Pages

ELIMU KWANZA.

ELIMU KWANZA.
FEDHA SIO KIPAUMBELE CHETU.

Sunday 12 January 2014

MAN CITY YAREJEA KILELENI LIGI KUU ENGLAND, MWAKA HUU KAZI IPO

MABAO ya Edin Dzeko na Alvaro Negredo yametosha kuipa ushindi wa 2-0 Manchester City dhidi ya Newcastle Uwanja wa St James Park na kurejea kileleni mwa Ligi Kuu England.
Nyota wa Bosnia alifunga bao la kwanza dakika ya nane akiunganisha krosi ya Aleksandar Kolarov kumtungua kipa Tim Krul.
Kikosi cha Alan Pardew kilidhani kimepata bao la kusawazisha baada ya shuti la mbali la Cheick Tiote kumpita kipa Joe Hart na kutinga nyavuni, lakini likakataliwa kwa sababu Yoan Gouffran alikuwa ameotea.
Negredo akaifungia City bao la pili dakika za majeruhi. Ushindi huo unaifanya City irejee kileleni baada ya kutimiza pointi 47 kutokana na mechi 21, ikiishusha Chelsea yenye pointi 46 baada ya kucheza mechi 21 pia katika nafasi ya pili. Arsenal sasa ni ya tatu kwa pointi zake 45, ingawa imecheza mechi 20.


Kazi nzuri: Mshambuliaji wa Manchester City, Edin Dzeko (kulia) akimtungua kipa wa Newcastle, Tim Krul kuifungia bao la kwanza timu yake

Krul (kulia) hakuweza kuuzuia mchomo wa Dzeko

Dzeko akikimbia kushangilia baada ya kufunga

Anapongezwa na wenzake

No comments:

Post a Comment