Pages

ELIMU KWANZA.

ELIMU KWANZA.
FEDHA SIO KIPAUMBELE CHETU.

Wednesday, 11 December 2013

Kipigo cha Kili Stars chamuibua Ndolanga

ALIYEKUWA Mwenyekiti wa kilichokuwa Chama cha Soka Tanzania (FAT, sasa TFF), Muhidin Ndolanga, amesema chombo hicho chini ya Rais Jamal Malinzi hakitapata mafanikio kutokana na uwepo wa mabaki ya uongozi uliopita chini ya Leodegar Chilla Tenga.

Ndolanga aliyasema hayo juzi jijini hapa, baada ya Stars kufungwa 1-0 na Kenya katika dakika ya nne.

Alisema kutokana na uwepo wa mabaki ya Tenga katika timu na shirikisho hilo, itakuwa vigumu kupata mafanikio hadi pale mizizi yote itakapong’olewa.

“Unajua ni kitendo cha aibu, haiwezekani timu ikafungwa dakika ya nne, kisha inashindwa kurudisha ndani ya dakika 86, bado kuna elementi za Tenga, zinatakiwa kuondolewa mara moja, sio hali ya kawaida hii,” alisema.

Ndolanga mingoni mwa Watanzania waliokerwa na matokeo hayo ya Stars, alikuwepo katika michuano hii tangu ilipoanza Novemba 27.

Tenga aliyeingia madarakani kwa mara ya kwanza Desemba 27, 2004, alimaliza muda wake Oktoba 27, akimpisha Malinzi aliyembwaga Athumani Nyamlani.

Ndolanga kiongozi aliyesifika kwa uamuzi wake mgumu, hasa anapoamua kusimamia jambo, alisema japo ni kazi ngumu, uwepo wa masalia ya Tenga ni hatari kubwa.

Tangu aingie madarakani, Malinzi amefanya mabadiliko kadhaa yakiwemo ya kuvunja na kuunda upya kamati mbalimbali pamoja na kumpa likizo ya malipo aliyekuwa Katibu Mkuu wa Shirikisho hilo, Angetile Osiah.

Wakati hayo yakiendelea, kukawa na habari kuwa uongozi huo mpya ulipanga kupangua idara nyingine zikiwemo za Kurugenzi ya Ufundi, Mashindano na Masoko.

No comments:

Post a Comment