Pages

ELIMU KWANZA.

ELIMU KWANZA.
FEDHA SIO KIPAUMBELE CHETU.

Saturday 11 January 2014

UGANDA BINGWA NETIBOLI KOMBE LA MAPINDUZI 2014

Na Zaituni kibwana, Zanzibar
TIMU ya Taifa ya netiboli ya Uganda ikiwa chini ya nahodha wake, Peace Proscocia, leo imefanikiwa kutwaa ubingwa wa michuano ya Kombe la Mapinduzi baada ya kuifunga Tanzania Bara magoli 52-39.
Mchezo huo wa fainali umefanyika leo jioni jijini hapa kwenye Uwanja wa Gymkhana visiwani hapa.
Kikosi hicho cha kina dada wa Uganda kilianza vyema michuano hiyo baada ya kuanza kuwa mbele kuanzia robo ya kwanza ya mchezo huo kwa kumaliza wakia na magoli 11-9.

Mwenyekiti wa Baraza Wawakilishi, Mgeni Hassan Juma kulia akimkabidhi Nahodha wa Uganda, Peace Proscovia Kombe la Mapinduzi ubingwa wa Netiboli 2014 jioni ya leo Uwanja wa Gymkhana, Zanzibar. Uganda iliifunga Tanzania Bara 52-39.

Ushindi huo wa awali uliwapa morari wachezaji hao na kufanya hadi mapumziko kutoka kifua mbele kwa mabao 24-20.
Hadi mwamuzi anamaliza mchezo huo, Uganda ilikuwa kidedea kwa mabao 52-39 huku nahodha wao Peace akitwaa tuzo ya kuwa mfungaji bora wa michuano hiyo.
Kufuatia ushindi huo, Mwenyekiti wa Baraza la wawakilishi, Mgeni Hassani Juma aliipatia timu hiyo kombe la michuano hiyo.
Licha ya Uganda kutwaa ushindi huo, Tanzania Bara chini ya mfungaji wake Mwanaidi Hassan ilitwaa nafasi ya pili ya michuano hiyo.
Mchezaji Bora wa michuano hiyo ni Betina Kazinja kutoka Tanzania Bara, Mwajuma Hilika kutwaa mlinzi bora wa michuano hiyo.

Peace Proscovia akidaka mpira mbele ya wachezaji wa Tanzania Bara


Mchezaji wa Tanzania, Sofia Komba akidaka mpira mbele ya wachezaji wa Uganda


Mwanaidi Hassan wa Tanzania Bara akidaka mpira pembeni ya wachezaji w Uganda


Mwanaidi kulia na mchezaji wa Uganda


Sofia Komba alicheza sana leo kujibu mapigo ya mpenzi wake, Joseph Owino aliyeifungia Simba SC bao jana katika ushindi wa 2-0 kwenye soka dhidi ya URA

No comments:

Post a Comment