Pages

ELIMU KWANZA.

ELIMU KWANZA.
FEDHA SIO KIPAUMBELE CHETU.

Wednesday 8 January 2014

CHEKA KUZIPIGA NA MRUSI FEBRUARI DAR

Na Dina Ismail, Dar es Salaam
BONDIA Francis Cheka, anatarajiwa kupanda ulingoni Februari 8, mwaka huu kuzipiga na bingwa wa zamani wa WBA, Mrusi Valery Brudov katika pambano la uzito wa Light Heavy, ambalo bado haijafahamika kama litakuwa la ubingwa au la.
Cheka anataka kurejesha heshima baada ya hivi karibuni kupigwa na Fedor Chidinov nchini Urusi na kupokonywa taji lake la WBF, alilolipata Agosti mwaka jana kwa kumchapa Phil Williams wa Marekani mjini Dar es Salaam.

Cheka akimuadhibu Mmarekani, je ataendeleza ubabe wake Dar?

Akizungumza na Waandishi wa Habari mjini Dar es Salaam jana, Promota wa pambano hilo, Jay Msangi ambaye pia alikuwa promota wa pambano la awali alisema, ameamua kumuandalia Cheka pambano hilo kali pia ili aweze kuendelea kujenga rekodi yake kikamilifu.
Msangi alisema, pambano hilo linatarajiwa kufanyika katika ukumbi wa PTA, Sabasaba mjini Dar es Salaam siku hiyo.
“Bondia huyu (Brudov) ana uwezo mkubwa sana nchini kwao, amecheza mapambano 42 kashinda 39, kati ya hayo 28 ameshinda kwa KO na amepoteza mitatu tu,”alisema Msangi na kuongeza kuwa.

No comments:

Post a Comment