Pages

ELIMU KWANZA.

ELIMU KWANZA.
FEDHA SIO KIPAUMBELE CHETU.

Friday 13 December 2013

Lulu: Nadhani sihitaji simu ya mkononi



Elizabeth Michael maarufu Lulu.PICHA|MAKTABA
Na Herieth Makwetta,Mwananchi
Akiongea na Starehe, Lulu alibainisha kuwa kwa siku hupigiwa simu zisizokuwa na idadi na zisizo na faida kwake, lakini akakiri kwamba idadi kubwa ya watu wanaompigia simu ni mashabiki wake.
Mwigizaji anayefanya vizuri sokoni kwa sasa,Elizabeth Michael maarufu Lulu, amesema kuwa hatamani tena kutumia simu ya mkononi kwani amekuwa akisumbuliwa na watu wasiokuwa na mambo ya msingi ya kumweleza wanaompigia simu mara kwa mara.
Alisema kuwa kero hiyo humfanya atamani kurudi katika enzi za kale za kuwasilia kwa kutumiana barua kwa njia ya posta.“Nadhani sihitaji simu ya mkononi kwa sasa, mwenye shida na mimi atanitumia barua. Sijui, hata sijielewi nikasimame wapi, maana hata nikibadili nambari ya simu inasambaa kwa kasi sana,”alisema.


Akiongea na Starehe, Lulu alibainisha kuwa kwa siku hupigiwa simu zisizokuwa na idadi na zisizo na faida kwake, lakini akakiri kwamba idadi kubwa ya watu wanaompigia simu ni mashabiki wake.


“Ninapigiwa simu nyingi kwa siku ambazo ni kero kwangu, nafurahi sana ninapopigiwa simu na shabiki wangu, lakini wapo wanaopiga simu kutaka mambo ya ajabu. Sawa ni wengi wao ni mashabiki wangu, lakini simu kwangu ni kero kubwa ingawa ni msaada mkubwa pia kwangu ni sehemu ya kitendea kazi,” alisema.

No comments:

Post a Comment