Pages

ELIMU KWANZA.

ELIMU KWANZA.
FEDHA SIO KIPAUMBELE CHETU.

Wednesday 11 December 2013

Kocha mpya Simba awaweka kiporo majeruhi

Dar es Salaam. Baada ya kuwapinga panga wachezaji tisa, Kocha wa Simba, Zdravko Logarusic amewaweka kiporo wachezaji wanne ambao ni majeruhi.
Wachezaji waliowekwa kiporo ni Miraji Adam, Ibrahim Twaha, Abdallah Seseme na Nasoro Masoud ‘Cholo’ kabla ya kutoa msimamo wake wa mwisho kama wabakizwe au wafungashiwe virago.

Chanzo cha habari cha kuaminika kutoka ndani ya klabu ya Simba kililiambia Mwananchi jana kuwa, Logarusic amekwama kutoa uamuzi kuhusu hatma ya wachezaji hao hadi pale watakaporejea kwenye mazoezi ya kikosi chake.
“Chollo, Miraji Adam, Seseme na Twaha kocha hajatoa uamuzi wowote kama wabaki au waondoke hadi pale atakapowaona mazoezini kwa vile kwa sasa ni majeruhi hajui hata sura zao,” kilisema chanzo hicho na kuongeza:
“Lengo la kufanya hivi ni kuhakikisha kama mtu anaondolewa basi iwe ni kwa haki na siyo kwa kumwonea ndiyo maana anafanya mambo kwa umakini mkubwa.”
Wachezaji ambao tayari Logarusic amebariki wasitishiwe mikataba na wengine watolewe kwa mkopo ni makipa Abel Dhaira na Andrew Ntalla, Frank Sekule, Rashid Mkoko, Marcel Kaheza, Ramadhan Kiparamoto, Sino Agustino, Emily Mgeta na Hassan Isihaka. Ambao wapo kwenye kundi la kusitishiwa mikataba ni Dhaira na mwenzake Ntalla na Sino Augustino wakati walio katika mpango wa kutolewa kwa mkopo ni Rashid Mkoko, Marcel Kaheza, Ramadhan Kiparamoto, Emily Mgeta na Hassan Isihaka.

No comments:

Post a Comment