA BEI YA KUMUUZA


David Moyes alionekana kwenye dimba la Vicente Calderon kwenye mchezo wa Atletico Madrid dhidi ya Porto usiku wa jana.

Kocha huyo wa Manchester United anategemewa kufanya usajili wakati dirisha la usajili mwezi ujao litakapofunguliwa baada ya kuwa na mwanzo mbovu.

BAADA YA KUSHIKA NAFASI YA PILI - ARSENAL KUCHEZA 16 BORA DHIDI YA AIDHA BARCA, MADRID, ATLETICO, PSG AU BAYERN - TOA MAONI UNGEPENDA TIMU YAKO NA TIMU GANI?

TIMU ZA ENGLAND DHIDI YA TIMU AMBAZO ZINAWEZA KUPANGWA NAZO KATIKA 16 BORA YA CHAMPIONS LEAGUE. UNGEPENDA TIMU YAKO IPANGWE NA NANI? TOA MAONI…

Kocha mpya Simba awaweka kiporo majeruhi

Dar es Salaam. Baada ya kuwapinga panga wachezaji tisa, Kocha wa Simba, Zdravko Logarusic amewaweka kiporo wachezaji wanne ambao ni majeruhi.

Monday 9 December 2013

STARS DHIDI YA KENYA ‘INAYOBEBWA VIBAYA’ NA MAREFA CHALLENGE 2013,



Mungu Ibariki Tanzania: Kikosi cha Stars Challenge 2013 na chini ni Harambee....na "Washindwe".



Na Mahmoud Zubeiry, Machakos

TANZANIA Bara 'Kilimanjaro Stars', leo inashuka dimbani kwenye Uwanja wa Kenyatta, Machakos, kumenyana na wenyeji, Kenya 'Harambee Stars' katika Nusu Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge kuanzia saa 7:00 mchana.
Hii ni mara ya pili mfululizo kwa Stars chini ya kocha Mdenmark, Kim Poulsen kufika Nusu Fainali ya michuano hiyo, baada ya mwaka jana pia mjini Kampala, Uganda ambako ilitolewa na wenyeji, Uganda 'The Cranes' kwa kufungwa mabao 3-0
Lakini Kim, amelipa kisasi kwa The Cranes, baada ya Stars kuivua ubingwa Uganda Jumamosi kwa kuitoa kwenye Robo Fainali, Uwanja wa County ya Mombasa, zamani Manispaa kwa penalti 3-2, kufuatia sare ya 2-2 ndani ya dakika 90.

MESSI,RIBERY NA RONALDO WAINGIA FAINALI YA KUWANIA TUZO YA MWANASOKA BORA WA DUNIA.






CRISTIANO RONALDO AZUNGUMZIA UGUMU WA KUNDI WALILOPANGWA URENO KOMBE LA DUNIA - ASEMA ALIKUWA AMELALA WAKATI RATIBA INAPANGWA


Katika droo ya kupanga makundi ya kombe la dunia iliyofanyika Ijumaa iliyopita ulimwengu ulishuhudia kikosi cha Paul Bento kikipangwa katika kundi gumu la (Group G), kwa pamoja na Ujerumani, Ghana na USA - kundi pekee lenye timu zote nne zilizopita kwenda kwenye hatua ya mtoano katika michuano iliyopita ya kombe la dunia 2010.

BAADA YA KUPIGWA FAINI KWA KUONYESHA FULANA YA MANENO YA KUMSHUKURU MANDELA - DROGBA ASEMA HAJALI NA AKIPATA NAFASI ATARUDIA TENA

Kenya yaanza njama kwa Kili Stars

Mombasa.Wenyeji Kenya wameingia mchecheto na makali ya Kilimanjaro Stars baada ya kulazimisha mchezo wa nusu fainali ufanyike Machakos badala ya Mombasa.

Kocha wa Azam aenda likizo

Dar es Salaam.Kocha mpya wa Azam, FC Joseph Omog ameondoka nchini mwishoni wa wiki kuelekea Cameroon na kumwachia majukumu msaidizi wake Kali Ongala.

Huyu ndio Mshindi wa Project Fame 2013




Irakoze Hope

HUYU NDIYE MCHUMBA WA MBWANA SAMATTA,ANAITWA SANDRA FRIEDRICH,tazama picha hapa.










HELIKOPTA YATUA UWANJANI BRAZIL KUBEBA MAJERUHI



HELIKOPTA ilitu uwanjani kubeba majeruhi baada ya kutokea vurugu katika mechi ya soka Brazil jukwaani baina ya mashabiki.