Pages

ELIMU KWANZA.

ELIMU KWANZA.
FEDHA SIO KIPAUMBELE CHETU.

Monday 9 December 2013

CRISTIANO RONALDO AZUNGUMZIA UGUMU WA KUNDI WALILOPANGWA URENO KOMBE LA DUNIA - ASEMA ALIKUWA AMELALA WAKATI RATIBA INAPANGWA


Katika droo ya kupanga makundi ya kombe la dunia iliyofanyika Ijumaa iliyopita ulimwengu ulishuhudia kikosi cha Paul Bento kikipangwa katika kundi gumu la (Group G), kwa pamoja na Ujerumani, Ghana na USA - kundi pekee lenye timu zote nne zilizopita kwenda kwenye hatua ya mtoano katika michuano iliyopita ya kombe la dunia 2010.
Nahodha wa Ureno, akiongea mbele ya wachezaji wake wa Madrid, Marcelo, Karim Benzema, Luka Modric, Angel Di Maria na Iker Casillas jana jumapili alisema kwamba hakuangalia droo hiyo moja kwa moja lakini alikuwa ana ufahamu changamoto ngumu nchi yake ilizokuwanazo mapka kuweza kuingia katika hatua ya 16 bora kwenye mashindano yaliyopita.
"Kiukweli, sikuangalia moja kwa moja droo ile," Ronaldo alisema. "Nilikuwa nimelala. Ni kundi gumu pamoja na Ujerumani, ambao ni moja ya timu zinazopewa nafasi kubwa kutwaa ubingwa, na USA pamoja na Ghana, ambazo ni timu nzuri pia. Kufuzu kwenda hatua ya pili ni kipaumbele cha kwanza na tutaona kitakachotokea. Tunaweza kabisa kufuzu kwenye kundi lile, lakini kujiamini na umakini ni vitu muhimu. Inategemea na sisi kama timu. Ninatumaini Ureno inaweza kufika mbali."
Hat trick ya Ronaldo katika mchezo wa kugombea kufuzu dhidi ya Sweden uliwahahkikishia Ureno nafasi ya kufuzu kwenda Brazil, lakini hakujihisi kuwa na mzigo wowote mabegani mwake kama kiongozi wa timu uwanjani.
"Malengo yangu siku zote yamekuwa yale yale. Kujaribu kufanya kila kitu kuisadia nchi yangu. Binafsi mara zote nimekuwa nikijitahidi kwa ubora wangu wote kucheza kwa juhudi, kufunga mabao na kujitoa kwa yote."
Mshambuliaji huyo pia kasema kwamba hajamuuliza nahodha wake wa Real Madrid na timu ya taifa ya Spain Iker Casillas inakuwaga namna gani pale unapopata nafasi ya kubeba kombe la dunia, lakini anadhani kwamba ni jambo la aina yake kama alivyojisikia wakati aliposhinda kombe la ubingwa wa ulaya na Manchester United mwaka 2008.
"Sihitaji kumuuliza. Nina akili, nafahamu umuhimu wa kubeba mataji muhimu. Kwenye level ya klabu, nafahamu namna inavyokuwa kubeba ubingwa wa Champions League na ninaamini kubeba ubingwa wa kombe la dunia ni jambo zuri zaidi. Ndoto ambayo wachezaji wenzangu na mimi tunayo ni kubeba ubingwa wa kombe la ulaya na dunia kwa kwa ajili ya nchi yetu, lakini inabidi tuweke miguu chini na kujituma kutimiza ndoto zetu. Ni timu bora pekee zinazoweza kushinda na ninaamini kwamba Ureno inaweza kuwa moja ya timu bora."

No comments:

Post a Comment