Pages

ELIMU KWANZA.

ELIMU KWANZA.
FEDHA SIO KIPAUMBELE CHETU.

Saturday 14 December 2013

Hii ndo misukosuko iliyojitokeza kwenye utengenezaji wa nyimbo ya Rich Mavoco


Mara nyingi kunatokea vitu vingi sana kwenye maisha ya kimuziki ambavyo huwa hatuvifahamu na vingine hatudhani kama vinaweza kutokea.

Prodyuza kutoka Mazuu Records,Mazuu mwenye hits kadhaa kama Kidela ya Abdul Kiba,I love u ya Kassim Mganga Nakomaa na jiji ya Shilole na Roho yangu ya Rich Mavoco.kaelezea mazingira magumu aliyokutana nayo wakati wa utengenezaji wa nyimbo ya Roho yangu ya Rich Mavoco.‘Aah kwakweli nyimbo ya Richard kulingana na usumbufu uliokuwepo ilinichukua mwezi mzima,,kwa sababu kila nikifanya file linafutika kwenye computer inabidi nichukue back up cd yani computer ilipata degedege kama wiki hivi haifanyi kazi vizuri,mpaka ikafika mahala nikamwambia usikanyage studio kwangu hebu kaa kando kwanza nijaribu kufanya mimi peke yangu nione itakuwaje lakini pamoja na kwamba nilifanya peke yangu bado ikawa haikidhi,bahati nzuri siku hyo zilibaki siku 3 kuachia ile ngoma akanifata akanambia Mazuu hebu leo tujaribu maana nimekuja bila taarifa kweli nilitumia kama masaa mawili hivi kuifanyia mastering ile nyimbo’.

‘mbilinge lilikua kubwa sana maana Richard alikua kila akifika studio lazima computer zizime au umeme ukatike,siku moja akaja kuchukua data file akasema kwa sababu wewe ulishapitia mixing acha nimpelekee master jay kidogo ajaribu kutupa baraka zake tuone kuna nini,siku aliyompelekea master jay file lile master jay akamwambia nitaisikiliza kwa muda wangu,siku ambayo ametoa taarifa kwenye vyombo vya habari kwamba nyimbo inatamabulishwa juma5 basi akaja juma 3 akanipigia simu anakuja studio ile anafika tu studio hapa nyimbo zikawa zimefutika zote kwenye computer ananikuta mi nimekaa tu,ananiuliza nini nikamwambia hapa file zote zimefutika lakini najua hiki kikwazo ni wewe tu,nikamwambia mpigie master jay akupe ile data file ili tumalizie,alipompigia akamjibu yuko njian anaenda kwenye Ebss akamwambia cd amempa man water kwa hiyo aende kwa man water kuichukua,ikabidi Rich akaifate, bahati nzuri akaipata akaja nayo studio ile anakuja nayo studio tu computer nayo ikagoma kufanya kazi,ikabidi nimpige stop nikamwambia bwana wiki hii nzima sitaki kukuona hapa’

‘Nyimbo ikabaki story kwenye media kwamba inatambulishwa leo mara kesho,siku moja rich alikuja tu bila taarifa akasema mazuu nimekuvumia hapam nachohitaji muda huu tufanye mixing akasema mazuu plz naomba tufanye leo,ikabidi nikubali pale bahati nzuri huwezi amini ndani ya masaa mawili ikawa imeisha na ikawa tayari asa sijui mwenyewe alipita wapi’.

No comments:

Post a Comment